Diamond kaangushwa na mameneja wake sio Wanaharakati

Diamond kaangushwa na mameneja wake sio Wanaharakati

Masikini Dogo inno chozi limemtoka
1624964659668.png

Cartoon By Kigoma Independent

cc Numbisa
 
Bado tupo kwa uyu kijana tu..hauna mambo mengine ya kufanya
 
DIAMOND KAANGUSHWA NA VIONGOZI WAKE, NA SIO KIGOGO WALA WANAHARAKATI.

Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi chama kiendelee. Kabla baadhi yenu hamjaanza kunisumbua kutaka nitoe maoni yangu kuhusu kushindwa kwa komredi Simba kwenye tuzo za BET, nimeona niyatoe mapema. Kama kawaida maoni

Sasa meneja wake SALAMU kazuiliwa kwenda USA kwasababu ni muuza madawa ya kulevya,BANNED US.

Babu tale shule Fa Fa Fa Fa Fa Fa , Mama Dangote yupo busy na Kiben10.
 
Hivi Diamond Platnumz ana tuzo ngapi kulinganisha na huyo Burna Boy? Nadhani Diamond is way too far from Burna Boy when it comes to number of awards winning...pia alikuwa na mameneja hao hao unaowaponda
Kwa tuzo za Kitaifa na za Afrika Mashariki..ni kweli Dai is way too far compared to Burna Boy! lakini kwa zile za KIMATAIFA...Dai anasubiri sana kwa Burna Boy!
 
Duuuuuh hiyo ni CV ya mama wa mwanamuziki mkubwa toka Africa mashariki na kati halafu ndo aweze kutoboa kimataifa kweli acheni ushamba, meneja wake ni mganga mzuia mvua mwingine muuza drugs na maisha ya ujanja ujanja unategemea nini hapo tena bora wameshindwa maana angerudi na tuzo huyo kwa tunayemjua na ushamba wake angeamuru WASAFI TV na WASAFI FM wamtangaze yeye tu kwa siku 7 mfululizo. Pia inawezekana kweli dogo alizuiwa kuingia ndani na mavazi yake hayo ya kike maana nnavyowajua wapambe wake wangeshatuonyesha mapicha picha mengi alivyokuwa ndani kiufupi dogo kariabisha taifa kmmk.
Mameneja hao hao ndio waliokuwa naye kipindi media zimemtupa na kumtenga na hakutokea hata mwanaharaka mmoja kumtetea,mameneja hao ndio walio mfanya ashinde tuzo nne za channel 0,mbili MTV Europe, Moja MTV MAMA na mameneja hao hao ndio walio mfanya leo hii awe ashapiga show zaidi ya 90% ya nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

Mameneja hao hao ndio waliomfanya awe hapo.
 
Meneja wake wa kimataifa ni Salaam SK ambaye amepigwa life Ban ya kuingia Marekani.
Meneja wake mwingine ndiyo huyo Babu Tale ambaye anaongea kwa ufasaha lugha ya Kiluguru na Kiswahili.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Babu tale ni empty box aisee. Sasa na mond kwanini awe na meneja mhalifu aliyezuiliwa kuingia marekani hyo tu siinakuwa Ina mchafulia CV.
 
Nakubaliana na wewe! pia isitoshe Wakati alipokuwa na Zali Diamond ndo alipata nafasi ya kufanya kazi nyingi na nzuri na wasanii mbali mbali wa nje-ata Zali angeweza kuwa manager mzuri kwake lakini amezungukwa na vilaza ambao awatopenda aje mwenye akili kuliko wao kwa Diamondi lazima watamfanyia figisu figusu atoke!! kule BET sijui kama ata Ukumbini aliingia[emoji1787][emoji1787][emoji1787] picha zote yupo nje na ni za mchana....mle ndani kulikuwa na wasanii wengi aliofanya nao kazi how comes akuna ata kapicha kamoja akiwasalimia??? Dogo aliishia nje ...so sad kwakeli
Na kingine kilicho mpoteza focus diamond ni ma drama ya kipumbavu na wanawake zake na kuzaa hovyo, tangu aanze hapo it was like Ali drop. Diamond anahitaji meneja mwenye exposure na hivi ni fighter atafika
 
Nilitaka kupita kimya pasipo kuchangia ila mtifuano uliopo umenishawishi nami kutoa maoni yangu, japo napenda ieleweke kuwa maoni yangu sio sheria, ila natoa maoni kama mdau wa muziki ambaye nina maarifa pia ya muziki( napiga chombo na ninajua kanuni za muziki). Naanza kuchangia kwa kusema kuwa, tukijadili uharari wa ushindi wa tuzo kwa kuegemea kwenye ushabiki hatutaweka kuona na kupata ufumbuzi wowote. Nawapongeza wote waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo kwani kuna kitu kilionekana ndani ya kazi zo, ikumbukwe kwenye mashindano yupo atakaye washinda wengine. Mtu akishindwa hatakiwi kuleta visingizio ila kuangalia namna ya kujipanga zaidi wakati mwingine.
Umeandika vyema.

