Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NIT wanafundisha kuwa,kwenye zebra unasimama endapo kuna waenda kwa miguu walio tayari kuvuka.Sio mtu anamaongezi na wenzake au anaongea na simu unamlazimisha avuke kisa umemuona eneo la zebra.Wala usimlaumu. Waliolikoroga sana suala hili ni traffic police wenyewe. Kama unakumbuka mwaka juzi walianzisha kampeni kubwa ya kukamata madereva wanaovunja sheria kwenye zebra.
Mambo makubwa mawili ambayo wao wenyewe traffic waliyashikia bango kama makosa na kuleta mkanganyiko sana ni;
1. Ni lazima kusimama kwa muda kwenye zebra(zisizo na taa) hata kama hakuna mwenda kwa miguu anayetaka kuvuka.
2. Kuwasha hazard unaposimama kwenye zebra.
Madereva wengi tu walipigwa faini kwa makosa haya na lilileta mjadala mkubwa nchini hata hapa JF.
Lakini baadaye wao wenyewe traffic wakasema siyo kosa na wengine kuacha kukamata kimya kimya. Nilichogundua hata traffic wenyewe wengi hawajui sheria za barabarani zote na mara nyingi wanafuata mkumbo. Nakumbuka wanasheria wengi waliingilia kati na kusema ni makosa.
... hawaelewagi Mkuu; wanachojua ni hesabu tu basi.You are absolutely right. Nadhani dawa ni kuwa muungwana na kumueleza changamoto nadhani kamanda ataelewa tu. Sheria inapaswa iendane na hekima katika kutafsiri.
... Jeshi la Polisi wanapaswa ku-sync na taasisi kama hizi. Inaoenekana kinachofundishwa ni tofauti na trafiki wanachojua au ku-practice.NIT wanafundisha kuwa,kwenye zebra unasimama endapo kuna waenda kwa miguu walio tayari kuvuka.Sio mtu anamaongezi na wenzake au anaongea na simu unamlazimisha avuke kisa umemuona eneo la zebra.
Hairuhusiwi kumlazimisha mtu kuvuka iwe kwa kumpigia honi au kumpigia kelele za mdomo.
Kusimami ilimradi umeiona zebra hata kama hakuna anayevuka wakati mwingine inasababisha ajali
endapo mnakuwa kwenye speed na dereva wa nyuma yako hajaweka nafasi inayotakiwa baina yako na yeye.
Suzuki carry huwa haipiti bila kusimamishwaNdugu gari yako ni aina gani?
Kama una suzuki carry au lori
jaribu kuliendesha siku moja uone tunachozungumza hapa.
Mimi nikiendesha gari nyingine kwa kweli nakumbuka nilisimamishwa nikiwa naenda mkoani tena
kwa mambo ya speed,basi lakini endesha suzuki carry liwe na kila kitu kimekamilika hata ile simamishwa simamishwa tu
inakufanya siku nyingine usiliendeshe maana uwe na uhakika utachelewa huko uendako.
Kwani unafikiri hiyo hekima hawana? Wanayo ila tatizo njaa ndugu, lazima afosi kingi hata kama huna kosaYou are absolutely right. Nadhani dawa ni kuwa muungwana na kumueleza changamoto nadhani kamanda ataelewa tu. Sheria inapaswa iendane na hekima katika kutafsiri.
Hii double sijui watu wanaitolea wapi, huwa nakwazika mtu akisema 'double hazard'.Hakuna double hazard kuna hazard
Hayo yote nakuwa nimeyafanya Mkuu tatizo mstari utaishia wapi?
Mimi pia ni muhanga wa hili mkuu, jamaa ni wapuuzi sana. Ila binafsi nilishasema sitoi hata jero kwa trafiki, yeye akubali tu kunionya au kuniandikia.Na mimi naomba kuchangia. Mko njia kuu nje ya mji kwa mfano nje ya 50; mbele kuna milori kadhaa imetangulia mwendo mdogo sana. Unayafuata taratibu ukisubiria upate sehemu inayokuruhusu ku-overtake.
