Straight to the topic.
Africans wengi wanaamini kwenye dini kuliko chochote kile hapa duniani.
Na watu wanaomini kwenye dini wanaamini wapo hapa duniani ili kumuabudu mungu tu na si kingine.
Well hapa kwetu africa kuna dini kubwa mbili yaani uislamu na ukristo.
Na kwenye hizo dini kubwa mbili kila mtu anajiona yuko sahihi na kitabu chake ni sahii na dini ndio sahihi.
Na dini nyingine zaidi ya kwake ni ya uongo wala si ya kweli.
Cha ajabu hizi dini sio za africa bali zinatoka nje ya africa. Unaona akili ya mwafrika ilivyo hapo?
Na cha kushangaza zaidi hizi dini kwa karibu asilimia 90% zinatoka kwa wakoloni walioivamia africa.
Na sio wakoloni tu waliotukandamiza watu weusi, hapana hata hizo dini zimekandamiza watu weusi.
Na bila shaka hizo dini zilikuwa na mipango ya muda mrefu kuanzia miaka 100 mbele ili zifanikiwe na kweli zimefanikiwa kwa kiwango kikubwa.
Kumbuka ukitaka kumteka mtu kwenye kila kitu basi anza kumteka ufahamu wake.
Dini za wakoloni ndio chanzo mojawapo leo tuko hapa.
**********
Binadamu unatakiwa uwe na uwezo wa kujitambua na kujielewa ili kuepuka kuendeshwa na hisia ila ukishindwa kujitambua na kujielewa basi tegemea uwe controlled na hisia na hiyo ni sign ya ukosefu wa hivyo vitu hapo juu na vingine vya ziada yaani
=Kujitambua
=Kujielewa
Unajua kuna vitu vya kuchagua na kuvifanya au kuvitenda na kuna vitu vya kuacha. Hayo yote yanategemea na ufahamu wako.
Sasa huyu muafrika kwa yote yale aliyofanyiwa kuteswa, kudhihakiwa, kudharirishwa na mengine mengi mabaya.
Still mwafrika huyu alikubali kupokea dini hizi za mkoloni na kukubali kuwa ndio ufahamu wake na kila kitu kwenye hiyo dini kipo sahihi na hatoruhusiwa kupinga au kuhoji chochote juu ya hiyo dini au atalaaniwa.
Mwafrika huyu mweusi amekubali kupokea dini ambayo.
=Amepewa na watu weupe waliomfanyia kila aina ya ubaya na ukatili.
=Kila mtume kwenye hizo dini ni mweupe
=Hata mungu wa kwenye hizo dini katuma watu weupe waje kutangaza hizo dini weusi sijui kwanini kawaacha
=Alikubali kupokea dini ambazo mtu mweusi ni nembo ya shetani na nyeupe ni nuru ya malaika.
(Huo ni ubaguzi pure)
=Dini ambazo inasema mweusi amelaaniwa nk
Hapohapo Yaani mwafrika yupo tayari
=Akuue
=Akutukane
=Akudharirishe
=Akudharau
=Akupige
=Akudhihaki au chochote kile kibaya mwafrika atamfanyia mwafrika mwenzake sababu ya dini aliyopewa na mtu aliyemtesa, kumtukana, kumdhihaki na kumdharirisha.
Still mwafrika mweusi huyohuyo anaamini yeye amelaaniwa kwa rangi yake na yeye si chochote mbele ya mweupe kwani mweupe amebarikiwa.
Hapo hakumbuki kama hiyo dini kampa huyohuyo mweupe aliyemtesa na kumpiga mijeredi ya mgongo ili asiangushe pembe za tembo.
Yes huyo ndio mwafrika wa africa usijali hata humu watajitokeza watu kama hao. Asilimia kadhaa za hao watu wapo humu jf.
Na hapo mwafrika huyo bado ataendelea kumchukia mwafrika wa dini nyingine kivyovyote vile.
*******
Labda mababu zetu walikosa hivyo vitu yaani kujielewa na kujitambua hivyo wakawa wanaendeshwa na hisia bila wao kujua hivyo ikawafanya wasie na akili wala maarifa ya kueleweka.
