Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Sooner they will start sending the attacks to Rayvanny, Matter of fact the kid has no hard skin like his brother Harmonize then will forget him soon.
Don't judge a book by it's cover, Rayvanny is by far more organised and he can play the game 'underwater' without making noises.
Silent snipers are more dangerous and more effective.
 
Kukataliwa na BSS sio kigezo kwamba fulani hajui muziki na hatakuja kufanikiwa. Wangapi walipoanza safari yao walikutana na vikwazo hivyo hivyo lakini hawakukata tamaa mpaka wakafanikiwa? Diamond mwenyewe unajua ni kwa kiasi gani amesota wakati anaanza safari ya muziki na alikatishwa tamaa mara ngapi?
 

Sawa kabisa mkuu.
Tatizo wanaolalama wengi muziki unavyozalishwa mpaka kuwa mzuri machoni na masikioni hawajui.
Na hii ni moja kati ya biashara ngumu msanii kufanya pekeake, kuna watu wanamshangaa mondi kuwaajiri na kuwalipa Babu tale,Salam na mkuu fela...Ni kwamba anajua ili ufike mjini kama watokea kijijini ni lazima ushikwe mkono na uelekezwe njia na waliotangulia kuja mjini fastaa utafika town na ndo anachokifanya mondi.
 
Hivi unajua Diamond mwenyewe pamoja na talent yake ila ALIMUOMBA PAPA MISIFA amsaidie baada ya THT kumwambia hajui kuimba?

Unali fahamu hili,sometimes huruma na moyo wa mtu kuweka hela yake.
 
Mkuu wakati the late Ruge akifanya haya mbona alishutumiwa sana kuwanyonya wasanii akiwepo huyu Dai?[emoji38]..
Hata kama alishutumiwa hilo haliondoi ukweli kuwa unapowekeza kwenye biashara lengo kuu ni kupata faida na lazima utengeneze mazingira ya kuipata hiyo faida, kumbuka kuna uwezekano wa kupoteza kila ulichowekeza kwa msanii husika(risks). Msanii anaweza kufariki wataki umeshawekeza hundreds of of millions au kuugua permanently au kuangukia kwenye madawa ya kulevya and so on and so forth, hivyo kuwekeza huwa ni kama kamari tu yaani pata potea.
So kwa yalisemwa kwa Ruge it's not an excuse ya kuzuia watu wasiwekeze kwa lengo la kupata faida na ukumbuke msanii wakisham-brand hilo hawezi kulifuta anakuwa ametengenezewa faida ya kudumu.
 
Hushawahi kusikia Konde kasema alikuwa anaingizia kiasi gani?

Au may be label yoyote Tanzania au Africa ushawahi kusikia wakisema wameingiza kiasi fulani kutoka kwa msanii fulani?
Akikujibu uni-tag tafadhali.
 
HAO NDO WANAOKURUPUKA NA KUSHINDWA KUELEWA ALICHOKISEMA DIAMOND. NASHINDWA KUAMINI KAMA HUJAELEWA AU UNAENDESHWA NA CHUKI AMA ROHO MBAYA
 
Diamond alisaidiwa na papaa misifa.
Harmonize alisaidiwa na Diamond
Rayvanny alisaidiwa na Diamond

Huu ni ukweli hatuwezi kubadilisha hata kama msaada ulizaa biashara. Nikikupa dili ya kutengeneza pesa hata kama utaweka nguvu yako lakini nimekusaidia.
 

BASATA wakijitia kimbelembele hao wasanii watawasaini wao.
 
Sio lazima... Lakini at least acknowledge mchango wake kwenye mafanikio yako na sio kutumia rungu la kusema umemchukua wakati hana jina na umewekeza hela kwake as if hana mchango wowote kwako.
Post 104 ujaijibu
 
Tulipandikizwa kuchukia kila anaefanikiwa toka zamani kutokana na sera na siasa zetu.Vile tu huyu n mwenzetu aah anaendeshaje gari kali,mbona kajenga na ana biashara fulani ,tunaenda kumchomea kwa mamlaka ili afilisike tumcheke. Ndo maana sisi hatuna tabia ya kusaidiana sababu tunachukiana sana.
Na hao wakongwe mi heshima yangu kwao ilishashuka zamani,wana chuki sana na wasanii wa leo,sikiliza argument zao kweney ishu kama aina ya muziki(amapiano) kwa mfano ndo utajua unafiki wao kwa madogo.NI ROHO MBAYA TU!!
 
Mikataba yao ikoje??tusiweke hisia kwenye hela aisee
 
Ushasikia popote Mavin Records wameingiza kiasi gani na wasanii wao wamegawiwa kiasi gani??
Tatizo la sisi bwana hakuna kitu hatujui,yyani tunaongozwa na chuki tuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…