tafsiri yangu kuhusu akili ni kuwa, Akili ni Ufahamu au kipawa kinachomuwezesha mtu kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kupanga/kupangua, kujifunza na namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili mtu kulingana na mazingira aliyomo.
Nimesema wazungu na waarabu walituzidi akili kwa kuwa kabla ya kufika Africa wao wenyewe walikuwa wameshapata changamoto nyingi za kimazingira, kiutawala na kimkakati ikiwemo vita nyingi walizopigana baina yao katika kugombea ardhi na kutanua himaya zao, hivyo basi changamoto hizo ziliwafanya kukuwa kiakili kwa kutafuta maarifa sehemu mbalimbali na kuwa wabunifu, kwa ubunifu wao waliweza kugundua namna bora za utawala na udhibiti. Hali hiyo huku Africa ilikuwa haijafikiwa japo vita miongoni mwa watawala vilikuwepo lakini ubunifu haukuwa mkubwa.
Hivyo wao walipofika huku walikuta sisi bado tupo chini kiakili hivyo ilikuwa rahisi kwao kutushika na kututawala wanavyotaka, ndiyo maana utaona hata tunajivunia kutumia majina yao kwa kuwa walitudanganya eti ni majina ya dini (kitu ambacho ni uongo). Wahindi wametawaliwa na Waingereza lakini ni nadra sana kukuta muhindi anatumia jina la Kiingereza. Hii ni kwa kuwa wanajielewa sana tofauti na sisi, Wachina walitawaliwa na Japan kwa muda mrefu lakini ni nadra kukuta mchina anatumia jina la Kijapani ni kwa kuwa wanajielewa na uwezo wao wa kufikiri na kuchambua ni mkubwa.