Dhana ya Kumuinua Mtoto wa Kike ni bomu kwa Vizazi vijavyo

Dhana ya Kumuinua Mtoto wa Kike ni bomu kwa Vizazi vijavyo

Ni kweli lakini mpaka sasa jamii imeathirika kwa kiasi kikubwa, na watoto wa kiume wameathiriwa na hizi kampeni, na imeathiri pia watoto wa kike kwa sababu asilimia kubwa ya wanandoa wa sasa mzigo mkubwa wa kulea na kuhudumia familia umebaki kwa mwanamke, wengine wamebaki single mothers, vijana wetu wengi wanatumia madawa ya kulevya na hawana mwelekeo
Unadhani hali hiyo unayoisema ilifikiwa kwa usanifu au kwa ajali?
 
Unadhani hali hiyo unayoisema ilifikiwa kwa usanifu au kwa ajali?
Nadhani hawakuangalia long term impact ya hili jambo, pengine walifanya kwa nia nzuri wakijua kwamba kumuinua mtoto wa kike kwenye jamii inatosha bila kuangalia madhara yatakayowapata watoto wa kiume na vizazi vijavyo kwa ujumla
 
Ulaya kwa sasa wameshaharibu taaasisi ya ndoa kwa sababu ya kumuinua mwanamke. Kule ukimzalisha mwanamke basi jua utamlea kwa Kila kitu mpaka mtoto atakapokuwaa mtu mzima. Pia mkiachana mnagawana nusu kwa nusu. So imewafanya wanawake wengi wakiolewa na mtu mwenye pesa wanadai talaka makusudi ili Kupata mgao. So badala ya kumsaidia mwanamke Sheria imefanya watu wengi ulaya hawaoi Tena badala yake wanatumia Malaya na njia zingine. Taaasisi ya ndoa ishakufa.
 
Nadhani hawakuangalia long term impact ya hili jambo, pengine walifanya kwa nia nzuri wakijua kwamba kumuinua mtoto wa kike kwenye jamii inatosha bila kuangalia madhara yatakayowapata watoto wa kiume na vizazi vijavyo kwa ujumla

Zifuatazo ni baadhi ya rejea, zinazoelezea matokeo uliyoyataja.

1. Raising Cain -- Hii video ni ya kuangaliwa na kila mzazi mwenye mtoto wa kiume. Na Kila mwalimu anayefundisha mtoto wa kiume.

2. The War Against Boys: How Misguided Policies are Harming Our Young Men -- Hoja kama uzi huu ilipata kuandikwa kitabuni. Komenti kwenye linki hiyo zinaelezea maoni ya wasomaji.

3. Men on Strike: Why Men Are Boycotting Marriage, Fatherhood, and the American Dream - and Why It Matters -- Kitabu hiki kinaelezea hatima ya yanayojiri. Komenti kwenye linki hiyo zinaelezea maoni ya wasomaji.

Mercy Mchechu - Mkurugenzi Rightway Schools

Hongera kwa kuandaa watoto kwenye hatua za awali katika safari yao ya kujielimisha.
 
Na pia kwa miaka hii ya karibuni limeibuka wimbi la watoto wa kiume ambao ni tegemezi au wanapenda kulelewa, hii ni moja ya impact ya hii kampeni ya kumwinua mtoto wa kike ambayo ilianza miaka mingi nyuma

Tusipoangalia hili jambo kwa jicho la tatu tutapoteza kizazi cha watoto wa kiume
Hao wanaume ni wavivu tu wasisingixie women empowerment hata zamani wanaume walikuwaga wavivu ni vile walidaganywa ni vichwa vya familia na kukuzwa kuliko uhalisia ukienda huko vijijini wanawake wanafanya kazi kuliko wanaume, na Tena zamani mama unalima na watoto baba anauza.
Wanaume waache uvivu na kusingizia haki sawa loh
 
Nchi za kimagharibi zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweka huo usawa.
Matokeo ambayo ni changamoto na hayadiscussiwi kama ni tatizo ni ongezeko la matransgender na kushuka kwa birthrate.

Wanaume wanatamani kuwa wanawake ili wafaidi upendeleo anaopata mwanamke.
 
3. Watoto wetu wa kiume tusipowaandaa kujua namna ya kuishi na hawa watoto wa kike tunaowajenga kwa sasa tutashuhudia ndoa nyingi kuvunjika, watoto wengi kulelewa na single parent, wanaume kutokujua majukumu yao kwenye familia. Mwisho wa siku hawa watoto wa kike tunaowajengwa kwa nguvu zote watakosa support kutoka kwa watoto wetu wa kiume.
Hii imeshaanza kujidhihirisha mapema sana. Wanaume wanalalamikiwa sana kukimbia majukumu yao lakini nadhani tatizo linaanzia hapo . Wanawake wanakwezwa mno na kuona kwamba wanaweza kila kitu hata bila msaada wa mumewe, hivyo kujijengea ego na kujiamin kupitiliza.
 
Note: Andiko hili lilitolewa May 16, Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kiume Duniani.

