TANZIA Dereva wa John Heche akutwa amefariki chumbani Kigoma

TANZIA Dereva wa John Heche akutwa amefariki chumbani Kigoma

DEREVA WA JOHN HECHE AKUTWA AMEKUFA DAMU ZIMETAPAKAA KWENYE SAKAFU.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kuwatangazia kifo Suez Dani Maradufu ambaye ni dereva wa Makamu wa Mwenyekiti Bara, Mheshimiwa John Heche

Suez amekutwa amefariki leo asubuhi Jumatano, Julai 01, 2026 chumbani kwenye nyumba ya wageni aliyofikia, mjini Kigoma.

Mwili umechukuliwa na Polisi kuupeleka hospitali ya mkoa wa Kigoma kwa ajili ya taratibu nyingine za uchunguzi.

Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, ndugu jamaa na marafiki kwenye msiba huu mzito.

Taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa.

Bwana alitoa. Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina
Kutapakaa kwa damu ni red flag!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinasikitika kuwatangazia kifo cha, Suez Dani Maradufu ambaye ni dereva wa Makamu wa Mwenyekiti Bara, John Heche.

Suez amekutwa amefariki leo asubuhi Jumatano, Julai 01, 2026 chumbani kwenye nyumba ya wageni aliyofikia, mjini Kigoma. Mwili umechukuliwa na Polisi kuupeleka hospitali ya mkoa wa Kigoma kwa ajili ya taratibu nyingine za uchunguzi.

Chama kinatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, ndugu jamaa na marafiki kwenye msiba huu mzito.

R.I.P Suez Dani Maradufu,

Allah akupumzishe mahali unapostahili, Aimen 🙏
 
Sidhani. The strike of a close aide is intended to induce fear in him.

Kwa jinsi ambavyo macho ya dunia yako kwao, kumuua kiongozi mwandamizi wa CHADEMA ni decision ngumu sana kwao kuifanya!
Siwezi kukukanusha. All is possible! Ila kumuua dereva definitely watahusishwa na kama ni kulipiza kisasi una uwezo utalipiza.....
 
Tusifike mbali, ishu ni kukubaliana tu ni mabadiliko gani yafanyike, haina haja ya kuuana, siasa haziendi hivyo. Kina starmer mambo yaliwashinda wakaona isiwe taabu, wakaachia madaraka ili wenye fikra mpya nao wazitumie kujenga nchi yao. Mtu akiona maji yamemfika shingoni ajiuzulu tu kuliko kufanya siasa za chuki, mara kuzuia siasa zisifanyike kunakopelekea uhasama na chuki, hizi ni siasa za aibu kubwa. Watu waachwe waseme tani yao ndio uhuru na demokrasia komavu hiyo. Watu wakibanwa hujenga chuki na uhasama wa kuuana
Heche kaamua kumuua dereva wke kuficha ushahidi wa madhambi yake
 
Back
Top Bottom