Dili gani ulipiga likakutoa kimaisha na sisi wengine tujifunze

Dili gani ulipiga likakutoa kimaisha na sisi wengine tujifunze

Tulia nikupe Dili la jamaa mmoja askari mkoa Fulani hapa Tanzania.

Dili likuwa hivi, kuna Kijiji Fulani katika huo mkoa kuna wafugaji wa Ngo'mbe sasa siku moja kukawa kuna Ngo'mbe wengi sana wameibiwa nadhani mnafahamu jamii za wafugaji.

Zile Ngo'mbe ziliibiwa maana jamii za wafugaji Huwa wana hizi tabia za kuibiana, basi ikapigwa simu kituo cha polisi Kijiji Fulani kuna wizi ya mifugo mingi , basi mapoti wakatoka kama sita na difenda mpaka uhuuuuu mpaka hapo kwenye Icho kijiji.

Basi polisi wale ikabidi waanze msako maana jamaa aliyebiwa mifugo ni msukuma na ana Ngo'mbe mpaka anasahau, basi wale mapoti waliendelea kutafuta mpaka Giza linaingia kwenye wengi lazima wapo wanaopata tamaa ndio kilitokea.


Wengine wakasema turudini hapa hakuna dalili halafu ni porini vbaya, wakasema nyinyi nendeni basi katika watu sita wakabaki watatu wale wenzao walikuja kuchukuliwa na bodaboda wao wakabaki na difenda.

Tafuta sana usiku kabsa wakawaona hao wajamaa walikuwa wamanga'ti wakawakamata.

Baada ya kuwakamata kuwabana wakasema sisi tunatumwa na boss wetu wakasema twendeni mmoja akasema unaweza ukaongea na boss ukavutwa waya boss akapokea, jamaa akasema boss tumekamatwa.

Boss akajibu shida nn hapo maliza kesi hiyo, akasema hawataki akasema nipe simu boss akapokea akasema mnataka shngap mapoti wakaanza kupanic ww unataka kutuonga boss hakuongea sana akasema kuna milioni200 hapa nataka tumalize jambo hilo daah kusikia vile wakaangaliana wakasema hata tufanye mpaka tuzeeke hatuipati.

Basi deal done likafanyika pale, makubaliano Jinsi ya pesa zao kuzipata.baada ya kutoka kule wakapanga wakisema tukifika tutasema tumewakosa.
Walivyorudi wakasema hivyo.

Huyo jamaa hapo katika mkoa wake amejenga hostel za watoto wa chuo, ana mabiashara ya Huduma za fedha mjini hapo kila sehemu. kutoka katika ile milion200

Alifanya miaka 3 mbele baadae akasema sababu za afya akaacha kazi huku usimamizi akiwapa watu ili wasimtilie shaka,

Ajabu zaidi katika hao watatu peke yake ndio katoboa wengine zile pesa ziliisha kwenye vikojoleo vya wanawake na pombe
"Ajabu zaidi katika hao watatu peke yake ndio katoboa wengine zile pesa ziliisha kwenye vikojoleo vya wanawake na pombe"[emoji871]
 
Wakuu nimekua nikipambana bila mafanikio. Nimejaribu fursa mbalimbali lakini mambo bado bilabila.

Nimejaribu kufanya kilimo changamoto yake ipo kwenye umwangiliaji na soko, nimejaribu kutoa boda za mkataba lakini bado napigwa ngumi za pua.

Najua JF pana wengi na hapakosi kuwa na mengi ya kujifunza!

Hivi ulifanyaje fanyaje hadi ukatoboa? Ni vipi ulipatata financial freedom, dili gani ulipiga likakutoa kimaisha!
Gunia la Bangi mara mbili ya bei ya mahindi na Mchele...... Uza Bangi Kwa jumla
 
Nilianza kwenye machimbo ya madini ya dhahabu Lubumbashi sio powa wazee yaani full kunguni na kushinda njaaa maana congo vyakula vingi ni vya ajaaabu hadi ikapelekea kupata vidonda vya tumbo nilikuwa napiga zile mishe za kuwa apolo yaani unavaa zako tochi unaingia shimoni sasa Kuna siku tukaona mzigo mzito kule chini yaani full mawe yanang'aa sana aisee na Mimi si nikasema fursa hii hapa tulikuwa watu 6 tukachukuwa dhahabu zote maana ndo ilikuwa mara ya kwanza ule mgodi wa mkongoman kutoa dhahabu maana ulikuwa mpya tulivotoka yule bosi wetu alifurahi sana yaani siku hiyo sisi ndo tulipata dhahabu nyingi sana katika kugawana yule bosi aliiuza ile dhahabu bilioni 5 ila alivyagawa pesa aisee nilimuachia mungu maana alitupa Kila mtu milioni 50 ila sio mbaya maana nilitoka Tz kusaka pesa nikasema kuanzia Leo naacha hii kazi basi nikaanza kufungua mgahawa na sehemu ya kuonesha mpira pale Lubumbashi ilini ingizia sana pesa ila wale wenzangu walienda zao Paris France kuendelea kutafuta nikarudi zangu bongo na pesa kibao na nikarudi mererani kama bosi wa mgodi hapa nipo zangu home kigamboni na wife
 
Dili sahihi kwa muda sahihi na watu sahihi,

Sijawahi kupiga dili la maana ila mpaka nimefika hapa leo maranyingi nimekua nikilipwa na wema wangu pamoja na kujua kuishi na walio fanikiwa basi, Mfano niliwahi kumsaidia dogo zaidi ya miezi mitatu bila kuwaza nitafaidika na nini kutoka kwake, hatuna undugu wala nini, sikua na uwezo wa kumwajili ila nilimnunulia chakula daily cha mchana, nilimwekea order kwa mama ntilie akawa akifika anakula mi nakuta bill, dogo akataseka ila akaja kufanikiwa kupata kazi kwenye kampuni ya logistics moja af mwarabu akamwachia office yote sababu ya kumwamini, sikumoja naona call dogo kanichek akanipa habari zake af na mimi kipind hiko niko mwisho, akanambia atanisaidia kwenye biashara yangu kunitolea product kariakoo prus usafiri juu yake, then nitakua namrudishia tuu ya mtaji akanipiga taff sana nikapona nikarudi kwenye ramani, mpaka leo dogo ndo boss wangu namuheshimu sana na yeye ananiheshimu sana na maisha yanaenda. Ninashuhuda kibao za kulipwa na wema wangu ila chukua huo.
 
Back
Top Bottom