Kipi wanachofanya Ccm hakikufanywa na Serikali ya Makaburu Afrika Kusini na ya Sheik Hasina Bangladesh?
Wote waliteka watu, wakafunga watu kwa kesi za uongo, walipoteza watu na kulawiti watu. Na haya yote yanafanywa sasa na ccm
Wote wamenyanyasa watu na kuziteka taasisi zote zinazoweza kuhakikisha mifumo inakuwa na checks and balances. Na haya yameshafanywa na ccm hapa Tanzania.
Unataka hatua zichukukiweje? Watu hawakuandamana? Hawakuuwawa? Unataka wandered kuandamana na kuuwawa?
Kwani wapi imeandikwa hadi mchukue hatua kwa muda mrefu ndo mnaweza pata msaada?
Nimeshakwambia. Wewe endelea kuishi kwa kufadhiliwa na hao mafisadi ili kurdish nyuma harakati ila sisi wengine haturudi nyuma na hatutorudi nyuma.
Jitihada zetu zitaendelea bila kukoma na ipo siku insha Allah tutapata matokeo mazuri kama Watanzania wapenda haki.
Sijasema kuna walichofanya CCM ambacho hakijafanywa na Hasina na makaburu, so why are you asking about this?
What is the relevance of this question? What is the logic of this question?
Nasema wewe hutakiwi kujifananisha na ANC wala watu wa Bangladesh kwa sababu hujafanya kazi waliyoifanya.
Hujaandamana hata kwa wiki mfululizo.
Wenzako wamefanya kazi yao kabla ya kusaidiwa. Hata watu wakiwasaidia wanaona hawa wanefanya hiki.
Wewe unataka kusaidiwa kabla hujafanya kazi unayotakiwa kufanya.
Pia, acha ujinga wa ad hominem attacks za kusema mimi naishi kwa kufadhiliwa na mafisadi. Vinginevyo weka ushahidi hapa.
Mimi ningetaka hayo maisha ya kuishi kwa kufadhiliwa na mafisadi ningeweza hapohapo Tanzania, lakini niliyakataa nipo Marekani nafanya kazi zangu karibu miaka 30 sasa. Hakuna anayenijua huku na survive kwa skills zangu. Out of all those years hata kuja Tanzania nimekuja like some 3 weeks tu mwaka 2012 kwa ajiki ya harusi ya famikia.
Najua nchi ua kifisadi sitaki hata kuja likizo.
Huku hakuna kuishi kwa kufadhiliwa na mafisadi wa Tanzania acha uongo na ujinga wa kumpakazia kila mtu anayekushinda kwa hoja kuwa anaishi kwa kufadhiliwa na mafisadi wa Tanzania.
Mimi nimefanya kazi kubwa Wall St. New York City, kazi ambazo huwezi kufanya kwa kufadhikiwa na mafisadi wa Tanzania. Kwa nini unanipakazia hiki kwa sababu huwezi kujibu hoja tu?
This is clearly ad hominem logical fallacy. Umeshindwa kujibu hoja, unamtukana personally mtoa hoja.
Bado hujajibu hoja.
Acha ujinga wa kunizushia uongo kwa sababu huwezi kujibu hoja.
Hoja ni hii.
Kutaka Marekani ije kumkamata Samia na kufanya regime change Tanzania ni ujinga kwa sababu Marekani yenyewe ina nefarious national interest zisizoendana na interests za Watanzania wengi.
Kwamba hata Marekani ikimuondoa Samia itamuweka kibaraka wake ambaye anaweza kufanya resource grab kubwa kuliko ya Samia, na akalindwa na nguvu kubwa ya Marekani msiweze kumuondoa.
Tumeona hilo Congo baada ya Marekani kumuweka Mobutu, nchi imesambaratika mpaka leo haijakaa sawa.
Huelewi wapi?