Dereva wa Basi la Saratoga apigwa na Askari wa JWTZ

Kwa hiyo suluhisho ni kipigo?!!
 
Nikiwa na safari za kibaha, najitahidi niende mapema kabla muda wa mabasi, au nitoke baada ya mabasi kupita, jamaa wana fujo.
 
Sasa Gari ya jeshi haitakiwi ku overtake? Mbna km hii habari sijaelewa, au kuna linginee??
over take vs take over wenye hiyo tabia ni mabus au malori yanayochukua muda mrefu kuwa barabarani. Kufanya take over kwa magari ya hospital & ulinzi wa mipaka ya nchi unastahili kichapo kwani unakuwa unahatarisha usalama wa wananchi.
 
1. Huyo dereva wa basi atakuwa alizingua (kusababisha ajali).
2. Kwanini iwe dereva wa Saratoga na sio wengine?
3. Wana fujo sana barabarani madereva wa mabasi.
4. Kuna mtu asiyejua fujo za madereva wa mabasi barabarani.
5. Kwanini tutetee hao wapuzi kupata mkong'oto toka kwa wanajeshi kwa rafu zao barabarani?

My take:
Sitetei wajeda kwa walilolifanya, ila mara nyingine tuwapongeze kuwa-discipline wapuzi kama hao madereva.

Wanakera sana hao na mipuuzi sana hao ndugu zetu madereva. Tutii sheria bila shuruti na hao wajeda hawatapiga mtu.
 

Barabarani huwa tunaheshimianaga sana, na hawa watu wanaobeba abiria ni wa kuheshimu sana. Hata kama wanaweza kuwa na mauzi hapa na pale
 
Kwa maana unataka kusema askari hatakiwi kufuata sheria za kiraia? Anatakiwa kufuata sheria zote za jeshi na za kiraia.
Akiwa kwenye operation za kijeshi hatakiwi kukupa copy anaenda wapi hapo anatakiwa kuzingatia za kijeshi tu

Ni vyema kupisha gari za jeshi lolote ziwe JWTZ, polisi,magereza nk hujui kulikoni hata magereza waweza kuwa wanakimbiza gaini kulipekleka mahakamani au lupango wapishe bila wanajeshi huwezi ishi kwa amani wakati wewe uwe mwanaume au mwanamke mnafanyana na mke au mume kitandani kwa raha zenu wao hawalali kuhakikisha mko salana mnaendelea kufanyana kwa raha zenui bika adui kuvamia nchi au eneo

Mnapofanyana kwa raha zenu wako lindo. Hivyo wape heshima zao ukiona wako mbele au nyuma na magari yao wapishe

Visheria vyako vya barabarani wakiwa kwenye magari official ya jeshi shika adabu yako usilete ujuaji watakuua mchana kweupe na huna kwa kuwapekeka
 
Tusikie na Upande wa pili ,si rahisi upigwe vibao kisa ku overtake ingekuwa hivyo Route ya Lugalo watu wangekuwa wanakula vibao daily.
Niliwahi kuzingua pale, nikaambiwa nizime gari, nianze kusuma..

Kilicho nitokea nakijua mwenyewe.. ila tuliwezena maana tulipita kidogo huko, tuli ongea lugha moja
 
Madereva wa mabasi makubwa baadhi ni washenzi Sana,wanaendesha Kama vile Barabara ni ya kwao peke yao,tungesikia na upande wa pili ilikuaje
Mkuu hao wanajeshi wa Nyumbu huwajui, kuna mda wanapita upande wa kulia wa barabara na usipowapisha kazi unayo ma hamna wanachowahi cha maana zaidi unakuta anapeleka watu kazin . Infact kimewahi kutumia huo usafiri humo ndani unaweza ukaambiwa usikae na siti zipo wazi kisa tu kuna mwanamke anakuzoea afu kuna mtu mnene amekataliwa na huyo huyo mwanamke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…