Kuanzia mwaka 2018, Dr Jerome wa Trinidad and Tobago alifanikiwa kuitambulisha tarehe 16 May ya kila mwaka kama siku maalum ya kutambua mchango wa mtoto wa kiume katika jamii. Tangu mwaka 2012 UN ilipotambulisha tarehe 10 October ya kila mwaka kama siku ya mtoto wa kike Duniani, swali liliibuka kwa nini tunatenga watoto? Kwanini tuna siku ya mtoto wa kike
Mwandishi wa mawazo Haya alikuwa mototo wa kike naye, ambaye aliwezeshwa mpaka amekuwa mkurugenzi was rightway pale makonde. Ukiona imefikia hatua mpaka wanufaika wanadoubt. Ujue tatizo nikubwa. Ngoja tulitaftie dawa
 
Hili sasa limekuwa tatizo hata wanaowekeza kwenye sekta ya elimu wanapendelea kuwekeza zaidi kwenye shule za mtoto wa kike.Nyakati hizi ukitafuta shule bora ya wavulana ni shida.Tunahamisha tatizo kwenda upande wa pili badala ya kulitatua.
 
Note: Andiko hili lilitolewa May 16, Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kiume Duniani.

Kuanzia mwaka 2018, Dr Jerome wa Trinidad and Tobago alifanikiwa kuitambulisha tarehe 16 May ya kila mwaka kama siku maalum ya kutambua mchango wa mtoto wa kiume katika jamii. Tangu mwaka 2012 UN ilipotambulisha tarehe 10 October ya kila mwaka kama siku ya mtoto wa kike Duniani, swali liliibuka kwa nini tunatenga watoto? Kwanini tuna siku ya mtoto wa kike na hatuna siku ya mtoto wa kiume?

Madam Abrianna,

Uko sahihi kabisa. Kampeni ya kumwinua mtoto wa kike/ mwanamke na kumshusha mwanaume ni mpango mkubwa na madhara yake ni kuharibu kizazi cha mwanadamu.

Ni mpango unaotekelezwa na wakuu wa giza watumishi wa shetani wanaoitawala dunia.

Isaya alitabiri haya yapata miaka 700 kabla ya ujio wa Kristo.

Isaya 3: 12 Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.

Kwa hio sio jambo la bahati mbaya au linalotokea by chance. Wenye jukumu la kutatua tatizo ni wakuu wa dini lakini nao wako busy na sadaka, siasa na umaarufu.

Biblia pia iko wazi kuhusu matokeo matokeo yake. Ndoa zitavurugika, wanawake hawataolewa na wanaume ndio hivyo watakuwa mashoga nk.

Isaya 4:1 Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
 
Jumuiya na asasi za kijamii pamoja na mm mwenyewe tusipokuwa makini tutaanza kampeni ya kumuinua mtoto wa kiume

Kwa miaka hii ya karibun kumeibuka haki sawa za kijinsia na hapo ndpo mtoto wa kike anapopewa kpaumbele Sana kuliko wa kiume

Usasa na wanawake wanaojiita wanaharakat wametufanya tuucheze huu wimbo wao nakumsahau mtoto wa kiume

Ongezeko la mashoga n kubwa Sana mitaani na wanaharakat wanasema n haki yao

Nje ya mada hivi Bibi @hellenkijobisimba kaolewa?
Hakuna mwanaume anaweza kukaa na mwanamke kama yule!
 
Mtoto wa kike anatakiwa apiganiwe sawa ila kama imekuwa "too much" hivi.
 
Zifuatazo ni baadhi ya rejea, zinazoelezea matokeo uliyoyataja.

1. Raising Cain -- Hii video ni ya kuangaliwa na kila mzazi mwenye mtoto wa kiume. Na Kila mwalimu anayefundisha mtoto wa kiume.

2. The War Against Boys: How Misguided Policies are Harming Our Young Men -- Hoja kama uzi huu ilipata kuandikwa kitabuni. Komenti kwenye linki hiyo zinaelezea maoni ya wasomaji.

3. Men on Strike: Why Men Are Boycotting Marriage, Fatherhood, and the American Dream - and Why It Matters -- Kitabu hiki kinaelezea hatima ya yanayojiri. Komenti kwenye linki hiyo zinaelezea maoni ya wasomaji.

Hongera kwa kuandaa watoto kwenye hatua za awali katika safari yao ya kujielimisha.
Asante sana mkuu, nitatajitahidi kupitia hayo machapisho pamoja na movie ili nipate uelewa zaidi wa hili jambo
 
Hili sasa limekuwa tatizo hata wanaowekeza kwenye sekta ya elimu wanapendelea kuwekeza zaidi kwenye shule za mtoto wa kike.Nyakati hizi ukitafuta shule bora ya wavulana ni shida.Tunahamisha tatizo kwenda upande wa pili badala ya kulitatua.
Kwa nyakati zijazo zitakua nyakati ngumu sana kwa watoto wa kiume, pengine hawatapata elimu bora, hawatauzika kwenye soko la ajira na pengine watakua hawana confidence mbele ya wanawake since they have been neglected
 
Back
Top Bottom