Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
- Thread starter
-
- #121
Asante kwa kumfafanulia, ila mimi wa zamani pia nimeanza kupoteza usikivu, mniombee nisije kuwa kiziwi nikaanza kugombea username na binti kiziwi 😂Mkuu,mleta mada sio binti kiziwi ni Binti wa zamani naona umechanganya ila wote ni Mabinti,mmoja ni wa zamani na mwingine ni kiziwi.
Maadam mke wake aliamua kumwambia ukweli, bas na yeye ana wajibu wa kuwatafuta ndugu upande wa mtoto akamtambulishe mtoto kwao, halafu halafu awaombe, ndugu wakimruhusu ndiyo aendelee kuishi naye.Baba wa kweli kibaiolojia alishakufa.
Busara nzuri, nitamfikishiaMaadam mke wake aliamua kumwambia ukweli, bas na yeye ana wajibu wa kuwatafuta ndugu upande wa mtoto akamtambulishe mtoto kwao, halafu halafu awaombe, ndugu wakimruhusu ndiyo aendelee kuishi naye.
Nado mtoto ana haki ya kuujua ukweli na kuwajua ndugu zake ili mradi hawakumkataa
Umenena vyema, siongezi neno, ushauri nitaufikisha.Mwanaume ampende huyo mtoto ili aishi maisha marefu ya furaha, kumchukia huyo mtoto kwa sasa hakutamsaidia chochote, zaidi hiyo chuki itamharakisha nae kwenda kaburini aache watoto wao yatima.
Anatakiwa kufanya kila awezalo arudishe upendo wake kwa huyo mtoto, kwanza mtoto hana kosa lolote, yeye ni matokeo ya makubaliano haramu kati ya marehemu wawili.
Siyo kawaida yangu kuandika kutokana na kuwa bize na moderationMke wa ndugu yetu amefariki baada ya kuumwa kansa kwa muda mrefu, kabla hajafariki amefichua siri kwa mumewe kwamba mtoto wao wa mwisho si mwanae bali ni mtoto wa shemeji (rafiki wa mumewe) ambaye alishafariki kwa ajali miaka 5 iliyopita.
Kabla ya usaliti, huyo shemeji alikua ni mtu wa karibu sana na mumewe kama kaka mkubwa na ndiye alitumika kuwapatanisha baada ya mumewe kukiri kuwa na mchepuko na kuuzalisha watoto mapacha miaka michache tu baada ya wao kuoana. Mke aliwapokea hao watoto, wakakubaliana kutowaambia watu kwamba si wanae na akawalea kama watoto wake wa kwanza. Baadaye na wao wakajaliwa watoto watatu (ikijumuisha huyo wa mwisho ambaye kibaiolojia si wake)
Siku mbili baada ya kutoa hiyo siri, mke alifariki. Imepita miezi 3 sasa ila ndugu yetu anashindwa kuachilia na kusamehe, amejawa na hasira na uchungu na amekua mtu wa pombe na ulevi kupitiliza.
Mtoto wao wa mwisho ambaye ana miaka 7, ndiye mtoto aliyekua karibu naye sana kama baba, ni mtoto wao pekee wa kike na mtoto ambaye wamekua wanaishi naye nyumbani kwa sababu watoto wengine ni wakubwa na wako mashuleni.
Tatizo jingine ni kwamba; sasa kila akimuangalia mtoto anajisikia chuki na hasira ya kusalitiwa na ameanza kupoteza upendo kwa mtoto. Ni kama mwezi hivi umepita tangu ajihakikishie kwa DNA kwamba yule si mtoto wake wa kumzaa ila hana cha kufanya wala pa kumpeleka kwa sababu mkewe na rafiki yake ambao ndiyo wazazi wa mtoto wote wameshafariki na hawana ndugu wa kueleweka ambao anaweza kwenda kumuacha mtoto kwao.
Mshaurini, atapitaje pitaje hapa? kama kuna ushauri mzuri nitascreenshot nimfikishie.
Shukrani!
Anaweza asiolewwe ila akawa anachakatwa vizuri tu.Usifanye niache wosia Nikifa MkeWangu Asiolewe 🤪
Vijana wanataka kuteleza, vilainishi vinawasaidia 😂Tena vijana wenyewe ni wa hovyo na matumizi yao ya mafuta 🙌
Asante kwa ushauri wenye busara, nimeupokea na nitaufikisha.Siyo kawaida yangu kuandika kutokana na kuwa bize na moderation
Hili suala linagusa sana. Ningekuwa mimi, ningepiga moyo konde na kuendelea kumpokea mtoto huyo kama mwanangu. Hata iweje sitothubutu hata kuwajulisha ndugu wa pande zote. Inakuwa siri baina yangu na marehemu.
Kwa ajili ya afya ya moyo, ajitahidi kusahau na kuongeza huruma na upendo kwa mtoto. Jaribu huwa halina miadi
Thanks and over.
Mimi ushauri wangu kwa mtoto tu hapo, masuala ya kunywa pombe kupitiliza sitaki kuyagusia kabisa.Mke wa ndugu yetu amefariki baada ya kuumwa kansa kwa muda mrefu, kabla hajafariki amefichua siri kwa mumewe kwamba mtoto wao wa mwisho si mwanae bali ni mtoto wa shemeji (rafiki wa mumewe) ambaye alishafariki kwa ajali miaka 5 iliyopita.
