Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

CCM mnapokesha kuijadili CHADEMA mnakisaidia chama chenu? Upumbavu wenu unawagharimu wenyewe..

chadema hatuangalii ukanda wa mtu, bali uwezo wa mtu kutuongoza
 
Yani mwana diwani,simiyu ninapuuza post zenu kama ninavyo wapuuza nyie wenyewe!.wajinga wapuuzi msiokua na akili,mnawaza kuwagawa watanzania kwa udini na ukabila.
 
Huyu nae,

pilipili usioila yakuwashia nini? ya chadema waachie wenyewe na ya ccm mkajadili huko.

habari za udini mara ukabila au ukanda ni zenu wanaCCM n kipimo hicho mnchotumia mtapigwa mapigo sawsawa na hayo mapigo
 
CCM mnapokesha kuijadili CHADEMA mnakisaidia chama chenu? Upumbavu wenu unawagharimu wenyewe..

chadema hatuangalii ukanda wa mtu, bali uwezo wa mtu kutuongoza
Ndugu,
Hayo ya CCM na gharama ya upumbavu wetu wala isikusumbue!.

Kama CHADEMA hakiangalii udini na ukanda, mbona Prof. Safari anadai anapenda kuchaguliwa ili auondoe ndani ya chama.

Ataweza kuuondoa?
 
Nadhani ama akili yako ni ndogo ama umeamua kujifanya mpumba.vu. prof Safari amesema anataka kupambana na dhana ya udini iliyobambikizwa Cdm. Shirikusha ubongo wako
 
Chadema ni chama cha dini hii iko wazi hata washirika wao ni chama cha kidini cha ugerumani CDU!
 
bob nyanga makani ni mmoja wa waasisi wa chadema, ni msukuma, mwislamu kutoka kutoka shinyanga na katibu mkuu wa kwanza wa chadema. katibu mkuu ndiye mwenye siri zote chama, ndiyo anakaa na mafaili yote, ni mwajiri wa wafanya kazi wa makao makuu nk. nimejifunza mambo yafuatayo. mosi, kama waanzilishi wa chadema wangekuwa na agenda udini wasingemchagua bob makani kwa sababu yeye ni mwislamu. ( binafsi nimejua dini yake wakati wa msiba) pili kama waasisi wa chadema wangekuwa wanaagenda ya ukanda wasingemchagua bob makani kwa sababu hatoki kanda ya kaskazini. tatu, kama waasisi wangekuwa na agenda ya ukabila wasingemchagua bob makani kwa sababu si mchaga. kitendo cha kumchagua msukuma, muislamu, kutoka kanda ya shinyanga katibu mkuu na baadaye kuongezewa cheo na kuwa mkiti ina maanisha kuwa alifanya kazi vizuri na alikuwa anakubalika na wajumbe wote bila kujali dini, ukanda wala ukabila. wale waliokuwa wanacheza cd ya udini, ukanda na ukabila dhidi ya chadema sasa inabidi watafute cd nyingine ya kucheza dhidi chadema vinginevyo hii ya ukanda, . Ukabila na udini sasa zimechuja. Haiuziki tena. ni mawazo yangu tu.
mwanadiwani kamuulize mansour himid yusufu aliyefukuzwa ccm kwa vile ni mzanzibar anayetaka serikali 3 lakini akina lugola,kunjobe,kesy kwa vile sio wanzanzibar hawawezi kufukzwa pili kamuulize salim ahmed salim mlichomfanyia wakati anataka kugombea urais ni ubaguzi wa rangi/ udini au ukabila?
 
Ndugu,
Ndiyo maana ninajaribu kuuliza kutokana na yaliyojiri katika hoja za Prof. Safari.

Labda ni kujibu kwa kifupi tu,Prof.kazungumzia 'DHANA' ambayo inaweza kuwa ndani ya wanachadema au nje wanachadema.Kitu ambacho hajaweka wazi,tofauti na wewe unavyotaka kuaminisha wajinga!! Lugha aliyotumia Prof.katika neno "dhana" ni fasihi zaidi.Lakini kwa watu timamu wanaelewa kuwa maneno ya Udini,Ukanda na mengineyo uliyoyataja au aliyoyataja Prof.dhidi ya CDM yamekuwa yakitoka kwa walionje ya CDM hasa wale "Chama Cha Majungu"kuwasemea wanachadema kwa kujikita kwenye huruma ya kinafiki kwa wana CDM.Sasa mimi nilivyomuelewa Prof.ni kwamba,amegombea nafasi ile ilikuondoa ile 'Dhaniadhania'ya Chama Cha Majungu kuwa CDM ni chama cha Udini n.k si kweli baada ya uthibitisho wa yeye kuchaguliwa.Watu wote wanajua Prof.ni dini gani,na CDM inadhaniwa kwa makusudi ni ya dini gani!!
 
