Ninja assasin
JF-Expert Member
- Jul 2, 2018
- 2,512
- 5,848
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo jeuri ya kumuona Zari msukule utaitolea wapi?Hamna sio hivyo bali maboresho ya ignore list yananipunguza kasi. Team domokaya msiniweke ignore list ee. Zari akirudia matapishi yake nae ntamuona msukule tu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Hiyo jeuri ya kumuona Zari msukule utaitolea wapi?
Moyoni ulipo umefurahi ile mbaya kumuona yupo karibu na diamond imagine wakirudiana rasmi si utafanya sherehe kabisa huo ndio ukweli wenyewe hayo mengine unaongea lakini si kutoka moyoni.Mimi sio kama wewe. Am free soul. Wait and watch
Moyoni ulipo umefurahi ile mbaya kumuona yupo karibu na diamond imagine wakirudiana rasmi si utafanya sherehe kabisa huo ndio ukweli wenyewe hayo mengine unaongea lakini si kutoka moyoni.
[emoji23][emoji23] huko aliko anaandaa bomu RobidinyoMond amewalipa billboard wam promote in Robidinyo voice[emoji16][emoji16][emoji16]
Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣wapiga ramli wa mondi taarifa hizi kwao ni chungu sana...
anewei endeleen kupga ramli huenda kuna siku shetani atazijibu maana mungu hua hajibu upumbavu wa wajinga
Kwani diamond na tanasha wamerudi na? Mpaka useme diamond hawezi kuwa na mama wawili?Team dona tulia basi Zari akirudi jua final say na domokaya watagombana vibaya mno. Domo hawezi kua na mama wawili ujue
kwani alikiba anaweza akawa anaumia katika hili...?maisha hayajawahi kua sawa, kiba na beki3 wake robidinyo wakihangaika kupost ujio wa kingoma chao kipya huku mwenzao anatolewa mfano na BILLBOARD, dah! sina chakuwaambia kiba & bek3 wako robidinyo isipokua kuwapa pole kwa maumivu mnayougulia mda huu
Kwani diamond na tanasha wamerudi na? Mpaka useme diamond hawezi kuwa na mama wawili?
Unge expand mpk kwa Konde gang Tembo mbona umemkata?
Mtandao maarufu wa kupanga charts za muziki duniani wa Billboard umeachia makala wakielezea namna ya kupata mafanikio kimataifa kwa kutumia mtandao wa Youtube huku wakimtolea mfano star wa muziki wa Tanzania @Diamondplatnumz
Makala hiyo imeandikwa "Wanamuziki wa Marekani wanatafuta njia za kutoboa kwenye Youtube, Wanapaswa kusoma mikakati ya kufanya na kuachia video kutoka kwa wasanii wa Kiafrika."
Wasanii wa Magharibi wanaweza kujifunza kutoka kwa kile wanachokifanya wasanii wa Kiafrika , haswa wale ambao wamefanikiwa kimataifa," Amezungumza meneja wa 'Youtube Music Trends' Kevin Meenan, ambaye anasimamia ukusanyaji na uchambuzi wa data za chati za Muziki za YouTube. Ameelezea kuwa alivutiwa sana na mbinu pamoja na ubunifu ambao anautumia msanii wa bongo flava wa Tanzania Diamond Platnumz kwenye chaneli yake ya YouTube - sehemu moja tu ya mikakati ya ujasiriamali ambayo inajumuisha kituo cha redio ya FM na TV pamoja na usimamizi kamili wa huduma, kurekodi, kuchapisha na kampuni ya burudani, @WCB_Wasafi.
Kwenye Makala hiyo Kevin Meenan amesema Ukubwa wa diamond kwenye Youtube ni wakustaajabisha akiwa na Subscribers Millioni 3.6 na zaidi ya jumla ya views Millioni 980 huku 80% ya watamazaji wakiwa wanatokea nje ya Tanzania. Kwa kipimo cha kipindi cha kutoka Mei 1, 2019 hadi Mei 1, 2020 Meenan anasema kwamba, kimataifa Diamond alitazamwa zaidi na watu wa Nchini ya Kenya ikifuatiwa na Tanzania na Marekani.
Billboard wameeleza kuwa Msimamizi huyo wa Youtube Trending alishangazwa kukuta Diamond ameweka zaidi ya video 600 kwenye mtandao wa Youtube "Kwa kweli ilibidi nichunguze mara tatu ili kuhakikisha kuwa ilikuwa sawa," Alielezea. Wamesifia kuwa Diamond anaweza kuweka hadi video 20 akitangaza Official video moja tu huku wakitolea mfano wa wimbo wa Jeje ambapo ukiachana na Official video, kuna dance video, cartoon video, lyrics video pamoja na official audio.
Kwenye Makala hiyo Billboard wameelezea kuwa uchunguzi wao umegundua kuwa wasanii wengi ambao wamefanikiwa kufikisha subscribers zaidi ya Million 1 basi huwa wanatazamwa zaidi na watu wa nje ya nchi zao.
View attachment 1466160
Sent using Jamii Forums mobile app
Kijana ajitahidi awafikie hao juu hapo! View attachment 1466675
Kwa nini Harmonize umemkata?