Lakini binadamu anabadirika kadri muda unavyozidi kwenda
Hivyo hata sisi tunaweza kubadirika na kuanza kujitambua na kujielewa na sio kuendeshwa na hisia tena au Africans itakuwa ngumu kubadirika.
kila kitu kimerahisishwa na hao wazungu ambavyo si vya kupotosha na kukandamiza kama dini hivyo tunaweza kutumia hivyo vitu vizuri kuweza kubadirika na kujiongeza na sio kuendelea kubomoka.
Kumbuka nilikwambia binadamu anatakiwa awe na sifa ya kujitambua na kujielewa ili aisendeshwa na hisia au imani hivyo ni lazima kujua kipi cha kuchukua na kuacha na sio kupelekeshwa kama fuso bovu na hizo hisia kama mababu zetu waliokubali hizi imani.
*******
SASA HII IMEATHIRI VIPI UFAHAMU AU UBONGO WA MWAFRIKA.
=Well baada ya hapo mwafrika akawa muoga wa kuhoji "kwanini. sababu ya kuogopa kukufuru na kulaaniwa alafu alishaalaniwa mara kwanza.
=Mwafrika akawa mvivu wa kufikiri kwa kusema kila kitu anapanga mungu hivyo huyo mwafrika kubweteka chini akitegemea mungu atamfanya apate anachokitaka huku amekaa tu chini ya mwembe. Hadi leo hawa watu wapo na ndio masikini wa kwanza yaani mafukara.
=mwafrika huyu anaamini wazungu ndio wamebarikiwa na ndio maana wameendelea.
=mwafrika ubongo wake wote umelala sababu ameaminishwa yeye si chochote kwani amelaaniwa na ndo maana rangi yake nyeusi.
=mwafrika anaamini duniani anapita tu na yupo hapa kumuabudu mungu tu.
Hivyo huyo mwafrika kuendelea kufa masikini na kuendelea kuishi na changamoto sababu yeye kaja kumuabudu mungu tu na kuijaza dunia na si kingine wakati huo weupe wakiendelea kukua kila siku.
=Mwafrika anaogopa kutumia na kutegemea ufahamu wake sababu dini imemwambia asitumie ufahamu wake sababu mungu yupo.
Na anashindwa kujiuliza vitu vyote anavyotumia vimetokana na ufahamu.
=Na watu kugombana sababu ya dini iliyoletwa na weupe hata huyo mweupe akiona anaweza shangaa akili zao zilivyo za ajabu hao Africans wakimpigania mtume mweupe wa kwenye kitabu.
Na mpaka leo africa hatuna kitu ambacho kimetokana na sisi wenyewe, labda kama wangetuacha kipindi kike labda tungechelewa lakini tungepata ufahamu taratibu kuliko kutuharibu kabisa na hizi dini.
Mbona china wana dini zao lakini wana maendeleo makubwa sana na ni wamoja tena wana ufahamu mkubwa ukilinganisha na sisi.
Africans hatuna umoja wala ushirikiano sababu tunachukiana na kubaguana kidini kwa dini ambazo zililetwa na watu kutoka nje kitu ambacho ni ujinga.
Najua wengi mmerukia mwisho sababu ndio tabia zenu za kutokupenda kushughulisha vichwa vyenu.
Sasa nakuambia popote utakapomtukana mtu yoyote sababu ya tofauti za kidini basi tambua hiyo dini si asili yako bali ulipewa na mweupe ili apate kukuendesha na kukucontroll so think again.
Nadhani baada ya hapo tutaacha kutukanana, kudhihakiana, kudharauriana, kubaguana sababu ya dini na hapo ndio mwanzo wa kujitambua.
na wote kuwa kitu kimoja kitu ambacho hakiwezekani.
Habari,
Binafsi nakushukuru kwa kuleta mada fikirishi kama hii, umeandika mambo mengi kwa kadiri ya uwezo wako wa kuchambua ulipofikia na kwangu mimi naona siyo jambo baya. Watu wengi hawajui hasa nini maana ya dini na nini lengo la dini miongoni mwetu sisi wanadamu ndiyo maana wengine wanapinga, wanalaumu na wengine wanaunga mkono lakini bado hawajatoa suluhu hasa ya nini matatizo yetu au dini imetusaidia nini. Binafsi nitajitahidi kadiri ya nilivyojaliwa kuelezea mawazo yangu machache.
