Diaspora mliopo Marekani tusaidieni kupata Arrest Warrant ya Samia na Wasaidizi wake katika Mahakama yoyote ya Marekani

Kwani wapi imeandikwa hadi mchukue hatua kwa muda mrefu ndo mnaweza pata msaada?
Hebu msome vizuri Kiranga bila mhemko wala midadi.

Hoja yake ambayo ni ya wengine pia, kabla ya kuwaita wamarekani sisi wenyewe tumefanya nini kwa ukubwa upi na kwa muda gani?

Jee maandamano yetu yaliratibiwaje na matokeo yake yanapimwaje?

Jee yalikuwa ni maandamano ya kutuma ujumbe kwa watawala ama yalikuwa ni maandamano kushinikiza kuwaondoa watawala madarakani na kubadili mfumo?
 
Sijasema kuna walichofanya CCM ambacho hakijafanywa na Hasina na makaburu, so why are you asking about this?

What is the relevance of this question? What is the logic of this question?

Nasema wewe hutakiwi kujifananisha na ANC wala watu wa Bangladesh kwa sababu hujafanya kazi waliyoifanya.

Hujaandamana hata kwa wiki mfululizo.

Wenzako wamefanya kazi yao kabla ya kusaidiwa. Hata watu wakiwasaidia wanaona hawa wanefanya hiki.

Wewe unataka kusaidiwa kabla hujafanya kazi unayotakiwa kufanya.

Pia, acha ujinga wa ad hominem attacks za kusema mimi naishi kwa kufadhiliwa na mafisadi. Vinginevyo weka ushahidi hapa.

Mimi ningetaka hayo maisha ya kuishi kwa kufadhiliwa na mafisadi ningeweza hapohapo Tanzania, lakini niliyakataa nipo Marekani nafanya kazi zangu karibu miaka 30 sasa. Hakuna anayenijua huku na survive kwa skills zangu. Out of all those years hata kuja Tanzania nimekuja like some 3 weeks tu mwaka 2012 kwa ajiki ya harusi ya famikia.

Najua nchi ua kifisadi sitaki hata kuja likizo.

Huku hakuna kuishi kwa kufadhiliwa na mafisadi wa Tanzania acha uongo na ujinga wa kumpakazia kila mtu anayekushinda kwa hoja kuwa anaishi kwa kufadhiliwa na mafisadi wa Tanzania.

Mimi nimefanya kazi kubwa Wall St. New York City, kazi ambazo huwezi kufanya kwa kufadhikiwa na mafisadi wa Tanzania. Kwa nini unanipakazia hiki kwa sababu huwezi kujibu hoja tu?

This is clearly ad hominem logical fallacy. Umeshindwa kujibu hoja, unamtukana personally mtoa hoja.

Bado hujajibu hoja.

Acha ujinga wa kunizushia uongo kwa sababu huwezi kujibu hoja.

Hoja ni hii.

Kutaka Marekani ije kumkamata Samia na kufanya regime change Tanzania ni ujinga kwa sababu Marekani yenyewe ina nefarious national interest zisizoendana na interests za Watanzania wengi.

Kwamba hata Marekani ikimuondoa Samia itamuweka kibaraka wake ambaye anaweza kufanya resource grab kubwa kuliko ya Samia, na akalindwa na nguvu kubwa ya Marekani msiweze kumuondoa.

Tumeona hilo Congo baada ya Marekani kumuweka Mobutu, nchi imesambaratika mpaka leo haijakaa sawa.

Huelewi wapi?
 
Nimemsoma na sijaanza kumsoma Leo.

Mpo kinadharia kwa nia mnazozijua wenyewe.

Watanzania tumechoka ufisadi, tumechoka rushwa, tumechoka uonevu, tumechoka kutekwa, kupambikiwa kesi, kuonewa, kupotezwa na sasa yamefika hadi mambo ya ulawiti.

Watanzania hatuangalii juhudi za kupambana na haya zitachukua muda gani? Tunachotaka ni haya mambo kukoma kwa namna yeyote itakayowezekana.

Hatutaacha kuomba msaada. Na tutaomba msaada kwa nguvu zote. Hadi tutakaowaomba msaada watusikie.
 
Wewe ndiye upo kinadharia.

Hakuna Mmarekani anayekuja kumtoa Samia.

Unajipa umuhimu ambao huna kwa Wamarekani.