Album ya Burna Boy ya African Giant ni moja ya album huwa sichoki kuisikiliza. Humo ameimba siasa (Collateral Damage), Mapenzi (Low) na kutafuta maisha (Wimbo Kama Dangote) na zingine nyingi Sana nzuri

Pia kwenye album ya TWICE AS TALL vile vile pia.

Cha mwisho ambacho Umeongea na ni point kubwa Sana , wasanii wa TANZANIA kuiga miondoko ya wanaijeria kunawaharibia sana kimataifa.
 
Meneja wake wa kimataifa ni Salaam SK ambaye amepigwa life Ban ya kuingia Marekani.
Meneja wake mwingine ndiyo huyo Babu Tale ambaye anaongea kwa ufasaha lugha ya Kiluguru na Kiswahili.
Kwann alipigwa ban mkuu
Huyo sk?
 
Si mziki tu, hata Nollywood, actors na actresses wao wengine wane akiwa Ulaya na Marekani. Wengi wa Master’s za sanaa. Nillywood imeifunika kabisa Bollywood. Wazungu pia wanaangalia sinema za Nollywood.
 
Nakubaliana na wewe! pia isitoshe Wakati alipokuwa na Zali Diamond ndo alipata nafasi ya kufanya kazi nyingi na nzuri na wasanii mbali mbali wa nje-ata Zali angeweza kuwa manager mzuri kwake lakini amezungukwa na vilaza ambao awatopenda aje mwenye akili kuliko wao kwa Diamondi lazima watamfanyia figisu figusu atoke!! kule BET sijui kama ata Ukumbini aliingia🤣🤣🤣 picha zote yupo nje na ni za mchana....mle ndani kulikuwa na wasanii wengi aliofanya nao kazi how comes akuna ata kapicha kamoja akiwasalimia??? Dogo aliishia nje ...so sad kwakeli
Sasa na ww mbna hate inazidid sasa?
Hukuona bet walionyesha anapokaa ndani?
Ah watanzania hadi vitu vivid tunavifumbia macho?
Duuuuuh hiyo ni CV ya mama wa mwanamuziki mkubwa toka Africa mashariki na kati halafu ndo aweze kutoboa kimataifa kweli acheni ushamba, meneja wake ni mganga mzuia mvua mwingine muuza drugs na maisha ya ujanja ujanja unategemea nini hapo tena bora wameshindwa maana angerudi na tuzo huyo kwa tunayemjua na ushamba wake angeamuru WASAFI TV na WASAFI FM wamtangaze yeye tu kwa siku 7 mfululizo. Pia inawezekana kweli dogo alizuiwa kuingia ndani na mavazi yake hayo ya kike maana nnavyowajua wapambe wake wangeshatuonyesha mapicha picha mengi alivyokuwa ndani kiufupi dogo kariabisha taifa kmmk.
Sasa mkuu mbna kama unakua kama mcheza kiduku kwenye ghala la mkaa

Sielewi ni nini shda mnamsema mama wa msanii
Burna kama burna kabahatika kuzaliwa katika familia iliokuwa njema sio kwamba yeye alichagua mimi namtaka huyu mama hapana..
Wasifu wa mama wa msanii usihusike hapa na nakataa kwamba ndio sababu ya kukosa tuzo kwa diamond
Kwa tunaofatilia mpira kuna wakina cr7 wametoka familia baba mlevi mama anaishi maisha ya kuunga unga lakini wana matuzo kuliko watu kama wakina pirlo waliozaliwa familia njema..
Nmezunguka saaana ila main point ni kumkebehi mzazi wa diamond si sahihi
Hakuna mtu anachagua mzazi we have to adapt to what we were given bwana mkubwa......

Watanzania sisi
Tunajudge mzazi wa msanii huyu kwa msanii yule kwenye kulinganisha nani apate tuzo smh
 
Umeandika vyema.

