Diamond platinumz atupiwa jini, lampata mama'ke!

Diamond platinumz atupiwa jini, lampata mama'ke!

Diamond usiwaige P-sqaure,Hakuna kama mama,kipi bora kati ya Fame na Mama?
 

Attachments

  • Jini pesa.jpg
    Jini pesa.jpg
    193.2 KB · Views: 541
  • Jini kitisho.png
    Jini kitisho.png
    79.8 KB · Views: 553
  • Jini moto.jpg
    Jini moto.jpg
    14.9 KB · Views: 555
Kuna watu wamechapa matokeo ya utafiti unaoonesha Tanzania asilimia 90 ya watu wanaamini hizi habari za uchawi na madini. Naweza kuona hilo kufanana na ukweli.

Mbongo anaweza ishi miaka 50 bila check up hata ya meno, siku akipooza kitu cha kwanza kusema ni jini au uchawi.
 
Pole bana. Mapito tu hayo, ni mtihani anaopewa binadamu yeyote lakini majibu anayo Mungu. Uwe mvumilivu Diamonmd, achana na mavuvuzela.
 
Wabongo kwa umbea wako vizuri kama alirushiwa jini angetakiwa kupelekwa kwa mchungali kuombewa au huko indiani ndo wana uzoefu wa kutoa mapepo.
 
Kuna watu wamechapa matokeo ya utafiti unaoonesha Tanzania asilimia 90 ya watu wanaamini hizi habari za uchawi na madini. Naweza kuona hilo kufanana na ukweli.

Mbongo anaweza ishi miaka 50 bila check up hata ya meno, siku akipooza kitu cha kwanza kusema ni jini au uchawi.

Au unakuta mtu kwa miaka mingi tu anaonyesha dalili za kuwa na ugonjwa wa akili na siku huo ugonjwa ukiwa full-blown na hatimaye anaanza kuokota makopo, anatafutwa mchawi aliyemrushia majini!

Na hapo huyu mtu usikute hata siku moja hakuwahi kujaribu kwenda kufanyiwa tathmini ya afya ya akili yake (licha ya kwamba hata wataalamu wa afya za akili kuwa wachache sana)
 
Hivi hawa Global ni Mungu gani wanamuongelea hapa? eti hakipenda Jini limpate Diamond ..kwa hiyo likampata mamaye!

Ujinga mtupu...
 
daddy nawe unaamini uchawi ?

Tatizo la uchawi uuamini au usiuamini wenyewe upo tu, ila siku ukikumbana nao ndio utajua kama unachagua wewe unauamini au lah.

Mfano kwenye muziki wa bongofleva hizi mambo zipo sana.

Nitakupa kisa kimoja cha kweli, juzi hapa kulikuwa na onyesho la tigo pale leaders club sasa katika maandalizi msanii mmoja hasimu wa Diamond alifanya tukio nashindwa niliiteje.....Alipelekwa mtaalam wa jadi, alimtengeneza haswa alimpa mbuzi beberu akamshika kwa mkono mmoja akimnyanyua juu, kuna maneno aliambiwa ayarudie kuyatamka wakati anayatamka basi yule mbuzi aliwaka moto akapukutika bila kuwashwa mpaka akabaki majivu. Tukio lilifanyika alfajiri kabla ya swala ya asubuhi.

Hii imetokea ilala hapo sio muvi, na huyo msanii alipewa masharti mengi sana ikiwemo kutogusana na yoyote ili kutovuruga power yake.

So haya mambo yapo msichukulie poa lolote lisemwalo linawezekana.
 
Back
Top Bottom