Mungu si Athumani, unaruhusiwa ku-overtake bila hiana mbele kweupe unaingia kulia. Lol! kumbe msafara mrefu kiasi, hamad, dotted line imefikia mwisho huwezi kurudi kushoto kwa sababu kuna gari; unakanyagia ili ulimalizie lile lori then unarudi kushoto tayari ulishavuka dotted line.
Duh! Balaa, kumbe walikuwa wamejificha mahali, ghafla wanaibuka barabarani unawekwa pembeni. Michezo hii ipo sana Kibaha - Mlandizi na Dumila - Gairo. Jamani, tukienda kiuhalisia hapo kosa langu ni lipi?
Kumbuka mstari wa kuniruhusu ku-overtake unapoanzia sijavaa darubini ili nijue unaishia wapi; ni hadi mita chache kabla ya unapoishia ndipo napoweza kugundua unaishia pale; siwezi kurudi kwa sababu kushoto kuna gari.
This is a very stupid regulation; nilishapigwa sana mabao ya aina hii. Sheria (I think rule) hii ilitakiwa izingatie zaidi ulipotokea/ingilia na sio pale dereva alipomalizia kutokana na changamoto niliyoileza hapo juu. Wahusika waliangalie hili.
8. Traffic haruhusiwi kuchomoa funguo ya gari anatakiwa achukue number ya gari tu endapo utakimbiaWadau wenye usafiri tuweze shirikishana mambo mbalimbali ambayo madereva wanapaswa kuzingatia barabarani hasa kwa upande wa Haki na Wajibu wao.
Na sisi tusio na magari pia tutapata darsa hapa.maana nakumbuka miaka ile sisi tunasoma tulijifunza kwenye Geography Kilimo cha Mahindi USA lakini hatukuwa wakulima.
Napenda tuweze shirikishana mambo kadhaa hasa Dereva anapokamatwa na Traffic au anapofanya kosa. Kwa wenye uelewa hasa kwa kuzingatia Sheria tuelekezane haya.
1. Dereva anapokuwa hana leseni (amesahau kubeba) sheria inamtaka ai present/wasilishe kwa traffic ndani ya masaa 72. Wakati huo je ataondoka na gari yake au gari itakuwa kituo cha polisi? Mfano umekamatwa kwa kosa au ktk ukaguzi.ukagundua hukubeba leseni. Nini kinafuata?
A. Je unamwachia gari?(unaacha na funguo/au unaondoka nazo)
B. Unaondoka na gari anabaki na namba za gari
C. Gari unaipeleka kituo cha polisi
2. Je ni sahihi mtu kuwasha hazard anaposimama kwenye zebra/alama ya pundamilia ili na wenzie nao wasimame?ni kwa mujibu wa sheria?
3. Je mtu anapovuka kwenye junction ni sahihi kuwasha hazard kuonesha kuwa ananyoosha na haingii kulia wala kushoto?
4. Inapotokea mtu yupo kwenye foleni ya mataa taa ikabadili njano then red akiwa katika mwendo amefika katikati ya barabara tayari.je asimame arudi nyuma au amalize kuvuka. Anapokamatwa na traffic aandikiwe au aonywe?
5. Ni makosa gani ya dereva ambayo akifanya anaweza elimishwa tu na asiandikiwe na anaweza goma kuandikiwa kisheria kabisa bila kuonekana amemkosea traffic
6. Je traffic anaruhusiwa kuchomoa bima ya gari na kuondoka nayo? Kwa sheria ipi?
7. Je traffic anaruhusiwa kuchomoa plate number kuondoka nayo au kuishikilia?kwa sheria ipi?
8. Je traffic anaruhusiwa kuchomoa funguo ya gari kuishikilia?kwa sheria ipi?
9. Je traffic anaruhusiwa kubaki na kadi ya gari ikiwa huna leseni au umegoma kumpa leseni?kwa sheria ipi?
10. Ikiwa traffic kaomba leseni yako akague ukampa akakutafutia kosa ambalo hujaridhika nalo akuandikie.ufanye nini?
11. Je inawezekana traffic akakuandikia kosa bila kutumia leseni?
12. Kama hujaridhika na kuandikiwa kosa na limeshaandikwa ufanye nini?
13. Unaendesha gari imefika jioni unawasha taa. Taa moja imeungua je traffic akuandikie kosa? Ikiwa taa ilikuwa nzima before.
