Dereva wa basi la Mtei Express auawa na madereva wa malori kutoka Rwanda

Mfano mimi abiria nishuke nianzishe vurugu je dereva anaweza kushuka kuja kunisaidia? Au atawasha gari aondoke na kuniacha? Nimewaza tuu.
 
Hawakuona wala kuingilia?
Angalia clip hio huyo muuaji anaonekana anazunguka na Chuma hilo baadhi ya abiria wapo pembeni hapo au huoni Jamaa anakata roho abiria wamevurugwa angalia tena clip vizuri au unaogopa?
 
Dereva wa lori,wangeakuwa angalau kuanzia mika 40 na kuendelea.
Hakuna Kampuni ya maroli inayochukua miaka 25 ni kuanzia Miaka 35 kuendelea na uwe na uzoefu Miaka isiyopungua 5/6 ndio wanakupa kazi, Kampuni nyingi ndio ipo hivyo kwa hio muuaji kilichosababisha aue sio umri
 
Mambo yamebadilika sana siku hizi.

Mtu anaweza akapigwa hadharani mchana kweupe mbele ya umati wa watu na hakuna atakayekuja kumsaidia/kumnusuru.

Hii hali nimeiona sehemu kadhaa sasa hapa duniani. Si Tanzania tu.

Tena mbaya zaidi, badala ya watu kutoa msaada, kila mmoja wao atatoa simu yake na kuanza kurekodi huku wakishindana nani atakuwa wa kwanza kurusha kwenye mitandao ya kijamii.

Hali imekuwa tofauti kabisa.

Zamani haikuwa hivyo. Mimi nakumbuka kabisa ilikuwa ikitokea ugomvi wa kupigana, watu [strangers] walikuwa wanaingilia kati na kuamulia ugomvi.

Siku hizi cha muhimu siyo utu. Cha muhimu ni mitandao ya kijamii na ‘likes’ zake.

Binafsi nimebadili kabisa mentality siku hizi.

Nikiwa kwenye public, najichukulia kama nipo mwenyewe tu.
 
na ana sifa za kijinga kujiona anajua kuendesha sana. Hivyo,angekuwa na akili timamu,akimuona mwenzie yuko lafu,kumuacha kwani kitendo cha dakika ngapi?
Alieenda kumwambia mwenzie unaendesha lafu ni dereva wa bus sio dereva wa Lori, kitendo cha dakika ngapi huku umebeba roho za zinazokulalamikia dereva huyo mwenye Lori anataka kutuua?
 
Kabisa mkuu, bora kuamini upo mwenyewe hata kama umezungukwa na watu.
 
jifunzeni uungwana, ubabe usio na kichwa wala miguu matokeo yake ndio haya unauawa watu wanaanza kulaumu abiria kwanini hawakuingilia.
 
✍️✍️
 
jifunzeni uungwana, ubabe usio na kichwa wala miguu matokeo yake ndio haya unauawa watu wanaanza kulaumu abiria kwanini hawakuingilia.
Kwa hio angemuacha tu aue tu abiria walio kwenye Gari na Lori lake? Maana it was do or die fanya au ufe ushaelewa angezembea yule Muhuni alidhamilia kuua abiria ndio maana kamuua dereva kwa kukwamisha mpango wake
 
Wanyama ndio wanaopigana hovyo. Kama una akili timamu tumia busara na sio kupigana ukitegemea watu wengine waingilie. Pigana kufa at your own risk.
 
Kwa hio angemuacha tu aue tu abiria walio kwenye Gari na Lori lake? Maana it was do or die fanya au ufe ushaelewa angezembea yule Muhuni alidhamilia kuua abiria ndio maana kamuua dereva kwa kukwamisha mpango wake
Alishaepusha ajali, angeenda mbele akawapa taarifa askari wakamsubiri huko. Kuzuia lori na kuanza kupigana kumesaidia nini sasa?
 
Nani kakwambia Hao madereva wa roli ni watutsi? Inaweza kuwa wabongo wenzetu, kuna wabongo wana roho mbaya sana.
Loli la Rwanda hao ni wanyarwanda wana roho chafu ya kuuana kwao kuua mtu ni kama kuua kuku genocide ni kielelezo tosha
 
Wanyama ndio wanaopigana hovyo. Kama una akili timamu tumia busara na sio kupigana ukitegemea watu wengine waingilie. Pigana kufa at your own risk.
Wewe umewahi hata kuendesha Gari ukayaona madudu ya madereva barabarani au unaropoka ropoka tu, yeye kaenda kuzungumza nae km dereva mwenzie sio ugomvi na ubabe nyinyi ndio mnakuza mambo na kumfanya marehemu km ana makosa wakati alichokifanya kwa Usalama wa abiria ni sahihi au ulitaka wafe abiria zaidi ya 30 ndio ufurahi hivi kumbe kuna watu ni Mazuzu humu Jukwaani halafu wanajiona ni GT?
 
Wanyama ndio wanaopigana hovyo. Kama una akili timamu tumia busara na sio kupigana ukitegemea watu wengine waingilie. Pigana kufa at your own risk.
Hoja hapa si waliopigana, ni unyumbu wa wanaotazama wakirikodi. Unadhani hiyo tabia ya kutazama na kurikodi inaishia kwa wapiganaji tu, hata ukavamiwa na fisi akaanza kukurarua nyumbu watarekodi utafunwe kila kitu huku wakiambatanisha na emoji za masikitiko.
 
Ntakupa scenario moja:

Kuna Jamaa walikua wanapita sehemu wakasikia Mwizi Mwizi Jamaa wakaliunga mpaka pale kwenye wakamshushia vipigo heavy mpaka akakata roho baada ya kukata roho Jamaa wakaongeza kitu kingine wakamburuta yule Mwizi mpaka kituo cha Polisi kuwakabidhi Polisi kwamba huyu ni Mwizi tumemkuta sehemu anashambuliwa na Sisi tukamuongezea kipigo, Polisi wanawaambia sawa mwekeni pale baada ya hapo anzeni kufungua mikanda suruali na Mashati yenu mna kesi ya kujibu

Hivi mpaka hapo umenielewa namaanisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…