Kwa kadri ninavyofahamu ni kuwa Dini ni njia ya Mwanadamu kumtafuta na kumuabudu
MUNGU (Tafsiri yangu), hivyo basi dini ni ya Mwanadamu maana
MUNGU hana dini kwa kuwa yeye anaabudiwa na haabudu kiumbe chochote. Mambo mengine mengi yaliyomo ndani ya vitabu vya dini (Biblia na Quran) ni sheria, mila na tamaduni zao (hao waleta dini) kwa jinsi walivyoishi zama zao hivyo kwetu sisi hazina uzito maana hata sisi tunazo. Kama Babu zetu wangekuwa na akili kubwa wangeweza kuhoji mathalani kuhusu majina maana tumeaminishwa kuwa majina ya kizungu ndiyo ya kikristo na majina ya kiarabu ni ya kiislamu wakati kiuhalisia siyo kweli maana majina yalikuwapo kabla ya dini hizo kuja na hakuna mtume yoyote aliyekuja na majina. Pia sisi Africa tuna majina yetu hivyo kama tukifikiri kwa kina tutagundua kuwa hatukua na haja ya kutumia majina yao.
Hao wazungu na waarabu tunaoshindana kuwalaumu kuwa walituletea dini hizi hata wao hawakuwa nazo hapo awali hivyo na wao waliletewa na wakati wakiletewa dini hizo za
Ukristo na Uislamu siyo kwamba wao hawakuwa na dini, zilikuwepo ila hazikuwa za kumuabudu
MUNGU wa kweli bali masanamu, jua, mwezi na wengine waliabudu nyota. (Hii ikiwa na maana kuwa walikuwa na
MIUNGU ila hawakuwa na
MUNGU wa kweli)
Kuhusu maendeleo na ustaarabu siyo kwamba vililetwa na dini bali dini hizi mbili zilikuta jamii za wakati huo zikiwa zimestaarabika maana tayari walikuwa na mavazi, walijenga majengo na walijua kuchimba visima vya maji pia walimiliki mali na walikuwa na mifumo ya utawala yenye kueleweka, hivyo ilichofanya dini ni
kunogesha ustaarabu huo kwa kuwafanya watu kumjua
MUNGU wa kweli, kupendana, kuheshimiana na pia kuelimika kwa kujifunza zaidi. Hivyo ukisema dini imeleta maangamizi Afrika utakuwa unakosea.
Kwangu mimi binafsi naona ni ujinga kumlaumu mzungu au muarabu kwa umaskini wetu, inafaa tukubali kuwa sisi tuna akili ndogo na wenzetu wana akili kubwa, bila hivyo hatuwezi kupiga hatua, tutaendelea kuwalaumu viongozi wetu huku tukijua wametokana na sisi hivyo na wao wana akili ndogo kama sisi. Kama ambavyo mgonjwa akienda kwa Daktari akaambiwa kuwa homa inayomsumbua ni malaria, inatakiwa mgonjwa huyo akubali kuwa ana malaria ndipo apewe doze lakini akikataa kuwa hana malaria hata akipewa dawa hawezi kuzimeza. Sasa kama sisi hatutakubaliana kuwa tuna akili ndogo basi kujifunza na kukosoana itakuwa vigumu hivyo tutaendelea kupiga marktime.
Matatizo tuliyonayo Waafrica yametokana na tabia ya uvivu, kutopenda elimu na kujidharau/kudharauliana sisi wenyewe kwa wenyewe (
KUJIENDEKEZA) na kisha kumtukuza Mzungu na Muarabu, yaani imefikia hatua kuwa Muafrika mbele ya mzungu au muarabu ni kama mmbwa mbele ya chatu.
Suluhisho ni kuwa, tukiacha kujiendekeza na kudharauliana na kisha tukachapa kazi kwa bidii na kuwa waaminifu miongoni mwetu, tutapiga hatua ya kimaendeleo na tutafika mbali, hata tusipowafikia wazungu au waarabu lakini angalau tutaweza kutatua matatizo yetu ya msingi kama vile ukosefu wa chakula bora (ardhi tunayo), elimu bora na uchumi endelevu. (Nina mengi ila nimechoka kuandika)