Dini zinamilikiwa na Wazungu au Waafrika?

Dini zinamilikiwa na Wazungu au Waafrika?

Kuna school of thought (mkondo wa uelewa) kwamba mojawapo ya madhara ya dini za kigeni ni mporomoko wa kimaadili ya asili ya Waafrika. Katika mkondo huo wa uelewa yafuatayo yanatajwa na asili yake:-

1. Ushoga ulitoka Ulaya.
2. Ubakaji ulitoka Ulaya.
3. Mlango wa KIA ulitoka Uarabuni.

NB. Waafrika waliishi bila nguo (nguo zililetwa na Mzungu) lakini hakukuwa na matukio kama haya au kama yalikuwepo basi ni kwa uchache sana ambacho hakitoshi kuhalalisha kuwa ni janga la dunia. Lakini hata hivyo leo watu wanaabudu kwa mfumo wa kigeni kwa kuvalia nguo zisizo na staha na kuibua mjadala mpya wa kimaadili.

Kwanini dini ihusike?

Kwa sababu Dini ndiyo ilitangulia ku-document mambo hayo kwenye Misahafu, Sheria za nchi dhidi ya maovu hayo hazikuwepo (zimetungwa hivi karibuni) na mila na desturi za asili hazikusisitiza dhidi ya maovu hayo kwa sababu ama hayakuwepo au yalikuwepo kwa uchache sana.

Aidha, nadhani adhabu kali haziwezi kumaliza kadhia hii, tunayo sheria kali ya ubakaji lakini bado Madawati ya Jinsia kwenye vituo vya Polisi yanapokea kesi nyingi sana. Watu wanachomwa moto wa matairi lakini bado. Kwenye Biblia kuliwa na kupigwa mawe hadi kufa, kufungwa jiwe la kusagia shingoni lakini bado akina Mfalme Daudi, Abimeleki walichepuka.
Sheria Kali ikitekelezwa ndugu yangu watu wanabadilika.

Daudi alichepuka mana alijua mfalme yupo juu ya Sheria. Ndio maana Mungu aliingilia kati na kumwadhibu mana hapakua na mtu wa kumwadhibu mfalme.

Wanawake wanakua bidhaa ya kujiuza na kutafuta kipato Kwa zinaa mana Kuna kitu kinaitwa haki sawa. Lakini hakuna shujaa mbele ya adhabu ya kufa.

Kuna mwamba alikaa madarakani miaka mitano TU nchi ikanyooka kwasababu ukikaidi unapitezwa fasta unaacha familia yako. Kila mtu akawa na hofu. Tatizo hata kesi za kubaka ni rushwa. Adhabu ikiwa Kali na rushwa inakua kubwa hivyo inageuka kuwa ni dili badala ya kudhibiti vitendo hivyo.

Sheria ya ubakaji hata mtu akipata ngono Kwa ahadi ya madaraka au cheo Huko ni kubaka. Je,ni wangapi wanabakwa Kwa manufaa yao ? Mashuleni,vyuoni na makazini Kwa kuahidiwa kupewa haki kwa Upendeleo?

Adhabu Kali inaondoa makosa kama rushwa itaondoka. Hakuna Sugu wa kufa. Vibaka wangekatwa mikono kama Mila nzuri za kiislam zinavyoelekeza wizi ungeisha kabisa. Kuna nchi hakuna wizi na maendeleo ni makubwa. Tanzania watu wanaambiana bila wizi huwezi kutoboa.

Matatizo ya Waafrika ni zao la viongozi wa bovu na sio Ukoloni. Wakoloni wameondoka miaka mingi na hatukusikia kuwa walikua wanaibia serikali zao ili wajilimbikizie Mali tofauti na Sasa viongozi Wanapeana ulaji kupitia ofisi za umma
 
Maswali magumu kuhusu ubaguzi katika Dini duniani:-

1. Mwafrika anawezakuwa Papa?

2. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Anglican duniani?

3. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Lutheran duniani?

4. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Suni duniani?

5. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Shia duniani?

6. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Ibadi duniani?

7. Mwafrika anaweza kuwa Mkuu wa Ismailia duniani?

8. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Kokni Muslim duniani?

9. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Mennonite duniani?

10. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa SDA duniani?

11. Mwafrika anawezakuwa Mkuu wa Budha duniani?

Je, dini hizi zinamilikiwa na Wazungu, Waarabu, Wahindi, Waasia (Budha) au Waafrika?

