Labda utakuwa huwajui vizuri waarabu mkuu,ukiniambia wazungu sawa nitakubali ila sio waarabu.Huwezi amini... waarabu hata hawakomai na uislaam kama waAfrica wafanyavyo...
Vatican hata hawakomai na Ukristo kama waAfrica wanavyofanya...
Mlokole wa nchi sizo za Africa na mlokole waAfrica wanaendesha mambo yao ya kiroho tafauti sana... waAfrica ni ugoko kwa ugoko...
Cc: mahondaw
PumbaaaaYou are not a right person to discuss this with me, I have a degree in theology, did it in LA Carlifonia
Degree yake humu haimsadii chochote namkubusha tu kua hili sio jukwaa la elimu au mashindano ya CV, zaidi kajionesha upande wake wa ujinga ambao umeturahisishia kumpuuza labda pengine ingetuchukua muda kugundua endapo asinge andika huo utopoloMkuu unanishangaza ulishasema mimi sio mtu sahihi kudiscuss na wewe sababu una degree in theology ambayo umeipata carlifonia.
Kitu ambacho sijakuuliza wala hakina mantiki kwenye hii mada hivyo umetoka nje ya mada.
Hiki kitu ni dalili ya uoga au inferiority mindset ambapo unaogopa kujihisi inferior ila ukweli wewe ni muoga hivyo unatumia degree kama defense mechanisms ambayo asilimia kubwa ya africans wanayo.
Mkuu Kwa ulichoandika basi elimu yako imekusaidia kupata pesa na ajira na si kingine ukiondoa dharau na majisifu ambayo ndani yake kuna mizizi ya ufahamu duni.
Sorry kwa maneno makali.
Sasa kwanini unaendelea kuniquote mkuu?
Au huna uhakika na kauli zako?
Kama huna uhakika na kauli zako
sasa una uhakika gani wa kusema mimi siwezi kudiscuss na wewe badala yake wewe ndo sio mtu sahihi kudiscuss na mimi?
Pumbaaaa
Mpaka hapa hujaelewa nilichoandika na umekiri hilo.Nimeshindwa kuelewa tatizo lako ni dini kumuathiri muafrika au ni dini zilizoletwa (uislam na ukristo) Tanzania ni nchi huru unaruhusiwa kuacha dini yako ulio nayo na kuwa chochote unachotaka.
Umesema hujanielewa lakini bado unaendelea kuargue.Ukitaka kuwa na dini hata ya kichina unaruhusiwa.Tatizo ni pale unapotumia akili ndogo Sana kutaka na wengine wakufuate Ilhali Kila mtu Yuko huru.
Waafrika wasiofuata ukristo ama uislamu ni wengi tu na sijaona tofauti yao.Ningetegemea niwaone wakiwa na Kila kitu na wakiwa na nafasi maeneo ya kipaumbele.
Hii inaprove kwamba dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika.(take out your head from your butt)
Wewe unayekijua kiweke hapa unachokijua then tujue nani ametumia facts na nani ametumia personal perspective.Kilichomsababisha mwafrika asiendelee hukijui na hutakijua
Umeenda nje ya mada probably sababu hujanielewa.Niliwahi kusema hata wazungu walikuwa na dini za asili lakini ukristo ulipowafikia waliacha dini zao za kiasili na wakaufuata ukristo.Maana ukristo umeanzia Israel na ukaenezwa dunia nzima.Lakini kumekuja kizazi Sasa Cha wazungu hawautaki ukristo na si ajabu wakarudi kwenye asili.
Bila Shaka ndio wanataka uhuru wa kijinsia na kuamua watakavyo bila kuwepo kipingamizi.
Na wanataka ukristo uondolewe Kila mahali.Haishangazi kuona marekani wanadai eti Kuna jinsia ya tatu.Kwa hio shuleni kuwe na vyoo vya jinsia tatu,,au sivyo jinsia ya kike na hio ya tatu zitumie choo kimoja.
Lakini kikwazo kikubwa kwao kikawa biblia na imani ya kikristo hivyo hutumia mbinu zote waichafue.ili waweze kuleta kitu wanachokitaka.
Wako huru Kama ma puppet wao huku Africa walivyo huru..ila wasitake Kila mtu achague njia yao.
Nimewahi kuandika thread kama hii kuhusu hili,Straight to the topic.
Africans wengi wanaamini kwenye dini kuliko chochote kile hapa duniani.
Na watu wanaomini kwenye dini wanaamini wapo hapa duniani ili kumuabudu mungu tu na si kingine.
