Dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika

Acha ku troll. Fanya research vizuri. Ukristu umeanzia ethiopia kabla hata wazungu hawajabadili story kwa manufaa yao.
 
Hebu muulize tu, babu wa babu yake alikuwa mkristo au Muisilamu???, kama hakuwa na moja kati ya hizo dini basi atuambie alikuwa na maendeleo gani mbali na kuwa mchawi na mshirikina katika zama hizo.
Wote hamjui mnachoongea. Hamjui kwann tulitawaliwa na hamjui the power of black african. Afu kwani tulitawaliwa sisi tu. Kwenye historia ya dunia kila race ilishawahi kutawaliwa. Sisi ndo tulikua race ya mwisho inayomalizikia katika utawala wa direct. Wachina walishawahi kutawaliwa lakini mbona hawajidharau kama nyie mnavojidharau kuhusu swala la kutawaliwa.
 
Hakuna aliye mzidi mtu akili. Its a matter of time and opportunity. Ujinga wako unaanzia pale unapoanza kusema una akili ndogo kuliko mwanaume mwenzako. Unajipeleka kwenye utumwa mwenyewe bila hata nguvu. Jiamini ili hata huyo mzungu akija kukuonea hutakua na mtazamo wa kipumbavu wa kumuogopa kwa kufikiri anakuzidi akili
 


Wewe si Genius ?!!, kwa kujiamini kwako umefanya kitu kipi cha kusaidia umma cha kukumbukwa??
 
Tatizo sie tunalalamika mambo ya kutawaliwa sijui tamaduni za kigeni utafikiri ni sie tu pekee ndio tuliotawaliwa au ndio sie pekee tunafuata tamaduni za watu wengine.
 
Unamwambia mwanamke tufunge ndoa ya serikali anakujibu "Yesu Maria na Yosefu, sitamkufuru Mungu " ni kudumaa kwa akili kutokana na hizi dini zilizosukwa na binadamu.

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Hawa wazungu sijui walifanikiwaje kwenye hili mbona kule China & India walitawaliwa na wazungu lakini bado walibaki na dini zao

Nilikuwa naenda kanisani, ila baada ya kustuka, sasa hivi nimewapotezea vibaya sana.
 
Kitendo cha kuacha mila zako na kufuata za kizungu ni "utumwa " uliokubuhu. Ni kudumaa kiakili! Haraka turudi kwenye matambiko yetu Waafrika. Zamani likipigwa tambiko la uhakika janga (njaa) inaondoka na mvua inanyesha. Sasa tumekufuru kwa kutokuzingatia matambiko.
 
Acheni kupotosha umma. Dini ina Mchango mkubwa Sana katika Maendeleo ya Dunia. Si Ulaya tu lakini hata Africa.
Shule za kwanza za Misheni ndio zimetuletea viongozi wapigania uhuru huku Africa.
Huduma Bora za jamii huku Africa mpaka leo ni zile zinazotolewa na Mashirika ya Dini..ikiwemo Afya na Elimu. n.k

Jibuni swali kivipi Dini inakufanya usivumbue vitu ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…