Je, dini hizi za Mzungu, Mwarabu, Mhindi na Mu-asia zilishushwa toka Mbinguni au zilianzishwa hapa hapa duniani?

Je, Waafrika hatukuwa na dizi zetu? Zilienda wapi?

Je, kuna madhara gani Waafrika tukirejea dini zetu na kuwaachia Wazungu, Waarabu, Wahindi, Waasia (Budha) za kwao wanazotubagua nazo?

Aidha, kwenye Soccer pia sina hakika kama Rais wa FIFA anawezakuwa Mwafrika.

Tujadili mada tupate maarifa.

View attachment 2125428
Mkuu wa Ufalme wa Uingereza na Mkuu wa Dhehebu la Kianglikana duniani.

View attachment 2128596
Mkuu wa nchi ya Vatican na Mkuu wa Dhehebu la Kikatoliki duniani.

See the source image

Mkuu wa Jumuiya (Diaspora) kubwa iliyosambaa duniani ya Wana-Ismailia na Mkuu wa Dhehebu la Ismailia duniani.

Taswira zote kwa hisani ya google.
Wengine tunaamini ni utapeli wa kiimani na kiroho.
Maisha ni kuamuwa tu, amini chochote na kuabudu hata ng'ombe poa tu, ila tahadhari, fuata sheria za nchi bila shuruti ama sivyo utaishia pabaya
 
Dini ni biashara ya uchuuzi wa sadaka kutoka afrika kuelekea roma. Na bado biashara hii ina nguvu zaidi afrika.
 
Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat.....?

Is this a new revelation?

Why not preached and taught in everyday life?

My friend! won't they behead you for this secret and bitter truth?
Hakuna mtu anayeweza kujitokea kuyafundisha haya ni kudanganyana tu ndo wanajua
 
Acha siasa.

Mmisionari wa kwanza aliika Zanzibar akakuta Kuna serikali ya Sultani na Waislam walikuwepo. Na hata waliotafsiri Biblia walikua ni waislam na walimpa mpaka Eneo la kujenga kanisa. Walikuta tayari waafrika tunatawaliwa na Waarabu Kwa Karne nyingi. Dini ni dini na serikali ni serikali tangu enzi za Farao.

Kinachafanyika ni serikali kuweka chawa wake Kwa baadhi ya watu kwenye dini ili watawake kwa urahisi. Mimi nimetokea kwenye Eneo lililofikiwa na Wamisionari wa mwanzo kabisa Amini usiamini walikua ni watu Wazuri sana huwezi kuwalinganisha hata na viongozi wa dini wa Leo.

Huwezi kuwalinganisha hata na wanasiasa wa Leo. Vitabu vingi vya historia ni vya uongo kutokana na mahitaji na malengo ya wapigania nafasi za madaraka kupitia kile walichokiita Uhuru. Wasingeweza kuwasifia wakoloni wakati wanataka kuwaondia madarakani. Hata Leo inatokea Kwa wapinzani wanapotaka kuwatoa watawala madarakani ni lazima wawape Jina baya.

Serikali ya Kikoloni ilikua ni katili kama zilivyo serikali nyingi Duniani mpaka Leo. Mbowe anateseka gerezani sio kwamba anateswa na wazungu Bali ni Watawala wanaolinda utawala wao dhidi ya upinzani. Wakoloni waligeuka kuwa wabaya sana baada ya watu kuanza kudai uhuru na kuhujumu Miundo mbinu yao ya kiuchumi.

Hata Leo ukitaka kuiona serikali kuwa Haina Cha mkoloni Wala Mwafrika jaribu kuhujumu Miundo mbinu yake au kudai haki Kwa nguvu. Ni hulka ya binadamu sio dini Wala rangi. Nyerere alilelewa na wamisionari na watawala wengi ni zao la wamisionari. Wangekua wabaya kivile tunavyodanganywa wasingewapa Elimu ya kujitawala.

Wangekua wabaya wasingeweza kuvunja ukabila uliokua umejichimbia kila mahali na kuzaa viligha vingi mana watu walikua hata hawachangamani. Watu wakajikuta wanakutana Misikitini na makanisani wa makabila tofauti. Wanakutana kwenye shule. Wamisionari walijitoa sana.

Leo hii Kuna wahubiri wabongo wenzetu lakini hawana msaada wowote wa kijamii zaidi ya kumiliki Makanisa mijini na kula Bata,hawawezi kuishi vijijini na maporini kama wamisionari walivyotoka kwao na kuja Afrika kuishi maisha mapya Kwa watu wasiojua kusoma Wala kuandika.