Mod's ninashindwa kuelewa kigezo mlichotumia kuiunganisha thread yangu yenye Heading, NI KWELI NDANI YA CHADEMA KUNA UDINI NA UKANDA.

Mimi siyo mpenda kulalamika, lakini kwa siku za hivi karibuni mmekuwa mkiunganisha thread zangu for no apparent reason..

Kama suala ni maudhui ya thread, ninaweza kuhesabu thread nyingi tu hasa ambazo zinahusu CCM mkiwa mmeziacha zinajitegemea wakati maudhui ni yale yale.

Where is the consistency?

Mfano, Suala kama la IPTL, Thread zote mmeziacha kuwa ingependent wakati maudhui ni yale yale au ni mwendelezo ya kinachoendelea kuhusiana na suala lenyewe.

Let's be fair as JF Motto, Where we Dare to Talk Openly

Kutumia silaha ya kuunganisha thread kama njia ya kuziondoa thread mbele ya jukwaa kwa vile hazijavunja taratibu na sheria za Jamiiforums siyo uungwana.
 
Mod's ninashindwa kuelewa kigezo mlichotumia kuiunganisha thread yangu yenye Heading, NI KWELI NDANI YA CHADEMA KUNA UDINI NA UKANDA.

Mimi siyo mpenda kulalamika, lakini kwa siku za hivi karibuni mmekuwa mkiunganisha thread zangu for no apparent reason..

Kama suala ni maudhui ya thread, ninaweza kuhesabu thread nyingi tu hasa ambazo zinahusu CCM mkiwa mmeziacha zinajitegemea wakati maudhui ni yale yale.

Where is the consistency?

Mfano, Suala kama la IPTL, Thread zote mmeziacha kuwa ingependent wakati maudhui ni yale yale au ni mwendelezo ya kinachoendelea kuhusiana na suala lenyewe.

Let's be fair as JF Motto, Where we Dare to Talk Openly

Kutumia silaha ya kuunganisha thread kama njia ya kuziondoa thread mbele ya jukwaa kwa vile hazijavunja taratibu na sheria za Jamiiforums siyo uungwana.

Umeshindwa kuelewa kwa nini tread yako imeungwa humu? Nikusaidie, imeungwa kwa sababu tread hii ndio majibu sahihi ya umbea uliotoa. Kwa hiyo badala ya kusoma umbea wako peke yake Mods wametuchanganyia na majibu ili tusisumbuke.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Sawa boss, lakini hata yanayoendelea ndani ya Chadema kila Mtanzania makini anayajua, shida hapa umemsigle out mtu mmoja kuelezea aliyoyataja kama mtaji wake. Hata CCM wanatumia mikakati kama hiyo kushinda. Tuliambiwa maisha bora kwa kila mtanzania, kwani wakati huo watanzania wote walikuwa masikii? Na sasa je watanzania wote wana maisha bora leo? Wanasiasa wote wanatumia slogans.Ungemuuliza angekuambia yeye atafanikishaje, mambo hayo ni ya vyama vyote sio CDM tu hata wewe wajua

hawa wajinga wasikuamishe kwenye point, pro, yuko sahihi na amejaribu kutoa tafsiri raisi tu kuwa kumbe cdm anawezq.kugombea yyte bila kujali dhana potofu kama ya akina ritz
cdm iko makini sana, na niseme tu ukweli uchaguzi huu ni wa kihistoria nq hauwezi linganishwa na uchaguzi wa taasisi yyte tanzania kwa sasa
kiukweli cdm kwa ss ndo tz na tz ni cdm,.
 
Ndugu,
Hayo ya CCM na gharama ya upumbavu wetu wala isikusumbue!.

Kama CHADEMA hakiangalii udini na ukanda, mbona Prof. Safari anadai anapenda kuchaguliwa ili auondoe ndani ya chama.

Ataweza kuuondoa?