Well hapa kwetu africa kuna dini kubwa mbili yaani uislamu na ukristo.
Na kwenye hizo dini kubwa mbili kila mtu anajiona yuko sahihi na kitabu chake ni sahii na dini ndio sahihi.
Na dini nyingine zaidi ya kwake ni ya uongo wala si ya kweli.
Cha ajabu hizi dini sio za africa bali zinatoka nje ya africa. Unaona akili ya mwafrika ilivyo hapo?
Na cha kushangaza zaidi hizi dini kwa karibu asilimia 90% zinatoka kwa wakoloni walioivamia africa.
Na sio wakoloni tu waliotukandamiza watu weusi, hapana hata hizo dini zimekandamiza watu weusi.
Na bila shaka hizo dini zilikuwa na mipango ya muda mrefu kuanzia miaka 100 mbele ili zifanikiwe na kweli zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Kumbuka ukitaka kumteka mtu kwenye kila kitu basi anza kumteka ufahamu wake.
Dini za wakoloni ndio chanzo mojawapo leo tuko hapa.
**********
Binadamu unatakiwa uwe na uwezo wa kujitambua na kujielewa ili kuepuka kuendeshwa na hisia ila ukishindwa kujitambua na kujielewa basi tegemea uwe controlled na hisia na hiyo ni sign ya ukosefu wa hivyo vitu hapo juu na vingine vya ziada yaani
=Kujitambua
=Kujielewa
Unajua kuna vitu vya kuchagua na kuvifanya au kuvitenda na kuna vitu vya kuacha. Hayo yote yanategemea na ufahamu wako.
Sasa huyu muafrika kwa yote yale aliyofanyiwa kuteswa, kudhihakiwa, kudharirishwa na mengine mengi mabaya.
Still mwafrika huyu alikubali kupokea dini hizi za mkoloni na kukubali kuwa ndio ufahamu wake na kila kitu kwenye hiyo dini kipo sahihi na hatoruhusiwa kupinga au kuhoji chochote juu ya hiyo dini au atalaaniwa.
Mwafrika huyu mweusi amekubali kupokea dini ambayo.
=Amepewa na watu weupe waliomfanyia kila aina ya ubaya na ukatili.
=Kila mtume kwenye hizo dini ni mweupe
=Hata mungu wa kwenye hizo dini katuma watu weupe waje kutangaza hizo dini weusi sijui kwanini kawaacha
=Alikubali kupokea dini ambazo mtu mweusi ni nembo ya shetani na nyeupe ni nuru ya malaika.
(Huo ni ubaguzi pure)
=Dini ambazo inasema mweusi amelaaniwa nk
Hapohapo Yaani mwafrika yupo tayari
=Akuue
=Akutukane
=Akudharirishe
=Akudharau
=Akupige
=Akudhihaki au chochote kile kibaya mwafrika atamfanyia mwafrika mwenzake sababu ya dini aliyopewa na mtu aliyemtesa, kumtukana, kumdhihaki na kumdharirisha.
Still mwafrika mweusi huyohuyo anaamini yeye amelaaniwa kwa rangi yake na yeye si chochote mbele ya mweupe kwani mweupe amebarikiwa.
Hapo hakumbuki kama hiyo dini kampa huyohuyo mweupe aliyemtesa na kumpiga mijeredi ya mgongo ili asiangushe pembe za tembo.
Yes huyo ndio mwafrika wa africa usijali hata humu watajitokeza watu kama hao. Asilimia kadhaa za hao watu wapo humu jf.
Na hapo mwafrika huyo bado ataendelea kumchukia mwafrika wa dini nyingine kivyovyote vile.
*******
Labda mababu zetu walikosa hivyo vitu yaani kujielewa na kujitambua hivyo wakawa wanaendeshwa na hisia bila wao kujua hivyo ikawafanya wasie na akili wala maarifa ya kueleweka.
Lakini binadamu anabadirika kadri muda unavyozidi kwenda
Hivyo hata sisi tunaweza kubadirika na kuanza kujitambua na kujielewa na sio kuendeshwa na hisia tena au Africans itakuwa ngumu kubadirika.
kila kitu kimerahisishwa na hao wazungu ambavyo si vya kupotosha na kukandamiza kama dini hivyo tunaweza kutumia hivyo vitu vizuri kuweza kubadirika na kujiongeza na sio kuendelea kubomoka.