Usifikiri ilikua ni kazi rahisi. Ilihitaji akili kubwa. Nilikaa Mzee mmoja alizaliwa mwaka 1904 akasomo mpaka darasa la nne akawa Karani wa Wazungu Mission sehemu Moja sitaitaja jina. Alikua ni Muislam . Sijawahi kumsikia akiwasema vibaya wamisionari. Waliheshimu sana dini yake na walimshauri abadili dini lakini alikataa kabisa.

Walikua wanafuga na kula nguruwe lakini yeye alikua anapewa chakula tofauti na nyama ya nguruwe. Walikua wanamtania TU na sio kimlazimisha kula nguruwe. Walikua ni waungwana sana. Huyo Mzee alikua analaumu sana serikali baada ya uhuru. Alikua anasikitika jinsi watu walivyokuwa wanavunja Sheria bila kuchukuliwa hatua Kali.

Hata Leo Kuna watu wasioipenda serikali kutokana na kukandamizwa; watu hao kwao viongozi wa dini wanaonekana kuwa ni usalama wa Taifa na kikwazo kikubwa na hata kuambiwa kuwa wanalinda Chama Tawala. Kumbe ni Ile hali TU ya dini kujaribu kujiepusha na Dola na mambo yake. Kuuchukia Ukolini isiwe sababu ya kuwachukia Wamisionari waliotutoa kwenye Giza Nene la ukabila na ujinga.

Wamisionari walikaa sana Kilimanjaro, Iringa, Kagera ,Lushoto na Masasi. Sasa ,jiulize, je, watu wa maeneo hayo waliteswa na kukandamizwa na wamisionari? Je,watu wa maeneo hayo walikosa maendeleo,Elimu,Afya na Miundo mbinu mingine?
Ni Kwa nini maeneo hayo ndiyo yenye maendeleo na wasomi wengi endapo wamisionari walikua ni wabaya.? Si wengeendelea zaidi maeneo mengine ?

Baada ya uhuru watawala wa Kiafrika walijilimbikizia sifa zote nzuri na kuandika historia inayoonyesha kuwa Watu weupe hakuna jema hata Moja walilolifanya Afrika zaidi ya kuiba Mali zetu. Wakati huo huo watawala hao walijigeuza na kuwa wakoloni wabaya mara mia ya wakoloni mpaka Leo Kwa kutumia vitabu vya historia.
Unasema "babu zetu wasingewepanda wamissionary kama wengukua wabaya".
Unasahau, wamissionary walifika na zawadi na tabasamu wakihubiri tu neno. Wamissionary hawakuingia na bunduki, bali zawadi na tabasamu kwasababu nia yao walifika ili watuchunguze. Wakajifanya ni marafiki. Lakini nyuma ya pazia walirudi kwao na kupeleka taarifa zilizotuletea matatizo na walijua serikali zao zingetufanya nini baada ya wao kurudi nyumbani na kupeleka taarifa.
.
Muafrika ni mtu rahisi sana kurubunika, cheki wewe maskini wamekurubuni hadi unawepanda wakoloni na huambiliki chochote. Matokeo yake wanakudharau tu. Inasikitisha sana😔
 
Acha siasa.
Mmisionari wa kwanza aliika Zanzibar akakuta Kuna serikali ya Sultani na Waislam walikuwepo.
Na hata waliotafsiri Biblia walikua ni waislam na walimpa mpaka Eneo la kujenga kanisa. Walikuta tayari waafrika tunatawaliwa na Waarabu Kwa Karne nyingi.
Dini ni dini na serikali ni serikali tangu enzi za Farao.

Kinachafanyika ni serikali kuweka chawa wake Kwa baadhi ya watu kwenye dini ili watawake kwa urahisi. Mimi nimetokea kwenye Eneo lililofikiwa na Wamisionari wa mwanzo kabisa Amini usiamini walikua ni watu Waziri sana huwezi kuwalinganisha hata na viongozi wa dini wa Leo. Huwezi kuwalinganisha hata na wanasiasa wa Leo. Vitabu vingi vya historia ni vya uongo kutokana na mahitaji na malengo ya wapigania nafasi za madaraka kupitia kile walichokiita Uhuru. Wasingeweza kuwasifia wakoloni wakati wanataka kuwaondia madarakani. Hata Leo inatokea Kwa wapinzani wanapotaka kuwatoa watawala madarakani ni lazima wawape Jina baya.