Album ya Burna Boy ya African Giant ni moja ya album huwa sichoki kuisikiliza. Humo ameimba siasa (Collateral Damage), Mapenzi (Low) na kutafuta maisha (Wimbo Kama Dangote) na zingine nyingi Sana nzuri

Pia kwenye album ya TWICE AS TALL vile vile pia.

Cha mwisho ambacho Umeongea na ni point kubwa Sana , wasanii wa TANZANIA kuiga miondoko ya wanaijeria kunawaharibia sana kimatawa

Umeandika vyema.

Album ya Burna Boy ya African Giant ni moja ya album huwa sichoki kuisikiliza. Humo ameimba siasa (Collateral Damage), Mapenzi (Low) na kutafuta maisha (Wimbo Kama Dangote) na zingine nyingi Sana nzuri

Pia kwenye album ya TWICE AS TALL vile vile pia.

Cha mwisho ambacho Umeongea na ni point kubwa Sana , wasanii wa TANZANIA kuiga miondoko ya wanaijeria kunawaharibia sana kimataifa.
Wanaiga sana sasa ukifika wakati wakushindanishwa na wenye muziki wao, wanategemea huruma ya washabiki wao na kuanza kutoa maneno ya shutuma na lawama zisizo na msingi. Angalia hata muziki wa dansi ulivyokufa, hapo kabla bendi za zamani zilipiga mapigo ya kiasilia na kufanya vizuri angalia watu kama wakina Marjan Rajabu, Baraka Mwishehee na Bendi kama Les Wanyika, ila kizazi kilichofuata walipoleta ucongo dansi ikapoteza muelekeo kabisa.

Wasanii wetu wamekuwa kama kasuku, kuiga kila wanachosikia mwisho wa siku wanabaki hawana kitu wanachokijua kwa usahihi, kasuku angekuwa anatumia muda kujifunza lugha moja angeweza kuongea ila tatizo kila anachokisika anakitaka au ndio wasanii wetu mara hawa wanakopy Nigeria wengine kule amapiano South Africa yaani ni shida tupu muziki umerudi nyuma sana na ndio maana uzuri wa nyimbo zenyewe haudumu kabisa.
 
DIAMOND KAANGUSHWA NA VIONGOZI WAKE, NA SIO KIGOGO WALA WANAHARAKATI.

Nawasalimu katika jina la Chama Cha Mapinduzi chama kiendelee. Kabla baadhi yenu hamjaanza kunisumbua kutaka nitoe maoni yangu kuhusu kushindwa kwa komredi Simba kwenye tuzo za BET, nimeona niyatoe mapema. Kama kawaida maoni yangu ndo yatakuwa msimamo wa JF. Soma kwa makini.

Kwanini kashinda Burna Boy na sio kada wa CCM Komredi Diamond Platinumz? Ieleweke Meneja wa Burna Boy ni mama yake mzazi. Unaweza ukakurupuka na kudhani labda Mama Dangote naye awe meneja wa mtoto wake ili kurahisisha kazi. Tuzingatie kuwa Mama Burna sio mgeni kwenye kazi yake ya umeneja. Huyu mama ni binti wa Benson Idonije ambaye alikuwa meneja wa mwanamuziki mkubwa kuwahi kutokea Afrika, komredi Fela Kuti. Mama Burna ana Masters degree toka Chuo Kikuu cha Port Harcourt. Huyu mama huzungumza kwa ufasaha lugha ya kiingereza, kifaransa, kijerumani, kiitaliano na kiyoruba. Amefundisha kifaransa kwa miaka 10 kwenye Chuo Kikuu cha Port Harcourt na kustaafu 2018. Kimsingi Mama Burna ana CV ya kutisha pia kakulia kwenye familia ya meneja. Hiyo kazi ipo damuni.

Pamoja na Burna Boy kupata Meneja mwenye viwango vya kimataifa bado tunaambiwa nguli P Didy (Sean Puffy Combs) ni meneja wake kwa upande wa Amerika. CV ya Diddy kwenye muziki ndani ya USA inaeleweka yaani hakuna haja ya maelezo. Tukiachilia mbali mameneja wa Burna, tukumbuke hata Burna ni msomi wa Chuo Kikuu.

Komredi Simba huenda ana kipaji kikubwa kuliko washindani wake lakini tunaona menejimenti yake ni dhaifu kuweza sawa na ushindani wa mameneja wengine. Mimi naona inabidi tukubaliane kwamba kijana aajiri meneja atakayeweza kwenda sawa kimataifa. Mameneja waliopo ndo uwezo wao ulipofikia hatuna cha kuwalaumu zaidi ya kuwapongeza. Ila nao waukubali huu ukweli mchungu. Meneja mwenye elimu ya darasa la saba ni ngumu sana kumvusha msanii wetu. Meneja anatakiwa awe mbali kimaono kuliko msanii. Lakini WCB inaonekana msanii ana akili kuliko mameneja.

