Dereva fahamu HAKI na WAJIBU wako unapokutana na Traffic Barabarani kuepusha Migogoro

Rushes ya barabarani no hatari
Askari hakupi onyo ni lazima umpe buku 5 au akutolee mkeka
 
NIT wanafundisha kuwa,kwenye zebra unasimama endapo kuna waenda kwa miguu walio tayari kuvuka.Sio mtu anamaongezi na wenzake au anaongea na simu unamlazimisha avuke kisa umemuona eneo la zebra.
Hairuhusiwi kumlazimisha mtu kuvuka iwe kwa kumpigia honi au kumpigia kelele za mdomo.
Kusimami ilimradi umeiona zebra hata kama hakuna anayevuka wakati mwingine inasababisha ajali
endapo mnakuwa kwenye speed na dereva wa nyuma yako hajaweka nafasi inayotakiwa baina yako na yeye.
 
You are absolutely right. Nadhani dawa ni kuwa muungwana na kumueleza changamoto nadhani kamanda ataelewa tu. Sheria inapaswa iendane na hekima katika kutafsiri.
... hawaelewagi Mkuu; wanachojua ni hesabu tu basi.
 
... Jeshi la Polisi wanapaswa ku-sync na taasisi kama hizi. Inaoenekana kinachofundishwa ni tofauti na trafiki wanachojua au ku-practice.
 
Suzuki carry huwa haipiti bila kusimamishwa
 
You are absolutely right. Nadhani dawa ni kuwa muungwana na kumueleza changamoto nadhani kamanda ataelewa tu. Sheria inapaswa iendane na hekima katika kutafsiri.
Kwani unafikiri hiyo hekima hawana? Wanayo ila tatizo njaa ndugu, lazima afosi kingi hata kama huna kosa
 
Kama mstari utaisha wakati hujamaliza kuovertake, kwa kifupi kabisa maana yake ni kuwa hukufanya proper assessment kabla, ukiadhibiwa kwa mazingira hayo haujaonewa.
Hayo yote nakuwa nimeyafanya Mkuu tatizo mstari utaishia wapi?
 
Mimi pia ni muhanga wa hili mkuu, jamaa ni wapuuzi sana. Ila binafsi nilishasema sitoi hata jero kwa trafiki, yeye akubali tu kunionya au kuniandikia.
 
8. Traffic haruhusiwi kuchomoa funguo ya gari anatakiwa achukue number ya gari tu endapo utakimbia
 
... Jeshi la Polisi wanapaswa ku-sync na taasisi kama hizi. Inaoenekana kinachofundishwa ni tofauti na trafiki wanachojua au ku-practice.
Ni ukweli kwamba askari wengi wana uelewa mdogo sana kuhusu sheria za usalama barabarani lakini hata wale wenye uelewa hutumia ignorance ya madereva kujipatia rushwa ama 'kutimiza malengo' ya faini wanayo wekewa na bosi zao.

Kuna baadhi ya sheria zinahitaji mapitio kuendana na uhalisia.

Pia haki zaidi itatendeka kwa madereva pale jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani likiacha kutumiwa kama kitengo cha kukusanya mapato.
 
Abiria wa kiti cha nyuma asipofunga mkanda ni kosa au sio kosa kisheria?
 
Kama mstari utaisha wakati hujamaliza kuovertake, kwa kifupi kabisa maana yake ni kuwa hukufanya proper assessment kabla, ukiadhibiwa kwa mazingira hayo haujaonewa.
... nashukuru kwa majibu mazuri. Proper assessment inafanyika vipi kwa case niliyoielezea? Kama ndivyo, kuna haja gani ya kuweka hiyo mistari badala ya kuwaachia madereva wajifanyie assessment wenyewe?
 
Mkuu, kwanza umesoma driving school?
Kabla ya kuovertake kuna vitu vya kuzingatia:
1. Je Eneo unalotaka kuovertake ni salama na sheria inakuruhusu kufanya hivyo (hiyo mistari)?
2. Kama namba 1 ni ndiyo je utamaliza kuovertake kabla hujatoka kwenye eneo salama?
3. Unaovertake gari ngapi zenye speed na urefu wa kiasi gani?
4. Gari yako ina uwezo wa speed and power kuziovertake hizo gari?

Ukizingatia yote hapo juu huwezi kutana na hiyo hali ya kumaliza mstari wa dot kabla hujamaliza kuovertake.
 
Hoja yangu iko hapo kwenye red; ni rahisi kuona object (gari, mnyama, mtu, n.k.) iliyoko mita kadhaa mbele lakini huwezi kuona dotted line inapoishia at the moment unaruhusiwa ku-overtake. Mfano fikiria mazingira ya usiku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…