Ushabiki wa kisiasa una mambo ya ajabu sana. Yaani kama vile washabiki wa Yanga wanavyomchukia Kagere moyoni mwao kisa tu ni mchezaji wa Simba hata afanyeje hawezi kupendwa na wana yanga labda atakaposajiliwa yanga. Au ni sawa na washabiki wa Simba wanavyomchukia Morrison moyoni mwao.
Devota Minja ameonesha kitu kizuri kinachopaswa kuigwa na wengineo, maana amesaidia watu wajikinge na janga hili la corona. Lakini ukiangalia kwa namna nyingine ni kwamba kuelekea kipindi hiki wanasiasa na vyama vya kisiasa kwao majanga yanayo kick ni fursa kubwa sana.
Hivyo pamoja na watu kutoa misaada hujui dhamira yake ni ipi ni kusaidia kweli au ni namna kujipa kampeni kuelekea kwenye uchaguzi.
Kumfananisha Devota na Abood hili linaweza kuamliwa na wana Morogoro wenyewe kwasababu wanajua kuwa; ukiachanana kupewa usafiri wa kwenda kuzika misibani ni vitu gani au mambo gani Abood amefanya kuleta maendeleo na pia wanajua kuwa ukiachana na huu msaada waliopewa wa Barakoa ni vitu gani vingine Devota Kavifanya katika kuleta maendeo Morogoro au mkuu kama una mizania yao hawa wawili tuorodhoshee hapa walivyovifanya ili tuweze kujua aliyemzidi mwenzie ni yupi. ila nachokumbuka mimi ni kwamba Abood kaanza kutoa magari ya kwenda kuzika misibani tokea zamani kabla hata ya kuwa mbunge.
Ifike wakati watanzania tuwe wadau wa maendeleo na tusiwe wadau wa vyama vya kisiasa.
Sent using
Jamii Forums mobile app