Msanii na mfanyabishara mkubwa sana nchini Tanzania, Diamond Platnumz amewataka watu wa Mbeya kujivunia Spika wa Tanzania na Duniani Madam Tulia Ackson. Diamond ameonekana kuvutiwa na namna Madame Tulia alivyoongoza mjadala mgumu wenye hisia kali kutoka kwa watu wenye weredi duniani aliongoza kwa ustadi mkubwa bila kuteteleka.
Sisi pia wazalendo wa nchi hii tunaungana na Diamond Platnumz kujivunia kuwa na mwanamama shupavu na kiongozi wa mfano ambaye dunia imezizima kwa uwezo alioonesha kwenye leadership, decision making, public speaking, influencing, supervision nk .
Ama kwa hakika hatupaswi kulipoteza ili jembe kwa sababu ya mihemko ya kisiasa.
Yule mvaa mlegezo anaejua kusoma, kuandika na kutukana matusi ya nguoni ni wakati sasa ajikite kwenye upishi kama mwenzie shilole maana kwenye muziki akiimba watoto wanamcheka.
Soma: Tulia Ackson awataka viongozi wa magharibi kumheshimu. Ni baada ya kushambuliwa kuhusu kukutana na Vladmir Putin