Dilemma: Je, nimwandikishe jina lake kwenye mali zangu au nikubali tuachane?

Ndugu zangu wanaJF, habari zenu!!!

Nimekuwa mfuatiliaji wa mada za JF tangu 2018 na nimekuwa nikivutika mno na elimu itolewayo hapa jukwaani lakini sikuona haja ya kujiunga kama member kwa kuwa nilihisi sina chochote cha kuchangia hapa,ila sasa nimeamua kujiunga rasmi ili kupata ushauri kuhusu tatizo linalonisumbua.

Mimi ni mtu mwenye hali nzuri ya kifedha. Nina nyumba tatu za kisasa na magari mawili (SUV ya kifahari na sedan ya kisasa).

Hata hivyo, hivi karibuni mpenzi wangu ambaye nipo naye mwaka wa tatu sasa ameniambia kwamba anataka niandikishe jina lake kwenye mali zangu, akisema kuwa nisipofanya hivyo basi huo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu.

Nampenda sana na sidhani kama ningependa kumuumiza kwa kumkatalia, lakini watu wa karibu wamenishauri nisithubutu kufanya hivyo. Najiuliza, je, ni sahihi kumwandikisha jina lake kwenye mali zangu, au nifanyeje?

Nahitaji ushauri wenu wa busara.

Asanteni!!!
Huyo Hana mapenzi ya kweli mpaka anapata na ujasiri wa kukwambia mshee mali zako yaani usijichanganye kabisa utakuja lia na kusaga meno
 
Ndugu zangu wanaJF, habari zenu!!!

Nimekuwa mfuatiliaji wa mada za JF tangu 2018 na nimekuwa nikivutika mno na elimu itolewayo hapa jukwaani lakini sikuona haja ya kujiunga kama member kwa kuwa nilihisi sina chochote cha kuchangia hapa,ila sasa nimeamua kujiunga rasmi ili kupata ushauri kuhusu tatizo linalonisumbua.

Mimi ni mtu mwenye hali nzuri ya kifedha. Nina nyumba tatu za kisasa na magari mawili (SUV ya kifahari na sedan ya kisasa).

Hata hivyo, hivi karibuni mpenzi wangu ambaye nipo naye mwaka wa tatu sasa ameniambia kwamba anataka niandikishe jina lake kwenye mali zangu, akisema kuwa nisipofanya hivyo basi huo utakuwa mwisho wa mahusiano yetu.

Nampenda sana na sidhani kama ningependa kumuumiza kwa kumkatalia, lakini watu wa karibu wamenishauri nisithubutu kufanya hivyo. Najiuliza, je, ni sahihi kumwandikisha jina lake kwenye mali zangu, au nifanyeje?

Nahitaji ushauri wenu wa busara.

Asanteni!!!
Ndugu hali nzuri ya kifedha uliyonayo ukashindwa tatua suala dogo namna hii mpaka ukaja huku

Chief Godlove kuna mtu anakuaibisha huku
 
Back
Top Bottom