Serikali ya Kikoloni ilikua ni katili kama zilivyo serikali nyingi Duniani mpaka Leo. Mbowe anateseka gerezani sio kwamba anateswa na wazungu Bali ni Watawala wanaolinda utawala wao dhidi ya upinzani. Wakoloni waligeuka kuwa wabaya sana baada ya watu kuanza kudai uhuru na kuhujumu Miundo mbinu yao ya kiuchumi. Hata Leo ukitaka kuiona serikali kuwa Haina Cha mkoloni Wala Mwafrika jaribu kuhujumu Miundo mbinu yake au kudai haki Kwa nguvu. Ni hulka ya binadamu sio dini Wala rangi. Nyerere alilelewa na wamisionari na watawala wengi ni zao la wamisionari. Wangekua wabaya kivile tunavyodanganywa wasingewapa Elimu ya kujitawala. Wangekua wabaya wasingeweza kuvunja ukabila uliokua umejichimbia kila mahali na kuzaa viligha vingi mana watu walikua hata hawachangamani. Watu wakajikuta wanakutana Misikitini na makanisani wa makabila tofauti. Wanakutana kwenye shule. Wamisionari walijitoa sana. Leo hii Kuna wahubiri wabongo wenzetu lakini hawana msaada wowote wa kijamii zaidi ya kumiliki Makanisa mijini na kula Bata,hawawezi kuishi vijijini na maporini kama wamisionari walivyotoka kwao na kuja Afrika kuishi maisha mapya Kwa watu wasiojua kusoma Wala kuandika. Usifikiri ilikua ni kazi rahisi. Ilihitaji akili kubwa.

Nilikaa Mzee mmoja alizaliwa mwaka 1904 akasomo mpaka darasa la nne akawa Karani wa Wazungu Mission sehemu Moja sitaitaja jina. Alikua ni Muislam . Sijawahi kumsikia akiwasema vibaya wamisionari. Waliheshimu sana dini yake na walimshauri abadili dini lakini alikataa kabisa. Walikua wanafuga na kula nguruwe lakini yeye alikua anapewa chakula tofauti na nyama ya nguruwe. Walikua wanamtania TU na sio kimlazimisha kula nguruwe. Walikua ni waungwana sana. Huyo Mzee alikua analaumu sana serikali baada ya uhuru. Alikua anasikitika jinsi watu walivyokuwa wanavunja Sheria bila kuchukuliwa hatua Kali.

Hata Leo Kuna watu wasioipenda serikali kutokana na kukandamizwa; watu hao kwao viongozi wa dini wanaonekana kuwa ni usalama wa Taifa na kikwazo kikubwa na hata kuambiwa kuwa wanalinda Chama Tawala. Kumbe ni Ile hali TU ya dini kujaribu kujiepusha na Dola na mambo yake. Kuuchukia Ukolini isiwe sababu ya kuwachukia Wamisionari waliotutoa kwenye Giza Nene la ukabila na ujinga.

Wamisionari walikaa sana Kilimanjaro, Iringa, Kagera ,Lushoto na Masasi. Sasa ,jiulize, je, watu wa maeneo hayo waliteswa na kukandamizwa na wamisionari? Je,watu wa maeneo hayo walikosa maendeleo,Elimu,Afya na Miundo mbinu mingine?
Ni Kwa nini maeneo hayo ndiyo yenye maendeleo na wasomi wengi endapo wamisionari walikua ni wabaya.? Si wengeendelea zaidi maeneo mengine ?

Baada ya uhuru watawala wa Kiafrika walijilimbikizia sifa zote nzuri na kuandika historia inayoonyesha kuwa Watu weupe hakuna jema hata Moja walilolifanya Afrika zaidi ya kuiba Mali zetu. Wakati huo huo watawala hao walijigeuza na kuwa wakoloni wabaya mara mia ya wakoloni mpaka Leo Kwa kutumia vitabu vya historia.
Kwahiyo hawa Waafrika na wengineo nisiowataja walikuja kusaliti uaminifu wao kwa wakoloni hawa waliowapa uhuru na vyeo vya Urais na Uwaziri Mkuu?

Mandela vs State President C.R. Swart 1962 and Pik Botha 1990.

Mugabe and Canaan Banana vs Ian Smith.

Kaunda and Banana, Mugabe vs Cecil Rhodes.

Nyerere vs Sir Richard Turnbull.

Karume and Nyerere vs Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said.

Oginga and Kenyatta vs Sir Patrick Muir Renison.

Obote and Mutesa II vs Sir Walter Coutts.

Sheria Kali ikitekelezwa ndugu yangu watu wanabadilika.