Nimalizie kwa kusema kwamba hawa kina Kigogo wa Twitter na wanaharakati uchwara kama Maria Sarungi & company hawakuwa na uwezo wowote wa kuzuia Simba kupata tuzo. BET haipo kisiasa. Na kama kungekuwa na jambo baya kwa vyovyote wangeuliza ubalozi wa USA nchini kama kweli madai ya kina Kigogo ni kweli. BET haina kipengele cha siasa kwenye shuguli zake. Kina Kigogo walichofanya ni kumuongezea umaarufu Diamond.
Kwali hili ndio nimeamini kweli upinzani ni utopolo...
 
Kweli huko aendapo anahitaji mameneja wenye upeo mkubwa zaidi ya hawa alionao! Kuna story hapo 👇🏼Kifupi mi kwamba:

1. Mondi hakufanya intavyu ya red kapet sababu waliona akifanya lile vazi litampa attention kubwa kwenye show yao wamarekani. Ni ajabu nominee hana intavyu ya red kapet! Angekuwa na meneja mwelewa angemshauri avae simple.

2. Hakupelekwa kukaa sehemu ya VIP kama nominee mwenzake Burna. Alikaa kajamba nani huku Burna akiwa VIP, pembeni ya DJ Khaled. Angekuwa na meneja mwenye upeo angeshughulikia hili kabla ya show.

Story.....

"Diamond was bounced from the red carpet"

kampalasun (dot) co (dot) ug

Jun 29, 2021 11:45 AM

By Ahmad Muto

Reports emerged on Monday, June 28 hours after the BET awards that singer Diamond Platnumz got bounced from the red carpet in Los Angeles, Carlifornia because of how he dressed. Social media in particular accused BET of being inconsiderate towards African artistes.
Then came former media personality turned socialite now based in the US, Kabs Haloha who was in attendance. He branded Diamond’s Masaai attire a ‘blunder’ and therefore the reason for his woes.
“His first blunder was dressing like he did so they ignored him. They assumed he was trying to crash the red carpet. He is a big star to dress like that. If it was a great style, he would be trending in the US but he is not. He is trending in East Africa because that is the understanding there. His entourage was way smarter than him. I love him and his music but the outfit was off,” said Kabs.
He also noted that as if to show Burnaboy was bigger than him, the Nigerian sat next to DJ Khaled in the VIP section while he sat in the regular section. Also, nobody bothered to interview him like the media normally does on the red carpet.
“I got in there, I had all access to the sections and there is a sitting arrangement. There is the VIP where you have the DJ Khaleds and then you have other sections. Diamond was in a different section, which I feel was unfair because Burnaboy was next to DJ Khaled,” he explained.
Kabs added: “I didn’t see his live interview on the red carpet. Being a nominee is a pass to have a live interview. But no TV station requested for his interview.”
Diamond lost the Best International Act award to Burnaboy.
 
Domo hajaangushwa na yoyote bali uwezo wake mdogo hana ubunifu zaidi ya kutegemea kurudia nyimbo za wenzie kwa kubembea kwenye msemo hakuna kipya duniani
Nyimbo zenyewe zimejaa matusi siku hizi
 
Hivi Diamond Platnumz ana tuzo ngapi kulinganisha na huyo Burna Boy? Nadhani Diamond is way too far from Burna Boy when it comes to number of awards winning...pia alikuwa na mameneja hao hao unaowaponda
Za kili
 
Nakubaliana na wewe! pia isitoshe Wakati alipokuwa na Zali Diamond ndo alipata nafasi ya kufanya kazi nyingi na nzuri na wasanii mbali mbali wa nje-ata Zali angeweza kuwa manager mzuri kwake lakini amezungukwa na vilaza ambao awatopenda aje mwenye akili kuliko wao kwa Diamondi lazima watamfanyia figisu figusu atoke!! kule BET sijui kama ata Ukumbini aliingia[emoji1787][emoji1787][emoji1787] picha zote yupo nje na ni za mchana....mle ndani kulikuwa na wasanii wengi aliofanya nao kazi how comes akuna ata kapicha kamoja akiwasalimia??? Dogo aliishia nje ...so sad kwakeli
Alienda kupiga photo akasepa zake
 
Back
Top Bottom