Dhana ya Kumuinua Mtoto wa Kike ni bomu kwa Vizazi vijavyo

Unadhani hali hiyo unayoisema ilifikiwa kwa usanifu au kwa ajali?
 
Unadhani hali hiyo unayoisema ilifikiwa kwa usanifu au kwa ajali?
Nadhani hawakuangalia long term impact ya hili jambo, pengine walifanya kwa nia nzuri wakijua kwamba kumuinua mtoto wa kike kwenye jamii inatosha bila kuangalia madhara yatakayowapata watoto wa kiume na vizazi vijavyo kwa ujumla
 
Ulaya kwa sasa wameshaharibu taaasisi ya ndoa kwa sababu ya kumuinua mwanamke. Kule ukimzalisha mwanamke basi jua utamlea kwa Kila kitu mpaka mtoto atakapokuwaa mtu mzima. Pia mkiachana mnagawana nusu kwa nusu. So imewafanya wanawake wengi wakiolewa na mtu mwenye pesa wanadai talaka makusudi ili Kupata mgao. So badala ya kumsaidia mwanamke Sheria imefanya watu wengi ulaya hawaoi Tena badala yake wanatumia Malaya na njia zingine. Taaasisi ya ndoa ishakufa.
 
Nadhani hawakuangalia long term impact ya hili jambo, pengine walifanya kwa nia nzuri wakijua kwamba kumuinua mtoto wa kike kwenye jamii inatosha bila kuangalia madhara yatakayowapata watoto wa kiume na vizazi vijavyo kwa ujumla

Zifuatazo ni baadhi ya rejea, zinazoelezea matokeo uliyoyataja.

1. Raising Cain -- Hii video ni ya kuangaliwa na kila mzazi mwenye mtoto wa kiume. Na Kila mwalimu anayefundisha mtoto wa kiume.

2. The War Against Boys: How Misguided Policies are Harming Our Young Men -- Hoja kama uzi huu ilipata kuandikwa kitabuni. Komenti kwenye linki hiyo zinaelezea maoni ya wasomaji.

3. Men on Strike: Why Men Are Boycotting Marriage, Fatherhood, and the American Dream - and Why It Matters -- Kitabu hiki kinaelezea hatima ya yanayojiri. Komenti kwenye linki hiyo zinaelezea maoni ya wasomaji.


Mercy Mchechu - Mkurugenzi Rightway Schools

Hongera kwa kuandaa watoto kwenye hatua za awali katika safari yao ya kujielimisha.
 
Hao wanaume ni wavivu tu wasisingixie women empowerment hata zamani wanaume walikuwaga wavivu ni vile walidaganywa ni vichwa vya familia na kukuzwa kuliko uhalisia ukienda huko vijijini wanawake wanafanya kazi kuliko wanaume, na Tena zamani mama unalima na watoto baba anauza.
Wanaume waache uvivu na kusingizia haki sawa loh
 
Nchi za kimagharibi zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweka huo usawa.
Matokeo ambayo ni changamoto na hayadiscussiwi kama ni tatizo ni ongezeko la matransgender na kushuka kwa birthrate.

Wanaume wanatamani kuwa wanawake ili wafaidi upendeleo anaopata mwanamke.
 
Hii imeshaanza kujidhihirisha mapema sana. Wanaume wanalalamikiwa sana kukimbia majukumu yao lakini nadhani tatizo linaanzia hapo . Wanawake wanakwezwa mno na kuona kwamba wanaweza kila kitu hata bila msaada wa mumewe, hivyo kujijengea ego na kujiamin kupitiliza.
 
Mwandishi wa mawazo Haya alikuwa mototo wa kike naye, ambaye aliwezeshwa mpaka amekuwa mkurugenzi was rightway pale makonde. Ukiona imefikia hatua mpaka wanufaika wanadoubt. Ujue tatizo nikubwa. Ngoja tulitaftie dawa
 
Hili sasa limekuwa tatizo hata wanaowekeza kwenye sekta ya elimu wanapendelea kuwekeza zaidi kwenye shule za mtoto wa kike.Nyakati hizi ukitafuta shule bora ya wavulana ni shida.Tunahamisha tatizo kwenda upande wa pili badala ya kulitatua.
 

Madam Abrianna,

Uko sahihi kabisa. Kampeni ya kumwinua mtoto wa kike/ mwanamke na kumshusha mwanaume ni mpango mkubwa na madhara yake ni kuharibu kizazi cha mwanadamu.

Ni mpango unaotekelezwa na wakuu wa giza watumishi wa shetani wanaoitawala dunia.

Isaya alitabiri haya yapata miaka 700 kabla ya ujio wa Kristo.

Isaya 3: 12 Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.

Kwa hio sio jambo la bahati mbaya au linalotokea by chance. Wenye jukumu la kutatua tatizo ni wakuu wa dini lakini nao wako busy na sadaka, siasa na umaarufu.

Biblia pia iko wazi kuhusu matokeo matokeo yake. Ndoa zitavurugika, wanawake hawataolewa na wanaume ndio hivyo watakuwa mashoga nk.

Isaya 4:1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
 
Hakuna mwanaume anaweza kukaa na mwanamke kama yule!
 
Mtoto wa kike anatakiwa apiganiwe sawa ila kama imekuwa "too much" hivi.
 
Asante sana mkuu, nitatajitahidi kupitia hayo machapisho pamoja na movie ili nipate uelewa zaidi wa hili jambo
 
Hili sasa limekuwa tatizo hata wanaowekeza kwenye sekta ya elimu wanapendelea kuwekeza zaidi kwenye shule za mtoto wa kike.Nyakati hizi ukitafuta shule bora ya wavulana ni shida.Tunahamisha tatizo kwenda upande wa pili badala ya kulitatua.
Kwa nyakati zijazo zitakua nyakati ngumu sana kwa watoto wa kiume, pengine hawatapata elimu bora, hawatauzika kwenye soko la ajira na pengine watakua hawana confidence mbele ya wanawake since they have been neglected
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…