TANZIA Demi Agoglia Afariki Dunia Wakati Akifanyiwa Upasuwaji Wa Kuongeza Shepu

TANZIA Demi Agoglia Afariki Dunia Wakati Akifanyiwa Upasuwaji Wa Kuongeza Shepu

Nimeshtuka sana nikajua nimpendae Demi ndo hivo tena. Naomba tu mods wakupige ban japo hauna kosa, umezua taharuki.
 
Mwanamke wa Uingereza aitwaye Demi Agoglia (26) amefariki dunia siku chache baada ya kufanya upasuaji wa kuongeza shepu (BBL) nchini Uturuki, Magazeti ya Uingereza yameripoti.

Demi ambaye alikua Mkazi kutoka Jiji la Manchester alipata mshtuko wa moyo saa chache kabla ya kuanza safari yake ya kurudi nyumbani Uingereza ambapo Mume wake alimpatia huduma ya dharura ya CPR kabla ya kumpeleka Hospitalini lakini jitihada zake hazikuzaa matunda.

Inaelezwa kwamba kiwango cha vifo vinavyotokana na upasuaji wa kuongeza makalio (BBL) ni kifo kimoja kati ya kila Watu 3000 ambapo upasuaji huo wa BBL ndio upasuaji wenye kiwango cha juu zaidi cha vifo vilivyorekodiwa kuliko upasuaji mwingine wowote wa urembo.

Upasuaji wa kuongeza makalio unakadiriwa kugharimu £3,500 (Tsh milioni 11.1) nchini Uturuki lakini hadi £10,000 (Tsh milioni 32) nchini Uingereza huku utafiti ukionesha kuwa ndio upasuaji hatarishi zaidi kuliko upasuaji mwingine wowote wa urembo.

Chanzo: Millard Ayo
Acha kuparaza roho zetu! Nilifikiri ni Demi wetu afariki bila na mimi kuonja kitumbua chake! Hii ingekuwa dhuluma ya hali ya juu
 
Kweli kabisa,nimekaa chini na kuiweka simu kifuani nimefungua picha yako moyo ukiwa unaenda mbio na kupata maumivu ila nikakumbuka kurudi kusoma upya ili nipate uthibitisho huku mikono ikiwa inatetemeka na kutokwa jasho jingi,Ahsante Mungu bado unapumua.
🤣🤣🤣🤣🤣Jamani ni habari za msiba ila zimenichekesha
 
Back
Top Bottom