Tetesi: Diamond kujiunga CHADEMA mwaka 2024 na 2025 kugombea Ubunge kupitia chama hicho

Tetesi: Diamond kujiunga CHADEMA mwaka 2024 na 2025 kugombea Ubunge kupitia chama hicho

Habari zenu wana JF wenzangu.

Katika pitapita zangu maeneo fulan nimekutana na hii habari kutoka kwa mtu wa karibu mno wa msanii huyo, akidai kwamba Diamond yuko katika mchakato wa kulishangaza taifa hapo mwakani.

Japo mimi sio mwanasiasa, lakini ningependa kumshauri ndugu yetu Diamond afikirie mara mbili uamuzi wake huo. Asije kuingia huko kichwa kichwa akaanza kufanywa mtaji wa kisiasa na hawa wanasiasa wetu uchwara wanaofanya siasa zao kupitia mgongo wa majina ya watu maarufu nk.

Na kama kweli ana lengo la kushinda uchaguzi basi akagombee katika jimbo moja la kwao Kigoma, maana kule anakubalika kuliko yule mmanyema mwenzake kwa jina anaitwa Zito.

Wewe kama mwana JF, una nini la kumwambia ndugu yetu Dangote wa tandale.

Lisemwalo lipo, na kama halipo laja.
NA WEWE UNAJIUNGA LINI NA ACT KUGOMBEA URAIS ? MAANA NAONA UNAWATAJA WENGINE
 
Me nimezungumza kuandamwa wewe unasema kuandamana uoni utofauti
Ok mkuu nahisi nilikuwa sijakuelewa.
Ila CCM ya sasa sio ya kuandama wala kuandamwa, ndio maana siku hizi ni kawaida kuwakuta kina Mbowe, Zito na magenge yao wakijichanganya na wana CCM bila bughuza yoyote.
 
NA WEWE UNAJIUNGA LINI NA ACT KUGOMBEA URAIS ? MAANA NAONA UNAWATAJA WENGINE
Siku kikipata viongozi makini nitajiunga nacho. Lakini kwa sasa naona kimejaa wachumia tumbo watupu kutoka pande za mwambao.
 
Katiba ya Tanzania unaijua ulishawahi kuisoma? Diamond siyo Mtanzania? Kugombea hilo jimbo unalosema ni makosa kisherI?
Sio mtanzania ni Mmarekani au mjerumani?
Anaishije ishije na familia yake hapa Tz?
Na akisafiri huwa anatumia passport ya nchi gani?
 
Huko kutaitwa kupatwa kwa Bunge

Maana Sasa litageuka kokoro.
Inasemekana nje ya mziki jamaa yuko vizuri kichwani.
Sema ndo hivyo mambo ya sanaa sometimes lazima ujifanye kichwanga ili kuvuta views na Like za kutosha mitandaoni.
 
Uongozi kwa ujumla siyo mahali pa kwenda kutafutia pesa, bali ni mahali pa kwenda kutumia pesa yako, ujuzi wako na uwezo wako, kuwasaidia unaowaongoza. Ni mahali pa kwenda kuwaonesha unaowaongoza njia ya kuondokana na umaskini, ja matatizo mbalimbali yanayowazunguka unaowaongoza. Kiongozi anastahili kuwa na majibu ya matatizo ya anaowaongoza.

Fikiria maskini anakuwa kiongozi, halafu wewe maskini mwenzie unaamini yeye anaweza kukuonesha njia ya wewe kutoka kqenye umaskini. Yaani akuoneshe njia ambayo hata yeye hakuiona.

Tanzania, ndiyo maana unasikia pesa za umma zinaibiwa, ni kwa vile maskini wanatafuta uongozi ili waondokane na umaskini.

Uongozi ni jambo la heshima. Wanatakiwa kwenda wanaotafuta heshima na recognition, na sio wenye njaa kali.

Hivyo, kwa Diamond kuutafuta uongozi siyo ni jambo jema. Ana uwezo wa kuyatatua matatizo kadhaa ya atakaowawakilisha, japo siyo sifa pekee anayostahili kuwa nayo kiongozi.
Umeandika maneno yenye busara na elimu tosha kwa watakaopenda kujifunza kupitia kwa haya uliyoandika.

Ila kwa tabia za sisi watanzania, tuliokuelewa ni wachache sana.
 
Kwanza aoe mke sio kuzaa ovyo nje ya doa. Ubunge ni kazi ya heshima sema imegeuzwa kua kazi ya kihuni kwa wahuni kugombea.
Japo umeandika kisela, lkn maneno yako yana make sense 😍👍😂
 
Back
Top Bottom