Hakuseama kuondoa udini, alisema kuondoa DHANA ya udini iliyojengwa na ccm juu ya chadema. Utakuwa umeanza tabia ya shetani kunyofoa kugeuza maandiko matakatifu ilikuwalaghai watu kwa kupotosha maana.
Kweli waliozoea kuishi kwa uongo hawawezi kusema kweli.
 
Usitufanye WAPUMBAVU!!! Bob MAKANE KAOA ndugu wa MTEI,Endeleeni kujidanganya kuchukuwa DOLA kwa kutegemea kanda MOJA.
 
Ukitaka kujua kama Chadema Waislam hawatakiwi muulize Said Arfi na Zitto Kabwe leo hii wapo wapi.

Mbona haujawataja Juliana Shonza, Mwampamba, Mwigamba na Kitila Mkumbo? vipi hao pia ni waislam? tatizo lenu ni akili fupi ambazo zinawafanya mnaandika vitu pasipo kufikiria kwa mapana na ndipo mnapojikuta mnaacha maubongo yenu UCHI.
 
Wewe ni kada wa CCM lakini naona siku zote moyo wako upo CDM.[/QUOTE
siyo kada tu ni kiongozi wa ngazi ya juu lkn anahangaika na cdm hadi chama chao kinapoteza mwelekeo nguvu mnayo poteza hapa kushughurikia cdm huenda ingekisaidia chama chenu kama mngezielekeza kwenye kutatua kero za wananchi.
 
Kuna Propaganda nyingine za Kitoto kbs na sijui km wanaozitoa wana "akili timamu". Mtu anatoka mapovu kupotosha CHADEMA ni chama cha wachaga.. hivi kweli amereason?

Chama kina wabunge kila kona ya nchi lakini kinaitwa cha wachaga. Chama kina wabunge Musoma, Mwanza, Arusha, Mbeya, Singida, Dar, Kigoma, Iringa kinaitwa cha Wachaga. Chama kina madiwani Songea, Shinyanga, Singida, Moshi, Tanga, Morogoro, Pwani, Geita, Simbawanga, Mpanda eti still ni cha wachaga.

Uchaguzi mdogo wa udiwani uliopita CHADEMA ilishinda kiti cha Idiwani Njombe mjini kilichokuwa chini ya CCM. Eti bado kinaitwa cha wachagga. Hivi hadi wabena nao siku hizi ni wachaga? Akili ndogo bhana.!!

Mbona hamsemi UDP ni chama cha wasukuma kwa sababu kipo Bariadi tu?? M/kiti UDP- John Cheyo (Bariadi), Makamu Isaac Cheyo (Bariadi), Viongozi wa juu wote wa Bariadi..

Chama kina mbunge mmoja tu wa Bariadi, chama kina madiwani wilaya moja tu ya Bariadi, Structure iliyokamilika ya chama iko eneo moja tu Bariadi,

Chama kina kiongozi mmoja tu wa Halmashauri Bw.Benjamin Stephen wa Bariadi....Mtaji mkubwa wa chama kwenye uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo upo Bariadi...

Mbona pamoja na hayo yote hamsemi UDP ni chama cha Wasukuma, mnang'ang'ana tu kuwa Chadema ni cha wachaga?? Hivi ukiwa CCM lazima uwe na akili ndogo ya kushindwa kureson hata vitu vyepesi hivi?? Shameee.!!
 
CCM walianza na propaganda za ukabila zikashindikana. Wakaja na mbinu za ukanda zikachuja. Wakaibuka na singo ya udini haikulipa. Wakaparamia mazingaombwe ya ugaidi yakawarudi. Wakaibuka na kitisho cha kuingia msituni, kikagota. Sasa wamekuja na katiba ya kitapeli lakini ndio kwanza katiba yenyewe ikawa chachu kwa wapinzani kuungana! Bado tunawasubiri waje na propaganda nyingine tena.
 
Ccm wamekwama wameokota chuma kinacho zaniwa ni risasi ya kombora wameokota kwa hawa watu wanao okota vyuma chakavu mbali kabisa na kanisa lakini wakakimbilia kuwatisha wana nchi bomu laokotwa kanisani kijito nyama na wandishi wetu sijuwi kwanini hawachunguzi mambo na wakiambiwa wana beba hivyo hivyo
Zote ni mbinu chafu za serekali ya ccm kuwatisha wana nchi !
Watu wameokota chuma chakavu wanataka wakauze leo wanasema bomu limetegwa tena bila aibu
 
Back
Top Bottom