Kumbe dereva taxi alimchukua abiria huyu tokea KIA moja kwa moja hadi Arusha hotelini.
Tokea hotelini alikwenda nyumbani kwake ambako ana mke na watoto 4. Wote hawa alishikana nao mikono.
Tokea nyumbani siku hiyo hiyo akapata abiria 2 kuwapeleka Karatu. Huko kuna shule ya watoto yatima ambako abiria hao 2 walikuwa wakienda.
Asubuhi watoto wote 4 wa dereva walielekea mashuleni kwao ambako maisha yaliendelea kama kawaida.
Kwa maelezo ya dereva taxi, wale walioenda kwenye ile shule wameshapatikana kule kwenye shule ya watoto yatima, lakini maisha yalishaendelea kama kawaida.
Hicho ndicho kipimo halisi cha mnyororo wa huu ugonjwa Corona ambao WHO imeuita kuwa ni janga la kimataifa.
Source: BBC Swahili leo.
Kwenu serikali, pasipo na kupepesa maneno hapa "inatakiwa kuwepo mkakati kamili sasa na kwa dharura kweli, si mkakati nusu nusu tena."
At this stage, "we urgently need a total strategy. A partial strategy is not an option anymore."