Dhuluma za Wakenya kwa bandari yetu

Dhuluma za Wakenya kwa bandari yetu

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
 
Wengine tumejua siku nyingi hujuma za kimafia za kenya. Sio kwamba mambo yanatokea tu. Ndio maana hatuamini kwenye ushindani wa soko peke yake.

Tunaamini soko linaweza kukamatwa kwa hila na ujanja. Kwa hivyo tunaamini kwenye udhibiti wa soko. Hapa lazima inteligensia yetu kufanya kazi kama ni genuine problem tuweze rekebisha. Kama kuna mtu anakunywa tujue.
 
Malori mengi ya Burundi na Rwanda pia Congo huwa nakutana nayo yakiwa tupu kuelekea Kenya hyo n miezi Kama mitatu iliopita nikawa najiuliza Sana kunani bandari ya DSM mbona hzi chuma nyingi Sana zinaelekea huko.

Hope ntaajihakikishia tena leo Mana Nina kasafari ka kupita njia yo tena.
 
Labda sijakuelewa..
Kwani Shipping Line inayofanya exportation kwa Port za Tanznaia ilikuwa ni MAERSK peke yake??
Mbona zipo Shipping Line nyingi tu..
Sijaelewa watu kwenda wenyewe Mombasa na kusema ni hujuma za Wakenya..kivipi??
Asante.
Nishangaa pia.., how now?
 
Wakenya siku zote wanasoma alama za nyakati. Wanatumia diplomasia kuliko nguvu. Wengi siyo walalamishi wanajua wanachokifanya kwa faida yao na hawahitaji kupiga kengele.

Ni watu wa kukanyaga ardhi ya Mungu polepole. Hivyo hatuhitaji kulalamika bali kuboresha utendaji wetu wa kazi.
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
kwani Maesrk inamilikiwa na nani? Kwanini unataka kumpangia mtu chakufanya?
 
Wakuu,

Wakenya wanaiua bandari yetu kimya kimya.

Hivi karibuni makampuni kadhaa hapa Tanzania yameanza kupeleka bidhaa zao Bandari ya Mombasa baada ya nafasi za shipping line maarufu ya Maersk kukosekana kabisa hapa nchini.

Msafirishaji akiangalia nafasi za kuexport mzigo kwa hapa nchini hapati ila akifanya hivyo kwa Mombasa anakuta nafasi za kutosha.

Ipo haja ya mamlaka za Serikali kuamka na kukemea hujuma hii kwani ikiachwa iendelee bandari ya Dar inakufa ikijiona.
Disclose the source of your argument and authentic statistics to support your claims. otherwise you better remain silent as no research no rights to speak.
 
Back
Top Bottom