Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

Dereva wa Dangote auawa na Polisi Lindi

Dereva wa gari la Dangote Ibrahim Said ameuawa na polisi baada ya kutaka kumnyang'anya askari bunduki.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinki anasema dereva huyo alifika eneo la kizuizi cha polisi akiwa kwenye mwendo mkali na hakusimama na alilenga walipokuwa wamekaa askari na askari hao walilikwepa kisha gari likaingia msituni.

Dereva alishuka katika gari na kuwafuata askari huku askari wakidhani dereva yule ana nia ya kuomba radhi kwa alichokifanya lakini haikuwa hivyo na dereva huyo alitoa kitu mwilini kinachosadikiwa kuwa ni kisu na kuanza kumshambulia askari na kumjeruhi huku akitaka kumnyang'anya silaha lakini askari alifanikiwa kumdhibiti kwa kumpiga risasi.

Askari watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.
Bora niamini Mimi sio binadamu kuliko kuwaamini polisi. Waseme sasi amepigwa sehemu gani tuanzr kichunguza. Hii mada inanikumbusha muvi ya kiusilamu, pale Yusuph alipobambikiwa kesi ya kumbaka mke wa mfalme na wakati mke die aliyetaka kumbaka Nabii wa Mungu
 
Nawajua polisiccm unadhani kwanini HAMZA Watanzania wengi walimuona ni shujaa? Unadhani kwanini polisiccm wanachukiwa sana na Watanzania wengi?
Utafiti wako ulifanyia wapi wa kuwa watanzania wengi walimuona Hamza shujaa?? Weka data hadharani mkuu
 
Uchunguzi usipofanyika na yasipojulikana au ukifanyika na bado yasijulikane je?
Uchunguzi utafanyika na yatajulikana. Lakini kama kweli alitaka kuchukua silaha kwa nguvu kwa polisi anastahili alichopata.

Kama alisimamishwa akakaidi anastahili pia.

Tanzania tunakua na tabia ya ajabu ya kuona sisi tuna haki kuliko wengine. Polisi wangegongwa wafe mngeshabikia. Lakini hamtaki kuona kwamba raia pia wana makosa.

Sikatai kuwa polisi wanazingua lakini ni ukweli kwamba na sisi raia tuna makubwa ya ajabu tunayowafanyia.

Hamza alichukua silaha kwa nguvu kwa polisi yakatokea yaliyotokea.

RIP DAVOOO. ILA KAMA ULIZINGUA JUA UMEACHA MAJONZI KWA WANAO
 
KAMA sio kweli?

Asee nimeiona hii habari hapa ITV. Kwamba dereva alitaka kuwagonga polisi kwa gari na baada ya wao polisi kukimbia gari ikagonga kichaka kisha dereva akashuka na kitu kama kisu kutaka kuwashambulia polisi na kuwanyang'anya bunduki ndio wakamchapa ganzi. [emoji23][emoji23]
Kuamini hili jambo linataka uwe na akili sijui za wapi, labda uazime fisiemu. Japo inawezekana kuwa kweli lakini mhuuu
 
We jamaa bana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwani we ulikuwepo eneo la tukio?
Yaani jamaa alishuka na kisu kwenda kuwanyanganya salaha police [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Basi sawa
 
Asee nimeiona hii habari hapa ITV. Kwamba dereva alitaka kuwagonga polisi kwa gari na baada ya wao polisi kukimbia gari ikagonga kichaka kisha dereva akashuka na kitu kama kisu kutaka kuwashambulia polisi na kuwanyang'anya bunduki ndio wakamchapa ganzi. [emoji23][emoji23]

Wakamchapa ganzi[emoji1787][emoji1787]
 
Polisi wanapenda sana kitu kidogo, nachokiona polisi wamemfanyia faulo huyo dereva!! Unatakiwa uchunguzi huru ufanyike!! Dhuluma no nyingi sana
 
Kutaka kumnyang’anya polisiccm silaha ni uongo wa hao jamaa ambao ni waongo WALIOKUBUHU.
Hata Hamza angepigwa risasi kabla hajafanya aliyoyafanya mngesema polisi ni waongo waliokubuhu.

Sometimes jipe muda wa kulitafakari jambo kabla hujaropoka, ukishakuwa na vielelezo unaweza kuja kutoa maoni yako
 
Back
Top Bottom