Diamond awatukana vijana wa Tanzania; 'wana njaa'!

Diamond awatukana vijana wa Tanzania; 'wana njaa'!

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, msanii wa muziki na mmiliki wa biashara, ikiwemo WASAFIBET, ameamua kuwatukana vijana wa kitanzania kwa makusudi kwa kuchapisha tangazo lenye nia ovu ya kudhalilisha, kutweza na kubagaza utu wa vijana wa Tanzania. Ni dhahiri shahiri kuwa amewalenga vijana kwa kuwa wengi wao hawana ajira, hivyo wanategemea kubet ili wapate fedha za kujikimu.
View attachment 3206254
MAONI YANGU
Diamond amefanya kitendo kinachopaswa kulaaniwa na kila mtanzania mwenye utu, mpenda amani na anayezingatia na kujali maisha ya wengine, bila kujali hali zao za kiuchumi. Haikuwa na haja kuchapisha tangazo hili la kidhalilishaji, kibaguzi, kichochezi na kibagazaji. Kuna namna nyingi za kutangaza lakini sio kwa udhalilishaji wa kiasi hiki. Naomba serikali iingilie kati kwa kumuonya huyu kijana aache dharau kwa vijana wenzake na pia aondoe hilo tangazo, kuwaomba radhi vijana wenzake na kuapa kutorudia kosa kama hili wakati mwingine.

Nawasilisha.
Braza tafuta tu hela ilo Tangazo halina shida
 
Hapo Kuna memo vijana, acha uzembe na uvivu chapa kazi
 
Nadhani hapo ni kwamba kwa wengi kipindi kirefu sana January imekuwa ngumu yaani after festive periods hivyo wanakuwa wamechakaa AKA juu ya mawe hivyo wana Njaa so ukiunganisha ile njaa kwenye January bado ina sound kama January...

Since am sure you know this nadhani hapo tu umeleta hili kuendelea kutangaza tangazo lako (No such thing as bad Publicity)
 
Huu msemo/kauli wa njaanuary, nimeusikia muda sana Toka Kenya.

Hasa katika redio Maisha, kwa wale wapenzi wa kusikiliza redio.

Redio Maisha na Mkangai, baba Nora man of tactics, nyota wakumemetuka uwanjaanii.

Maisha magumu sana mtaani, ukishindwa mumunya sumu, Mimi stakuhukumu nitatoa tu rambi rambi.
 
Shida sio diamond na tangazo lake,shida ni sisi wenyewe, hatujui fasiri sahihi ya misamiati ya kiswahili. kabla hujamlaumu diamond nenda kamusi ya kiswahili sanifu ukapekue maana ya neno njaa kisha urudi hapa umpe diamond maua yake na samahani zisizo na idadi. ni hayo tu bhanandugu.
 
Hivi kwanini ukiwa huna pesa unakuwa mtu wa makasiriko muda wote.....?? Ehh yaani hapo hata ukikutana na mtu anaongea zake kidhungu utasikia linajifanya limesoma kidhungu kira wakati.......sijui lipoje hili
 
Back
Top Bottom