Get that through your head.
 
Wewe ndo huna hoja. Kwani kuishi Marekani kunaondoa hoja kuwa wewe ni sehemu ya wanufaika wa ufisadi na udhalimu unaoendelea Tanzania?

Kwani kote wanapoomba msaada kusaidiwa kuondolewa tawala dhalimu wanaomba kwa watu engine wakiamini ni Malaika?

Marekani anaweza kuwa na mapungufu yake ila kwa hatua tuliyofikia sasa Tanzania hatutaki tena kutekwa, kupotezwa, kulawitiwa na kupewa kesi za uongo.

Tunachotaka Tanzania ni kusaidiwa kuondolewa kwa hawa madhalimu wanaoishi kwa kumwaga damu zetu huku wakifurahia.

Tutaomba msaada kwa yeyote aliyd tayari kutusaidia na hatutaacha kuomba msaada kwa yeyote.

Haijalishi Marekani ni shetani au Malaika sie tunachotaka ni kusaidiwa kuondolewa kwa hawa madhalimu wanaotunyanyasa.

Unatoa mifano ya sehemu mbaya mie nimekupa mifano ya sehemu ambazo waliashirikiana na Marekani na wapo vizuri hadi Leo.

Wewe chukua mfano wa Congo na kwingineko mimi nachukua mfano wa Korea Kusini
 

First things first.

Weka ushahidi hapa kuwa mimi ni mfaidika wa ufisadi na udhalimu unaoendelea Tanzania.

Hii ni serious allegation naichukulia seriously.

Ukishindwa wewe ni muongomuongo unayeunganisha na kuzusha mambo bila hoja.

Weka ushahidi hapa.

Weka ushahidi hapa acha longolongo.
 
Kiranga achana na kumjibu mambo yako binafsi... Rejea kwenye hoja.

Lord Denning hebu elezea sisi kama Taifa ni kwa nini tunataka wamarekani waje waingilie jitihada zetu za kuibadili nchi yetu kwa kuondoa mfumo mbovu uliopo na watawala waliopo?
 
Kiranga achana na kumjibu mambo yako binafsi... Rejea kwenye hoja.

Lord Denning hebu elezea sisi kama Taifa ni kwa nini tunataka wamarekani waje waingilie jitihada zetu za kuibadili nchi yetu kwa kuondoa mfumo mbovu uliopo na watawala waliopo?
Ni mubimu kiweka rekodi sawa, kanichafua.

Kama huyu ni mtu mjingamjinga, mzushimzushi, muongomuongo tu, ni muhimu hilo lijulikane na wote hapa.
 
Ushahidi ni namna unavyotetea utawala huu wa kidhalimu usitolewe.

Kuna lolote linaloweza kukutambulisha wewe ni mtu waxnamna gani zaidi ya hilo?


Huwezi kuwa mtu wa haki wakati unasimama kutetea madhalimu. Never
 
Ushahidi ni namna unavyotetea utawala huu wa kidhalimu usitolewe.

Kuna lolote linaloweza kukutambulisha wewe ni mtu waxnamna gani zaidi ya hilo?


Huwezi kuwa mtu wa haki wakati unasimama kutetea madhalimu. Never
Hakuna ushahidi kuwa natetea utawala huu dhalimu usitolewe.

Ila wewe umeweka ushahidi hapa kuwa wewe ni mjinga.

Unaona kila mtu anayepinga hoja ya kumualika Mmarekani kuja kuutoa utawala huu ni mtu anayeutetea utawala huu dhalimu.

You are an idiot making a false dichotomy logical fallacy.

Kwani utawala huu hauwezi kuondolewa bika wewe kumuita Mmarekani?

Kwa nini unamuachia Mmarekani afanye kazi unayotakiwa kufanya wewe wakati Mmarekani ana interest zake tofauti na zako?
 
Hawa watu wapo desperate sana! Wana utoto mwingi mno. Awali ungeweza fikiri wana akili sawa sawa juu ya tambo na mipango kabambe ya kupigana na CCM kumbe na ni wale wale wazee wa 'talk shops'
 
Hawa watu wapo desperate sana! Wana utoto mwingi mno. Awali ungeweza fikiri wana akili sawa sawa juu ya tambo na mipango kabambe ya kupigana na CCM kumbe na ni wale wale wazee wa 'talk shops'
Wajinga sana. Na ukishangaa kwa nini CCM wanadumu kwenye madaraka, ukianza kuwasikiliza wanaharakati na wapinzani kama hawa unaanza kuelewa kwa nini CCM wanawashinda.

