Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

Dr anasema kapokea majeruhi wawili,hao majeruhi hata sura zao hazionyeshwi
 
Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinki anasema dereva huyo alifika eneo la kizuizi cha polisi akiwa kwenye mwendo mkali na hakusimama na alilenga walipokuwa wamekaa askari na askari hao walilikwepa kisha gari likaingia msituni.

Dereva alishuka katika gari na kuwafuata askari huku askari wakidhani dereva yule ana nia ya kuomba radhi kwa alichokifanya lakini haikuwa hivyo na dereva huyo alitoa kitu mwilini kinachosadikiwa kuwa ni kisu na kuanza kumshambulia askari na kumjeruhi huku akitaka kumnyang'anya silaha lakini askari alifanikiwa kumdhibiti kwa kumpiga risasi.

Askari watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.
Polisi hawa wa sasa wanaaminika kweli! Si kwamba wamempora fedha na mali alizokuwa nazo na hatimaye kuanza kuokoteza sababu za kuhalalisha dhuluma yao kwake?

Imeshazoeleka sasa na kujitokeza kwa tabia sugu pale mfu anaposingiziwa mambo ambayo hawezi kujitetea mwenyewe. Imefika kipindi ambapo jeshi letu limegeuka kuwa wakala muaminifu wa Ibilisi.
 
Waislamu wana nini na polisi wetu?? Alianza Hamza sasa Saidi anataka kutuulia askari wetu tena. Au ndio mambo ya jihadi sijui haya !!!![emoji16][emoji16]
 
Hao polisi utakuta hiyo stori wametunga tu, utakuta huyo jamaa wamemuua tu kwa makusudi kisha wanapika stori za uongo.

It seems that's one of a series of the trigger happy police force engaging in extra judicial killings of innocent people before wrongly implicating the victims with a non-existent crime.
 
Asee nimeiona hii habari hapa ITV. Kwamba dereva alitaka kuwagonga polisi kwa gari na baada ya wao polisi kukimbia gari ikagonga kichaka kisha dereva akashuka na kitu kama kisu kutaka kuwashambulia polisi na kuwanyang'anya bunduki ndio wakamchapa ganzi. 😂😂
Haya ni maelezo ya polisi au mashahidi? Polisi sio wakweli huenda walitaka kumwibia makaa ya mawe wakizani mkaa wa miti.
 
Kama habari imeletwa na maandishi ni muongo,Kama polisi hua hawasemagi ukweli naishia hapo.
Wana staili,wanamkata mshukiwa wa uhalifu halafu wanamuamuru kimbia then wanampiga ya kidogo,Kisha wanatoa taarifa alikua akipambana na polisi.
Hawa jamaa hawa.washa niishie hapo.
 
Kama hakufanya?
Uchunguzi utafanyika na yatajulikana. Lakini kama kweli alitaka kuchukua silaha kwa nguvu kwa polisi anastahili alichopata.

Kama alisimamishwa akakaidi anastahili pia.

Tanzania tunakua na tabia ya ajabu ya kuona sisi tuna haki kuliko wengine. Polisi wangegongwa wafe mngeshabikia. Lakini hamtaki kuona kwamba raia pia wana makosa.

Sikatai kuwa polisi wanazingua lakini ni ukweli kwamba na sisi raia tuna makubwa ya ajabu tunayowafanyia.

Hamza alichukua silaha kwa nguvu kwa polisi yakatokea yaliyotokea.

RIP DAVOOO. ILA KAMA ULIZINGUA JUA UMEACHA MAJONZI KWA WANAO
 
Mmmh....ili kuiamini hii "single story" ya polisi....inahitaji mtu uwe na moyo wa upendo sana kwa jeshi la polisi.

Hivi ile issue ya "gaidi" Hamza iliishaje? Ama ndio lile onyo la "aijipii" la kutuonya watanzania tusizae magaidi?
 
Back
Top Bottom