Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Marehemu ni fala sana, kwanini alitoa siri aliyoishi nayo kwa muda mrefu. Angebaki nae aende nayo kwa Mungu.

Haoni km atamuacha mtoto kwenye mazingira magumu sana km hivyo baba hampendi tena binti.

Huyu baba anaweza fanya tukio baya sbb anaona siyo damu yangu na kisasa.

Sijapenda kbs kitendo cha marehemu kutoa siri hizi ni siri za kufa nazoooo.
 
Huyo mke aliharibu sana.
Ingawa alitubu baada ya kuona maiti mbele yake akaona ile dhambi inaweza kumzuia kuingia mbinguni.
Ni vizuri alitubu na kumuomba mumewe msamaha!
Hii case ngumu sana.
Hili ni jaribu zito kwake, asipokaa vizuri na nafsi yake soon naye atakufa.
Ndiyo maana tunajaribu kumsaidia, ana watoto watano wanaomtegemea kama mzazi pekee.
Vijana tuache dhambi, dhambi inaua roho na mwili
💯 🔥
 
Yani uleee bao la mwanaume mwingine na unajua!!!


Huo ni ukichaa


Piga chini mtoto peleka Kwa baba yake
Mbona mke kalea mapacha ambao hawakutokana na tumbo lake

Huyo mtoto anajua baba halisi ni wewe, mlee kwa upendo kama tunavyowajali yatima wengine

Vipi kama mke aliamua kusema hayo kwa kudanganya ili akupe maumivu kama alihisi yeye wakati unamletea mapacha
 
Mimi tu siwez kudate na mwanamke ambae ninamjua X wake. Ndio ije kuwa naona mtoto wa shahawa zingine za mwanaume mwingine na evidence za mtoto zipo. THUBUTU.


Maisha ni Episode za movie Kila mtu Dunian ana script yake kuonesha. Hakikisha unaenjoy maisha yako. Episode yako ikiisha unashuka jukwaani ( kifo ) wanaendelea wengine.

Hakuna kulipwa ubaya.
Hakuna kulipwa mazuri.

Tenda usiyotaka kutendewa.
 
Kubwa sana analopaswa kuzingatia kwa sasa ni hatima ya huyo mtoto, maamuzi yake yamebeba hatima ya huyo mtoto (Izingatiwe mtoto hana kosa lolote katika hili tukio), kwa sababu mtoto anaye anahisia, hatujui atalipokeaje atakapo ambiwa.
Nina mshauri aendelee kumlea huyo mtoto kama kawaida, na ukizingatia wahusika wote hawapo, hajui nini MUNGU ameweka ndani ya huyo mtoto, ajitahidi kuvumilia muda unavyokwenda hasira zitapungua.

Mtafutie watu wazima wenye hekima wamshauri na kumjenga kisaikolojia.

MUNGU aponye moyo wake ulioumia.
 
Uneshasema yatima ni mtu asie na wazazi. Yatima namlea kwasababu sijasalitiwa.


Huyo mwanamke kama alisamehe ni yeye na misingi yake.

Acha assumption za kama mke aliamua kusema uongo. Uongo Gani na DNA imethibitisha mtoto sio wake.
 
Ushauri mzuri wa kuomba msaada wa Mungu, nimeupokea nitamfikishia.
 
Mwambie asisahau huyo mtoto ana kaka zake ambao wanamuita baba.
 
Tuliza komwe lea mtoto wake wake wanaweza kuja kuwa vibudu huyo wa jamaa akasaidiwa big time kubabako wewe mwenyewe msaliti alafu unamlaumu marehemu.
 
Kitanda hakizai HARAMU KAMWE!
ATUNZE TU KAMA WA KWAKE.
 
Binti wa zamani Je Baba mzazi wa huyo mtoto aliye fariki miaka 5 iliyopita kwa ajali,yeye binafsi alikua anaijua hiyo siri kua alimzalisha mke watu? alikua anajua kua kuna mtoto wake kwa mke wa mtu?
 
Si umeona hapo huyo baba mtoto kafariki mkuu
Mkuu,ukiusoma uzi vizuri,mleta mada amesema kua Baba mzazi wa huyo mtoto alisha fariki miaka 5 iliyopita kwa ajali.
Shukrani kwa kunirekebisha na kunikumbusha.
Anachotakiwa akamtambulishe mtoto kwao, huko ndiyo wampatie ruhusa ya kulea maana mama wa mtoto hayupo tena ila kwao na mtoto wapo. So akawaombe hao, bado ni mtoto wa watu, hawajamkataa.
 
Mwambie asisahau huyo mtoto ana kaka zake ambao wanamuita baba.
Aiseeeh hakuna mtu ameongelea hili, asante sana.
Nimelichukua hili na nitamkumbusha kwamba huyo mtoto ni ndugu wa watoto wake wa damu na hiyo ni sababu tosha ya kumlea ili kuwabakisha ndugu wa mama mmoja wawe karibu kwa pamoja.
 
Uneshasema yatima ni mtu asie na wazazi. Yatima namlea kwasababu sijasalitiwa.


Huyo mwanamke kama alisamehe ni yeye na misingi yake.

Acha assumption za kama mke aliamua kusema uongo. Uongo Gani na DNA imethibitisha mtoto sio wake.
Kila mmoja na maoni yake, yangu yalikuwa hayo

Kwani ukimlea huyo mtoto unapungukiwa Nini

Wanaume tunapoteza hela ngapi kwenye uchi

Huyo mtoto anakugharimu milioni ngapi hadi ushindwe kumlea pamoja na watoto zako uliyezaa kwa kumsaliti mkeo

As a gentleman, tunafunika kombe mwanaharamu apite

Kitanda hakizai haramu
 
Kuna siri unatakiwa ufe nazo
 
Shukrani kwa kunirekebisha na kunikumbusha.
Anachotakiwa akamtambulishe mtoto kwao, huko ndiyo wampatie ruhusa ya kulea maana mama wa mtoto hayupo tena ila kwao na mtoto wapo. So akawaombe hao, bado ni mtoto wa watu, hawajamkataa.
Upo sahihi kabisa,mtoto pia anayo haki ya kuwajua upande wa Baba yake mzazi.
 
Binti wa zamani Je Baba mzazi wa huyo mtoto aliye fariki miaka 5 iliyopita kwa ajali,yeye binafsi alikua anaijua hiyo siri kua alimzalisha mke watu? alikua anajua kua kuna mtoto wake kwa mke wa mtu?
Hilo hatujui, baba mzazi alifariki almost miaka 2 baada ya mtoto kuzaliwa.
Bado haijulikani kama mke alimwambia huyo shemeji kama mtoto ni wake au naye alimificha pia.
 
Aiseeeh hakuna mtu ameongelea hili, asante sana.
Nimelichukua hili na nitamkumbusha kwamba huyo mtoto ni ndugu wa watoto wake wa damu na hiyo ni sababu tosha ya kumlea ili kuwabakisha ndugu wa mama mmoja wawe karibu kwa pamoja.
Mkumbushe kuna hatari ya upendo wa watoto wake kwake kuingia doa iwapo watashuhudia mdogo wao akinyanyasika.

Mwambie hana cha kupoteza kumjali huyo mtoto sababu hana baba mwingine anayemfahamu zaidi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…