These people are bitching like Karens with their fantasies, like America cares.
 
Ile siku Lissu alipokamatwa mkarudisha mikia nyuma nilimsikitikia sana Lissu kwa jeshi alilojiamini nalo lote limeingia shimoni. Nikawatolea mfano Kesha Ruto asingeweza fanya vile kwa Odinga au Gachagua!!

Mmejawa na midomo sana mitandaoni na mko too desperate!! Hata wale waliokua na uwezo wa kuwasaidia hata kifedha Ndani ya CDM mliwatukana na kuwadhalilisha sana!! Huwezi kuwa na adui CDM na CCM kwa wakati mmoja ukajiona mjanja zaidi ya Mjinga!!

Mna safari ndefu sana na hata ile hofu ndogo ambayo CCM ilikua nayo juu yenu imeyeyuka!!
 
Wajinga sana. Na ukishangaa kwa nini CCM wanadumu kwenye madaraka, ukianza kuwasikiliza wanaharakati na wapinzani kama hawa unaanza kuelewa kwa nini CCM wanawashinda.

These people are bitching like Karens with their fantasies, like America cares.
Halafu si watu ambao wana feeling ya utaifa ndani yao. Nakubali simpendi Samia wala CCM kama ambavyo sikumpenda Magufuli. Lakini katika yote hayo siwezi vuka mipaka yakufikia kutamani kurudi walikokutoa kina Nyerere!! Sijawahi tamani Tanzania ipoteze Sovereignity yake kwa uvamizi wa wageni!

CCM haitodumu milele kama ambavyo mimi au Samia pia hatutadumu lkn Nchi yetu inaweza kudumu!!

Hawa watu unaweza wafananisha na baba mwenye mji wake anaefurahia au kutamani aje tawaliwa na mwanaume mwenzie kwenye mji wake!!

Ni watu wapumbavu sana na kama umegunduq kadiri siku zinavyosonga wenye akili wanaanza kuwapuuza.

Kile kipindi cha 29 october huyo jamaa alikua akitoa maagizo kwa jeshi eti chukua Bunge mara chukueni INEC sijui chukueni Ikulu 🤣🤣🤣🤣 unabaki unashangaa huku ndo kukinukisha?
 
Hawa watu wapo desperate sana! Wana utoto mwingi mno.

Kwanza usiongee kwa wingi. Kwenye harakati za kuiondoa CCM kuna kila aina ya watu na wengi wao ni makini.

Kubadili mitizamo ya ubwege mtozeni kutoka kwa watu wengi wanaoiunga mkono na kuilinda CCM siyo tukio bali ni mchakato.

Wengine hatuna haraka iko siku inakuja watanzania wataondokana na CCM. ANC ya Afrika ya kusini ilianzishwa mwaka 1912 lakini ilishika dola miaka 82 baadae mwaka 1994, ndiyo ikashika dola.

Wabinafsi wanaowaza kuwa CCM itaitawala milele!!
 
Hawa wajinga hawaelewi kuwa CCM na Samia ni tatizo dogo ambalo tunaweza kulimaliza ndani ya miaka michache, na ubeberu wa Marekani ni tatizo kubwa sana ambalo tukijiingiza inaweza kutuchukua zaidi ya miaka 100 kulimaliza.

Ukijibizana nao unagundua ni watu wajinga wasioelewa historia, wasioelewa geopolitics, wasioelewa logical thinking, wasiojitambua.
 
CCM itaondokaje madarakani?

Mimi nasema haiwezi kuondoka. Na sababu kuu ni Stockholm’s syndrome.

Kama unabisha, tuweke dau hapa….
 
Acha Mmarekani atetee interest zake na sie tutetee interest zetu.

Hata ANC ilichukua muda kuweza kuishawishi jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua dhidi ya Makabulu na siku ya mwisho walifanikiwa.
Kile kipindi cha mwanzo kabisa cha harakati zenu nilikwambia umechanganyikiwa ukanitukana! Kadiri siku zinavyokwenda kila mwenye akili anang'amua hilo kuwa umechanganyikiwa!! Mbaya zaidi una nafasi huko CDM sidhani kwa hii thinking kuna mahali mtafika!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…