14. Umegongwa ukiwa parking taa imepasuka huna uwezo wa kununua taa muda huo je traffic akikukamata akundikie kosa?
15. Ni kosa lipi ambalo traffic atakuwa ONYO TU au ELIMU na kukuruhusu uondoke pasipo kudai Rushwa au Kutaka kukuandikia kosa.
Na mengine mengi sana... Tuweze kuelimishana itusaidie tunapokuwa barabarani kuepuka migogoro isiyo na faida.
NB. WAPO TRAFFIC WENYE AKILI NZUERI NA WASTAARABU SANA MPAKA UNAJISIKIA VIBAYA KWA KUKOSEA. HAO TUWAHESHIMU SANA
Ni ukweli kwamba askari wengi wana uelewa mdogo sana kuhusu sheria za usalama barabarani lakini hata wale wenye uelewa hutumia ignorance ya madereva kujipatia rushwa ama 'kutimiza malengo' ya faini wanayo wekewa na bosi zao.... Jeshi la Polisi wanapaswa ku-sync na taasisi kama hizi. Inaoenekana kinachofundishwa ni tofauti na trafiki wanachojua au ku-practice.
Na Noah kwa mikoani.Suzuki carry huwa haipiti bila kusimamishwa
Ni kosa. Abira wote wanapaswa wafunge mkandaAbiria wa kiti cha nyuma asipofunga mkanda ni kosa au sio kosa kisheria?
OkNi kosa. Abira wote wanapaswa wafunge mkanda
Dah [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] mnatuonea wamiliki wa passo jamaniJe Passo inastahili kukatiwa bima ya gari au Bajaj?
... nashukuru kwa majibu mazuri. Proper assessment inafanyika vipi kwa case niliyoielezea? Kama ndivyo, kuna haja gani ya kuweka hiyo mistari badala ya kuwaachia madereva wajifanyie assessment wenyewe?Kama mstari utaisha wakati hujamaliza kuovertake, kwa kifupi kabisa maana yake ni kuwa hukufanya proper assessment kabla, ukiadhibiwa kwa mazingira hayo haujaonewa.
Mkuu, kwanza umesoma driving school?... nashukuru kwa majibu mazuri. Proper assessment inafanyika vipi kwa case niliyoielezea? Kama ndivyo, kuna haja gani ya kuweka hiyo mistari badala ya kuwaachia madereva wajifanyie assessment wenyewe?
Hoja yangu iko hapo kwenye red; ni rahisi kuona object (gari, mnyama, mtu, n.k.) iliyoko mita kadhaa mbele lakini huwezi kuona dotted line inapoishia at the moment unaruhusiwa ku-overtake. Mfano fikiria mazingira ya usiku.Mkuu, kwanza umesoma driving school?
Kabla ya kuovertake kuna vitu vya kuzingatia:
1. Je Eneo unalotaka kuovertake ni salama na sheria inakuruhusu kufanya hivyo (hiyo mistari)?
2. Kama namba 1 ni ndiyo je utamaliza kuovertake kabla hujatoka kwenye eneo salama?
3. Unaovertake gari ngapi zenye speed na urefu wa kiasi gani?
4. Gari yako ina uwezo wa speed and power kuziovertake hizo gari?
Ukizingatia yote hapo juu huwezi kutana na hiyo hali ya kumaliza mstari wa dot kabla hujamaliza kuovertake.