Kabla ya usaliti, huyo shemeji alikua ni mtu wa karibu sana na mumewe kama kaka mkubwa na ndiye alitumika kuwapatanisha baada ya mumewe kukiri kuwa na mchepuko na kuuzalisha watoto mapacha miaka michache tu baada ya wao kuoana. Mke aliwapokea hao watoto, wakakubaliana kutowaambia watu kwamba si wanae na akawalea kama watoto wake wa kwanza. Baadaye na wao wakajaliwa watoto watatu (ikijumuisha huyo wa mwisho ambaye kibaiolojia si wake)
Siku mbili baada ya kutoa hiyo siri, mke alifariki. Imepita miezi 3 sasa ila ndugu yetu anashindwa kuachilia na kusamehe, amejawa na hasira na uchungu na amekua mtu wa pombe na ulevi kupitiliza.
Mtoto wao wa mwisho ambaye ana miaka 7, ndiye mtoto aliyekua karibu naye sana kama baba, ni mtoto wao pekee wa kike na mtoto ambaye wamekua wanaishi naye nyumbani kwa sababu watoto wengine ni wakubwa na wako mashuleni.
Tatizo jingine ni kwamba; sasa kila akimuangalia mtoto anajisikia chuki na hasira ya kusalitiwa na ameanza kupoteza upendo kwa mtoto. Ni kama mwezi hivi umepita tangu ajihakikishie kwa DNA kwamba yule si mtoto wake wa kumzaa ila hana cha kufanya wala pa kumpeleka kwa sababu mkewe na rafiki yake ambao ndiyo wazazi wa mtoto wote wameshafariki na hawana ndugu wa kueleweka ambao anaweza kwenda kumuacha mtoto kwao.
Mshaurini, atapitaje pitaje hapa? kama kuna ushauri mzuri nitascreenshot nimfikishie.
Shukrani!
Ndugu yako hatakiwi kumkataa wala kumnyanyasa huyo mtoto, wakati ametokea baada ya yeye kufanya mwanzoni tena mapacha.Haya toa comment yako sasa wewe shombeshombe, labda ni kweli hujarithi unafiki kutoka kwenye ngozi nyeusi.
TrueKwa vile msaliti (Marehemu mkewe) amesha fariki,basi amlee tu huyo mtoto ambaye hana makosa,
Kama yeye alisamehewa na mkewe kwa kuzaa nje ya ndoa huku akiwa ndani ya ndoa,halafu mkewe akakubali kuwalea hao watoto,basi na yeye amlee huyo mtoto wa marehemu mkewe coz hata Baba wa huyo mtoto alisha fariki pia,
Huyo jamaa nae ni msaliti pia,kupunguza hasira zake akumbuke kua hata yeye alimsaliti mkewe,
Nina wasiwasi na hiyo issue ya DNA,aliipimia wapi? Mahakama gani ilimpa ruhusa ya kufanya hiyo DNA? coz DNA ina taratibu zake,sio kama kwenda kupima Malaria tu.,
Labda swali langu niwaulize tu wana jamii,Je marehemu alikua sahihi kutoa hiyo siri kua huyo mtoto hakua mtoto wa mumewe?
Kwanza kabisa tuanze na yeye mwenyewe..Mke wa ndugu yetu amefariki baada ya kuumwa kansa kwa muda mrefu, kabla hajafariki amefichua siri kwa mumewe kwamba mtoto wao wa mwisho si mwanae bali ni mtoto wa shemeji (rafiki wa mumewe) ambaye alishafariki kwa ajali miaka 5 iliyopita.
Kabla ya usaliti, huyo shemeji alikua ni mtu wa karibu sana na mumewe kama kaka mkubwa na ndiye alitumika kuwapatanisha baada ya mumewe kukiri kuwa na mchepuko na kuuzalisha watoto mapacha miaka michache tu baada ya wao kuoana. Mke aliwapokea hao watoto, wakakubaliana kutowaambia watu kwamba si wanae na akawalea kama watoto wake wa kwanza. Baadaye na wao wakajaliwa watoto watatu (ikijumuisha huyo wa mwisho ambaye kibaiolojia si wake)
Siku mbili baada ya kutoa hiyo siri, mke alifariki. Imepita miezi 3 sasa ila ndugu yetu anashindwa kuachilia na kusamehe, amejawa na hasira na uchungu na amekua mtu wa pombe na ulevi kupitiliza.
Mtoto wao wa mwisho ambaye ana miaka 7, ndiye mtoto aliyekua karibu naye sana kama baba, ni mtoto wao pekee wa kike na mtoto ambaye wamekua wanaishi naye nyumbani kwa sababu watoto wengine ni wakubwa na wako mashuleni.
Tatizo jingine ni kwamba; sasa kila akimuangalia mtoto anajisikia chuki na hasira ya kusalitiwa na ameanza kupoteza upendo kwa mtoto. Ni kama mwezi hivi umepita tangu ajihakikishie kwa DNA kwamba yule si mtoto wake wa kumzaa ila hana cha kufanya wala pa kumpeleka kwa sababu mkewe na rafiki yake ambao ndiyo wazazi wa mtoto wote wameshafariki na hawana ndugu wa kueleweka ambao anaweza kwenda kumuacha mtoto kwao.
Mshaurini, atapitaje pitaje hapa? kama kuna ushauri mzuri nitascreenshot nimfikishie.
Shukrani!
Ningelikuwa mimi ningetumia huyo mtoto ku rasimisha unconditional love. She's an angel hana kosa lolote wenye makosa wameshatangulia mbele za haki.Wanaume tunapenda kusaliti, lakini sio wake zetu wasaliti
Mimi huwa nachukia hata mchepuko wangu akinisaliti (imagine), tunaweza tukaachana kabisa yaani
Mwambie atumie busara zetu Wazee wa mwaka 47 "Kitanda hakizai haramu"
Yeye alileta mapacha, mke kaleta mmoja
Watoto ni baraka, ampokee na kumlea kama mwanaye wa damu