Dhana mbovu iliojengwa na mashabiki pamoja na viongozi wa Simba

Zama hizo zinaondoka saizi, watu wanawekeza kwenye mbinu na wachezaji hizo kelele zina asilimia chache kwenye ushindi.... Madrid na full house yao alikalia kwa Arsenal.... Vivyo hivyo Arsenal na full house yake alikalia na psg. Dhana ya hovyo ndio inawadanganya mpk wachezaji wanatumia vibaya viwanja vya ugenini.
 
Usisahau simba hiyo unayoiita ilikuwa bora ndo ilikuwa inapigwa tano mtawalia ikiwa away
 
Wanashida kubwa na bado kwa Mkapa au Amaan shughuli itakuwa nzito.. majamaa yanakaba na mpira wanajua labda wamkodishe Kefa Kayombo huenda akawapa goli
Wana matumaini na timu yao mkuu tutulie tuandae popcorn tukisubiri mbungi ya pili tusheherekee Ubingwa wetu sisi waaarabu weusi 😁
 
Na berkane atawafundisha nini maana ya timu kubwa kwa kushinda home and away
 
Zamani sio miaka ya hv karibuni hizo timu kupata matokeo mazurie,enzi za kufungwa goli 5 hizo ndizo unazoziongelea wewe
Mkuu em ngoja kidogo si tulikubaliana mnajenga timu lakini? Ko simba hii unaifananisha na ile ya Kina miquesson, chama, Wawa, Kagere, Mugalu na wengineo?
 
Ni wapuuzi tu wakubali Awana timu yenye ubora kupambana na berkane, uko walikotoka wamekutana na timu zote mbovu mbovu wakisaidiwa na marefa,,rejea kiwango cha Al masry walishinda kwao goli 2 lakini wakaja kwa mkapa wakatolewa kwa penalty sasa ebu tupime ubora wa Al masry na berkane je vinaendana? Kama umekohoa damu dhidi Al masry utawezaje kupindua meza dhidi ya berkane ambayo Iko vizuri Kila idara? Mambo mengine ni kuchangamsha genge tu siku ipite!
 
Simba SC Bingwa CAFCCL 2024/2025, Hutaki hamia Burundi au andamana, This is Simba SC nguvu moya...💪.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Umeongea point kubwa sana mkuu , tatizo watu wanaweka ushabiki mbele anyway ngoja sisi tungojee zetu tu
 
MAANDALIZI MUHIMU✍️
 
Washasahau kuwa walisema msimu huu bado wanajenga timu 😂
 
Mkuu em ngoja kidogo si tulikubaliana mnajenga timu lakini? Ko simba hii unaifananisha na ile ya Kina miquesson, chama, Wawa, Kagere, Mugalu na wengineo?
Haifanani lakini hata ile ilikua inaishia robo,so mpira sometimes ni mchezo wa bahati
 
Wakati huohuo unatakiwa ujiulize pia ni kwa nini caf wanalazimisha mechi ichezwe nje ya benjamini mkapa (pamoja na uwanja kukidhi vigezo vyote vya mechi kuchezewa) na pia kwa nini uamuzi huo ulionesha kufurahishwa na mpinzani wa simba .
✌
 
Waache waendelee kuamini hivyo utafikiri hawajawahi kufungwa hapo kwa mkapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…