Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Mkuu umetoa mfano ambao sio relevant. JPM alikuwa Rais, alijitoa akiwa kama Rais. Baada ya kufariki familia yake inatunzwa, inalindwa na Mke wake kila mwezi anapokea 80% ya mshahara wa JPM pamoja na marupu rupu mengine.Mzee hakuna changes bila sacrifices, sehemu yeyote unapoona mabadiliko huwa yanakuja na gharama thus why hata JPM hayupo leo. He was striving for changes japo hakuishi muda mrefu ila leo hii treni inatembea bwawa la Nyerere limekamilika na tunatembea kwenye 8 lane road inayoamzia Kimara mwisho to Kibaha. Hizo ni faida za mapambano yake japo yeye hayupo ila familia yake inafurahia matunda hayo.
Turudi kwa akina sisi tusiojulikana na system. Ujitoe muhanga kwenye maandamano, upigwe risasi ufe, lakini maandamano yalete tija mabadiliko yatokee. Je, ni nani atakayekukumbuka? Ni nani atakayewatunza watoto wako na Mkeo?
Nikupe mfano mzuri, kule Tunisia walikufa watu kwenye maandamano yaliyoleta mabadiliko ya Serikali, baada ya mabadiliko hao waandamanaji walio kufa familia zao zimepata nini?
Je, Serikali iliyopo madarakani imewakumbuka kwa kuzijali familia walizoacha??
Jibu ni dogo sana, "hakuna anayewakumbuka". Wamesahaulika katika makaburi ya "sahau".
Ndiyo maana nimeuliza tena, unaandamana na kupoteza maisha kwa faida ya nani????