Dini zimechangia kudumaza ufahamu wa mwafrika

Mkuu bila shaka sidhani kama umesoma uzi wote.
Hivyo vyote nimeelezea dini ilivyoingia hapo.
 
Hayo nimeandika kwenye uzi na wewe uliniambia huwezi kusoma uzi wote.

Bahati mbaya Mimi sina muda wa kupoteza kuelezea vitu ambavto nimeshaelezea.

Soma uzi wote.
Uzi wako hata tuusome wote kumbuka lazima maswali yatakuwepo.

Okey Ila sio lazima kujibu
 
Mkuu bila shaka sidhani kama umesoma uzi wote.
Hivyo vyote nimeelezea dini ilivyoingia hapo.
Kijana pengine unaona umeelezea kwa maelezo yako lakini wasomaji hatujaona mahusiano hivyo tunataka maelezo ya ziada.

Usione kwamba mada yako iko kamilifu sana kiasi kwamba watu wasihoji yaliyo ndani ya mada ati kwa kuwa mada yako imegusa kila kitu kwa UNAVYOONA.

Ukianzisha mada unatakiwa uitetee.

Watu wanajafili kilichokuwa ndani ya mada yako yaani ulichoandika kwaaama wako ndani ya mada.

Wewe unasema ati yote umeeleza,basi kusiwepo na comment ati kwa maana hii.
 
na sio kwamba inatosha kwa mtu mmoja kuathiriwa na fikra za dini hiyo na kumdumaza endapo ataiamini ?
Nikikuambia wewe peke yako ukajenge daraja la kigamboni je ungeweza?
Kwa hiyo unataka kutuambia dini ili ilemaze na kumtia mtu ujinga basi lazima dini hiyo ipokelewe na watu wengi saaaaaana ?
Hapana.
 
Moja wapo ya kikwazo cha maendeleo ya waafirika ni kuwa na watu wenye mawazo ya kijinga kama ya kwako.
Kwahiyo ukiwa mkiristo au mwislam basi ndo kigezo cha kushindwa kufanya maendeleo au?
Kama ndio hivyo mbona Thairand ambayo asilimia 90 ni mabudha isizizidi maendeleo UAE,Qtaar,saudia, Uturuki, Malaysia,Indonesia,Iran,Burunei ambayo asilimia karibia 95 ya raia wake ni waislam?
Kama ndio hivyo mbona Mianimar ambayo aslimia 95 ya raia wake ni mabudha isizizidi maendeleo ,Marekani, Ujerumani,ufaransa,Italia ambazo zaidi ya asilimia 90 ya raia wake ni wakiristo?
Hao wahindi unao wasifia kuabudu dini zao za asili ndo kila siku wana kimbilia Ulaya na mashariki ya kati kutafuta kazi kwa hao wenye hizo dini ambazo una ziponda.
Hata hapa Tz asilimia kubwa ya wasukuma hasa wa vijijini hawaaini katika hizo dini je wamefanya maajabu gani ndani ya Tz?
Mkuu kabla hujaleta mada jaribu kuangaisha akili yako.
 
Nikikuambia wewe peke yako ukajenge daraja la kigamboni je ungeweza?
Unachanganya madawa kabisa hapa.
Daraja ni suala la kimaendeleo linalohitaji nguvu ya watu kadhaa ili likamilike.

Aje na dini inahitaji nguvu ya watu kadhaa kuikubali na kuiamini ili ndo iwe dini ni ujinga rasmi ?

Yaani haitoshi dini kuwa ujinga mpaka waiamini watu wengi sana ?
 
Kama shida yako ni dini, hakuna binadamu asiye na dini, ni swala la tafsiri tu, ...
Sasa dini hizo mbili ndio chanzo mojawapo kati ya vingi vilivyolemaza ufahamu africa.

Sidhani kama kuna special scientist yoyote kutoka africa anayefanya tafiti kubwa za kidunia kama wapo basi wachache sana.
 
Wanafikiri kutukana dini ndo suluhisho.
 
wasukuma wanaonesha dhaili the weakeness of African religion and traditional
 
Mtoa mada yeye mwenyewe anamini maandishi asiyoyaleta mwenyewe. Matusi yanayoelekezwa kwenye Dini na waumini wake hayafanani na mafanikio ya watu kimaisha hata China wapo maskini km walivyoa Africa
 
Kimsingi jamani dini inayo muhusisha mungu niyakuiga kutokana hajawahi kuwaacha watu pa baya " jaribu kujiangalia wewe binafsi kwamba ni dini gani inakuweka huru" then ndo utuambie mmoja kwa mmoja kuwa umejifunza mangapi kuliko kutopotosha.
 
Kimsingi jamani dini inayo muhusisha mungu niyakuiga kutokana hajawahi kuwaacha watu pa baya " jaribu kujiangalia wewe binafsi kwamba ni dini gani inakuweka huru" then ndo utuambie mmoja kwa mmoja kuwa umejifunza mangapi kuliko kutopotosha.
 
Mkuu nadhani mtoa mada angebase kwenye utabaka na ubaguzi na siyo maendeleo

Ali in all namuunga mkono
 
Fantastic, well said bro.
 
USILOLIJUA...NI SAWA NA USIKU WA KIZA

Nina hakika
Uislam huujui,na wala huna mpango wa kuujua
Kwasababu umemezeshwa maji yasiyofaa

FAHAMU DOGO
Uislam,unahimiza sana elimu,kujitambua,kushindana katika maendeleo

Huu ndio Uislam
Hakuna sehemu katika Uislam,inasema usisome Dunia yako na wala usiifikirie

Bali uhakika na uhalisia
UISLAM NI DINI YA ELIMU

Lakini wengi(mfano wako)hawajui

Jioni njema
 
Ahsante Sana, Ila Nina swali, wewe unayodini?
 
mkuu maswali unayouliza yote yapo kwenye mada, soma tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…