FaizaFoxy
DADA FAIZA NAOMBA UNIJIBU HAYA MASWALI ILI NISLIM.
Nianze kusoma shahada.
Muhammad Alitumwa kwa Waarabu Pekee yao.
Ndugu zetu Waislamu wanapenda sana kudai kuwa Yesu alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao na sio kwa ajili ya ulimwengu wote. Na andiko wanalolitumia tena na tena ni la Mathayo 15:24 pale Yesu alipozungumza na mwanamke Mkananayo: Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Nitakwambia kwa niniYesu alisema hivyo.
Kwa sasa tuangalie sababu 10 ambazo Allah mwenyewe anazitoa kuthibitisha kwamba alimtuma Muhammad kwa Waarabu na si kwa wasio Waarab.
Kwa mujibu wa Quran, Muhammad ni mtume wa Waarabu Majahila peke yao kwa sababu zifuatazo:
SABABU YA KWANZA Surat Yunus 10:47 Na kila umma una Mtume. Alipowajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “kila umma" si maana yake kila aina ya watu? Iwe ni Wazungu, Wahindi, Waafrika, nk?
2. Je, “Mtume wao” maana yake nini kama si wa kwao peke yao?
3. Je, Muhammad si ni Mwarabu ?
SABABU YA PILI
Surat Ibrahim 14:4 Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia.
Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “kwa ulimi” si maana yake kila mtume kwa lugha anayoongea?
2. Je, “wa kaumu yake” si maana yake ‘wa watu wake’; kama ni Mhindi kwa Wahindi?
3. Je, ulimi wa Muhammad si ni Kiarabu na kaumu yake ni Waarabu?
SABABU YA TATU
Suurat an Nah'l 16:36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.
Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “kila umma" si maana yake kila aina ya watu, mfano Wahindi na Waafrika?
2. Je, “tuliutumia Mtume” si maana yake mtume wa Wahindi si mtume wa Waafrika?
3. Je, Muhammad si ni Mwarabu?
SABABU YA NNE
Surat Al Maida 5:48 Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.
Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni.
Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake” si maana yake kila watu (Wazungu, Waafrika, nk) wamewekewa sharia zao wenyewe?
2. Je, Allah anaposema, “Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka angekufanyeni nyote umma mmoja” si anamaanisha kuwa angetaka tuwe na mtume mmoja na imani moja angetufanya taifa moja? Angalizo: “Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja”, inasomeka hivi kwa Kiingereza katika Sahih International:
“To each of you We prescribed a law and a method. Had Allah willed, He would have made you one nation [united in religion]” Katika tafsiri ya Yusufu Ali, inasema hivi:
“To each among you have we prescribed a law and an open way. If Allah had so willed, He would have made you a single people”
SABABU YA TANO
Surat Assajdah 32:2-‐3 Huu ni mteremsho wa Kitabu kisichokuwa na shaka yoyote kinachotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Au wanasema: Amekizua? Bali hichi ni Kweli iliyotoka kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka.
Tujiulize: 1. Kama kila umma Allah anadai aliupelekea mtume, je, “ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako” si maana yake anasema kuwa, ‘kwa vile Waarabu nilikuwa sijawaletea, wewe Muhammad ndio uende sasa’?
2. Je, kwa kuwa Muhammad si wa ule umma ambao tayari ulishaonywa, umma wake si unajulikana (Waarabu Majahila)? Maelezo tunayoyapata kwa Sayyid Abul Ala Maududi – Tafhim al-‐Qur'an -‐ The Meaning of the Qur'an (
32. Surah As Sajdah (The Prostration) - Sayyid Abul Ala Maududi - Tafhim al-Qur'an - The Meaning of the Qur'an) wazi:
yanasema The main theme of the Surah is to remove the doubts of the people concerning Tauhid, the Hereafter and the Prophethood, and to invite them to all these three realities.
The disbelievers of Makkah, when they talked of the Holy Prophet in private, said to one another, "This person is forging strange things sometimes he gives news of what will happen after death. Yaani, kwa kifupi, watu wa Makkah ambao hawakumuamini Muhammad ndio walikuwa wakimwambia kuwa anatungatunga tu uongo na kuwaambia ni Mungu kasema.
SABABU YA SITA
Surat Ya-‐Sin 36:2-‐6 Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima! Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa, Juu ya Njia Iliyonyooka. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.
Tujiulize:
1. Allah anapomwambia Muhammad, “wewe ni miongoni mwa waliotumwa”, maana yake ni nini kama si ileile kwamba Allah alituma mitume mbalimbali – kila watu na mtume wao – na huyu Muhammad ni mmoja wa waliotumwa?
Je, “Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa” maana yake si ni hao ambao ndio kaumu’ ya Muhammad? (Rejea sababu yatano hapo juu). SABABU YA SABA Surat Al -‐ An-‐A'am 6: 156-‐ 157 Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyokuwa wakiyasoma. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungelikuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo?
Tujiulize: 1. 2. 3. 4. Je, si kweli kwamba Allah anaongea na taifa Fulani hapa? Je, si kweli kwamba Allah anaonyesha kuwa kuna mataifa mawili (mengine) ambayo aliyateremshia vitabu vyao?
Je, si kweli kwamba Allah analiambia taifa hili analoongea nalo kuwa na wao amewaletea kitabu ili wasije kutoa visingizio kuwa hawakujua?
Je, Muhammad taifa lake si linajulikana?
SABABU YA NANE
Surat Ash-‐Shua'raa 26: 192-‐199 Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Ameuteremsha Roho muaminifu, Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji, kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi. Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale.
Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili? Na lau kuwa tungeliiteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, Na akawasomea, wasingelikuwa wenye kuamini.
Tujiulize:
1. Je, ulimi wa Kiarabu (lugha ya Kiarabu) iko wazi kwa mimi niliye Msukuma au Mnyakyusa au Mkikuyu?
2. Je, Allah anaposema, “Na lau kuwa tungeliiteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,” kuna asiyeelewa maana yake? -‐-‐-‐ kumbe unataka aseme wazi kiasi gani ndipo uelewe? – Basi maana yake ni kuwa kwa asiyekuwa Mwarabu Quran haimhusu!!
SABABU YA TISA
Surat Al -‐ An-‐A'am 6:92 Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Tujiulize: 1. Je, Allah anaposema “Mama wa Miji” si maana yake Makkah?
2. Je, “uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake” maana yake si ni kuwa Quran ni kwa ajili ya wakazi wa Makka na walio karibu na mji huo? Labda utasema kwamba “pembezoni” maana yake hata Marekani na Tanzania ni pembezoni. Basi soma sababu ya kumi ndio utajua ukomo wake.
SABABU YA KUMI
Surat Ash-‐Shuura 42:7 Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na walio pembezoni mwake.
Tujiulize:
1. Je, kwa kuwa tumeona kuwa “Mama wa Miji” ni Makkah, pembezoni mwake nako ni wapi?
2. Je, Allah anasema “tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu”, je, maana yake si kuwa, ni hadi pale Kiarabu kilikokuwa kinazungumzwa?
3. Je, kama alimaanisha hadi mwisho wa ulimwengu, angetaja kigezo cha lugha?
Hitimisho
Kwa mujibu w Allah, ni wazi kabisa kuwa, Quran haikuletwa kwa ajili ya kila mwanadamu bali kwa ajili ya Waarab peke yao. Muhammad si mtume wa kila mwanadamu bali ni mtume wa Waarabu peke yao.