Dilemma: Mke alikiri mtoto wa mwisho si wa mume na kisha akafariki. Mshaurini mume afanyaje baada ya huu usaliti

Kugongewa sijawahi thibitisha mzee,
Basi usiombe mzee Mimi nilipokuwa chuo nilikuwa nakaa na mwanangu yule mwanangu alipojua brother alietutangulia darasa amegonga manzi yake mbaka alipata disco mzee.
Na kamasi tulikuwa tunafuta.
Binafsi sijui kama nishagongewa ila naomba nisijue na mungu asinipe Hilo jaribu kabisa kwenye maisha yangu.
 
Kuna siri ni za kwenda nazo kaburini. Ona sasa ujinga wao now mtoto anateseka.
Msaliti akisalitiwa inauma kumbe🤣🤣
Atulie tu amlee mtoto wao, kitanda hakizai haramu.
 
Kimsingi mtoto hana makosa na kwa vile mamake na babake halali wamekwishafariki na mtoto hajui kabisa hiyo siri.Nashauri huyo ndugu yako asimwadhibu amchukulie kama mtoto yatima amemuasili.
 
Amlee tu kwa upendo kwakuwa wahalifu wote hawapo tena duniani na asimwabie mtoto juu ya DNA wala mtu mwingine ale buyu kama hajapima vile
 
Hii ndio maana halisi ya kwamba hata wanawake hawasamehi usaliti, wanakulia taimingi tu.
 
Wahenga wanasema kitanda hakizai haramu.

Kama tunaweza kulea watoto wa ndugu zetu why ushindwe kulea mtoto wa mke wako. Kama mke alimvumilia kulea wanae mapacha afanye hivyo kwa mtoto wa mke wake.

Chochote cha hasira atakachofanya ni kumharibia maisha mtoto na kumfanya yatima duniani hapa.

Afunike kombe mwanaharamu apite.

Na marehemu naye alishindwa kushikilia mpaka atoe siri au ndio wenge la kufa.....

All in all afanye kumtafuta mchepuko wake waliyezaa waishi maisha yaendelee. Au atafute pisi mpya iliyokomaa aendelee na maisha. Bila mwanamke atakuja kufa na mipombe.
 
Hebu nielezee mzee mwenzangu, huwa sielewi, kwanini mnakua hivi?
Wanaume kwa asili sisi ni watawala. Hulka yetu mwanamke ni wangu pekee yangu.

Kingine, wanaume huwa tuna tabia ya kuwaza mambo beyond horizon pindi tugunduapo tumesalitiwa. So, hii hututesa sana kisaikolojia.

Ila, mke kafariki, baba kafariki, jamaa apate mnasihi, alee huyo mtoto. Hakuna namna
 
Ampende kwa dhati,amlee na asimpe taarifa ya hizo habari. Wakosaji hawapo tena hivyo asimchukie asije akamdhuru huyo mtoto asiyekuwa na hatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…