Nilitaka kupita kimya pasipo kuchangia ila mtifuano uliopo umenishawishi nami kutoa maoni yangu, japo napenda ieleweke kuwa maoni yangu sio sheria, ila natoa maoni kama mdau wa muziki ambaye nina maarifa pia ya muziki( napiga chombo na ninajua kanuni za muziki). Naanza kuchangia kwa kusema kuwa, tukijadili uharari wa ushindi wa tuzo kwa kuegemea kwenye ushabiki hatutaweka kuona na kupata ufumbuzi wowote. Nawapongeza wote waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo kwani kuna kitu kilionekana ndani ya kazi zo, ikumbukwe kwenye mashindano yupo atakaye washinda wengine. Mtu akishindwa hatakiwi kuleta visingizio ila kuangalia namna ya kujipanga zaidi wakati mwingine.
Kwa mtazamo wangu na kwa ujuzi kidogo nilionao wa muziki kama nilivyosema hapo mwanzo, naamini kijana kutoka Nigeria yaaani Burner Boy, ameshinda kihalali kabisa na sio kwa sababu za visingizio wavavyotumia mashabiki wa upande mwingine, japo sikatai kuwa management inaweza mpeleka msanii mbali, lakini hakuna ubunifu katika kazi ya msanii huyo, siku zote ataishia kulalama tu bila mashiko, management sio kigezo kilichomuangusha msanii wetu Diamond, kilichomwangusha ni ubunifu finyu, ndugu zangu hata ukijunze vipi kuogelea hauwezi kumshinda samaki kuogelea.
Wakati Wanigeria wanatengeneza muziki wao kwa kuingiza zaidi utamaduni wao, sisi tumekuwa tukiokoteza midundo na mitindo kutoka kwao, halafu tunategemea kushinda nao, angalia asilimia ya nyimbo za wasanii wetu, hapa simtaji Diamond tu, ila na wasanii wengine wengi wa kitanzania, mara nyingi ukisikiliza nyimbo zao hazina misingi ya muziki naweza kuziita ni kelele tu ambazo watu wameamua kuzikubali, na wasanii wengine wanaofanikiwa kusikika zaidi wengi hawana ubunifu ukocopy aina za muziki za watu wengine ambazo nazo hawazijui vizuri yaani ni kama kusema, ukocopy nyimbo ya salsa kutoka Latin America halafu uende ukashinda nao jibu nadhani unalo.
Najua wengine watasema mbona Wizkid naye kashindwa kwani naye anakocopy, jibu ni kuwa pamoja kwamba Wizkid na wasanii wengineo kuwa na management nzuri na kufuata misingi ya muziki wao, wameshindwa na Burner Boy kwa sababu moja tu msimu huu jamaa amewazidi ubunifu, ukitaka kujua hilo sikiliza album zao. Uhusiano wa Burner Boy na P.didy au kuwa management nzuri sio kitu pekeee kilichochagiza yeye kupata tuzo hio bali ni ubunifu narudia tena ni ubunifu wa hali ya juu, ubunifu huo umeonekana kuanzia kwenye uandishi, midundo ya nyimbo zake na namna anavyotumia sauti yake.
Ushauri wangu, wasanii wa hapa nyumbani yaani Tanzania wanatakiwa kuacha kucopy kwani kunarudisha nyuma ubunifu wao, pia wanapoandika nyimbo wanatakiwa wajua watu wanaowalenga, hizi nyimbo zao za matusi zinawafubaza akili zao, wanapoona zimepata muitikio hususani kutoka katika kundi la vijana wasiojua kitu kuhusu muziki bali wenye kiu ya kusikia maneno ya ngono na viungo vya uzazi vikitajwa, wajiona wamekuwa wakubwa sana, lakini ukitaka kujua kinachowafanya wasikilize nyimbo hizo ni upuuzi unaosapoti upuzi wao, ni muda ambazo hizo nyimbo zinabaki vichwani mwa watu, mara nyingi nyimbo hizo hazidumu kwanini jibu ni kuwa kilichopendwa ni maneno ya hovyo na sio muziki wenyewe. wasanii kutunga tungo zitakazodumu na kukonga watu nyonyo bila kujali lugha zao, kumbuka muziki ni lugha inayoeleweka na watu husasani pale unapotungwa na kupangwa kwa ueledi.