Kumbuka nilikwambia binadamu anatakiwa awe na sifa ya kujitambua na kujielewa ili aisendeshwa na hisia au imani hivyo ni lazima kujua kipi cha kuchukua na kuacha na sio kupelekeshwa kama fuso bovu na hizo hisia kama mababu zetu waliokubali hizi imani.
*******
SASA HII IMEATHIRI VIPI UFAHAMU AU UBONGO WA MWAFRIKA.
=Well baada ya hapo mwafrika akawa muoga wa kuhoji "kwanini. sababu ya kuogopa kukufuru na kulaaniwa alafu alishaalaniwa mara kwanza.
=Mwafrika akawa mvivu wa kufikiri kwa kusema kila kitu anapanga mungu hivyo huyo mwafrika kubweteka chini akitegemea mungu atamfanya apate anachokitaka huku amekaa tu chini ya mwembe. Hadi leo hawa watu wapo na ndio masikini wa kwanza yaani mafukara.
=mwafrika huyu anaamini wazungu ndio wamebarikiwa na ndio maana wameendelea.
=mwafrika ubongo wake wote umelala sababu ameaminishwa yeye si chochote kwani amelaaniwa na ndo maana rangi yake nyeusi.
=mwafrika anaamini duniani anapita tu na yupo hapa kumuabudu mungu tu.
Hivyo huyo mwafrika kuendelea kufa masikini na kuendelea kuishi na changamoto sababu yeye kaja kumuabudu mungu tu na kuijaza dunia na si kingine wakati huo weupe wakiendelea kukua kila siku.
=Mwafrika anaogopa kutumia na kutegemea ufahamu wake sababu dini imemwambia asitumie ufahamu wake sababu mungu yupo.
Na anashindwa kujiuliza vitu vyote anavyotumia vimetokana na ufahamu.
=Na watu kugombana sababu ya dini iliyoletwa na weupe hata huyo mweupe akiona anaweza shangaa akili zao zilivyo za ajabu hao Africans wakimpigania mtume mweupe wa kwenye kitabu.
Na mpaka leo africa hatuna kitu ambacho kimetokana na sisi wenyewe, labda kama wangetuacha kipindi kike labda tungechelewa lakini tungepata ufahamu taratibu kuliko kutuharibu kabisa na hizi dini.
Mbona china wana dini zao lakini wana maendeleo makubwa sana na ni wamoja tena wana ufahamu mkubwa ukilinganisha na sisi.
Africans hatuna umoja wala ushirikiano sababu tunachukiana na kubaguana kidini kwa dini ambazo zililetwa na watu kutoka nje kitu ambacho ni ujinga.
Najua wengi mmerukia mwisho sababu ndio tabia zenu za kutokupenda kushughulisha vichwa vyenu.
Sasa nakuambia popote utakapomtukana mtu yoyote sababu ya tofauti za kidini basi tambua hiyo dini si asili yako bali ulipewa na mweupe ili apate kukuendesha na kukucontroll so think again.
Nadhani baada ya hapo tutaacha kutukanana, kudhihakiana, kudharauriana, kubaguana sababu ya dini na hapo ndio mwanzo wa kujitambua.
na wote kuwa kitu kimoja kitu ambacho hakiwezekani.
Umeenda nje ya mada probably sababu hujanielewa.
Hata mimi nashangaa haya mambo yanawezekana vp? Lakini pia mfano mzuri ni kutawaliwa kwa prof K'budi na pole pole, hawa jamaa ukiwaangalia kabla na baada ya uteuzi utagundua kwa sasa ni koloni la mtu fulani hapa mjini-Hawa wazungu sijui walifanikiwaje kwenye hili mbona kule China & India walitawaliwa na wazungu lakini bado walibaki na dini zao
Kwanza niulize hapo.... Kristi ni nani.!?... Na Nani alimpa Hilo jina na imani ya kikristo maana yake tunamuabudu kristo si ndo maan yake ... Fafanua hapoTafadhali naomba urekebishe mada yako, ukristo sio dini. Kwaza kabisa kristo ni Mungu mtu. Ukristo ni Imani ya kuamini katika kristo. Dini ni mfumo, taratibu, sheria na kanuni anuai zinazoendesha imani ya kikristo
Soma uelewe makala yake nzima.... Ndo uulize ... Hzi dini zimetudumaza kweli waafrika ... Minmpka Leo sijajua kwann Mungu akutuletea mtume hata mmoja wa kiafrica...Hivi mtu akiamini Mungu imani hii ndio itamfanya asiweze kutengeza gari ?
Ama kuna dini inayomkataza Mtu asitengeneze gari ?
Ama asitengeneze na kuvumbua teknolojia ?