Daudi alichepuka mana alijua mfalme yupo juu ya Sheria. Ndio maana Mungu aliingilia kati na kumwadhibu mana hapakua na mtu wa kumwadhibu mfalme.

Wanawake wanakua bidhaa ya kujiuza na kutafuta kipato Kwa zinaa mana Kuna kitu kinaitwa haki sawa. Lakini hakuna shujaa mbele ya adhabu ya kufa.

Kuna mwamba alikaa madarakani miaka mitano TU nchi ikanyooka kwasababu ukikaidi unapitezwa fasta unaacha familia yako. Kila mtu akawa na hofu. Tatizo hata kesi za kubaka ni rushwa. Adhabu ikiwa Kali na rushwa inakua kubwa hivyo inageuka kuwa ni dili badala ya kudhibiti vitendo hivyo. Sheria ya ubakaji hata mtu akipata ngono Kwa ahadi ya madaraka au cheo Huko ni kubaka. Je,ni wangapi wanabakwa Kwa manufaa yao ? Mashuleni,vyuoni na makazini Kwa kuahidiwa kupewa haki kwa Upendeleo?

Adhabu Kali inaondoa makosa kama rushwa itaondoka. Hakuna Sugu wa kufa. Vibaka wangekatwa mikono kama Mila nzuri za kiislam zinavyoelekeza wizi ungeisha kabisa. Kuna nchi hakuna wizi na maendeleo ni makubwa. Tanzania watu wanaambiana bila wizi huwezi kutoboa. Matatizo ya Waafrika ni zao la viongozi wa bovu na sio Ukoloni. Wakoloni wameondoka miaka mingi na hatukusikia kuwa walikua wanaibia serikali zao ili wajilimbikizie Mali tofauti na Sasa viongozi Wanapeana ulaji kupitia ofisi za umma
Hahahaaaa..... "...wanabakwa kwa manufaa yao..." hahahaaaa.....
 
Kwahiyo hawa Waafrika na wengineo nisiowataja walikuja kusaliti uaminifu wao kwa wakoloni hawa?

Mandela vs State President C.R. Swart 1962 and Pik Botha 1990.

Mugabe vs Ian Smith.

Kaunda and Mugabe vs Cecil Rhodes.

Nyerere vs Sir Richard Turnbull.

Karume and Nyerere vs Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said.

Oginga and Kenyatta vs Sir Patrick Muir Renison.

Obote and Mutesa II vs Sir Walter Coutts.

Hahahaaaa..... "...wanabakwa kwa manufaa yao..." hahahaaaa.....
First year ana miaka 17 anabakwa ili asipate sup. Akikataa anafeli anarudi mtaani jamii haimsikilizi inamcheka na wengine wanadiriki kumwambia acha ujinga kwani ataondoka nayo ,mtumikie kafiri upate mradi wako.
Akienda Polisi ,anaombwa ngono( anabakwa Tena) asaidiwe kesi yake. Akienda Kwa wajuu yake naye anamwambia nikubalie Mimi mana yule yupo chini yangu hawezi kukusaidia. Akienda Kwa mkuu kitengo naye hamsikilizi mana hua anambaka secretary ili ampe safari na posho.
Akienda mahakamani anakutana na hakimu aliyekua amebakwa ili asifelishwe kwenye mitihani. Ni jamii iliyojaa waovu wenye nguvu kifedha ,kielimu na kimadaraka.

Sheria Kali inayosimamia Kwa haki bila Upendeleo ni mwiba Kwa waovu.
 
Kwahiyo hawa Waafrika na wengineo nisiowataja walikuja kusaliti uaminifu wao kwa wakoloni hawa waliowapa uhuru na vyeo vya Urais na Uwaziri Mkuu?

Mandela vs State President C.R. Swart 1962 and Pik Botha 1990.

Mugabe and Canaan Banana vs Ian Smith.

Kaunda and Banana, Mugabe vs Cecil Rhodes.

Nyerere vs Sir Richard Turnbull.

Karume and Nyerere vs Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said.

Oginga and Kenyatta vs Sir Patrick Muir Renison.

Obote and Mutesa II vs Sir Walter Coutts.

Hahahaaaa..... "...wanabakwa kwa manufaa yao..." hahahaaaa.....
Mugabe alikua ni kuwadi wa Mabeberu Kwa muda mrefu mpaka vilipoanzishwa vyama vingi ndipo akaona wananchi wamemchoka. Akataifisha mashamba ya Wazungu akawagawia maafisa wa juu wa Jeshi na Polisi na usalama wa Taifa kama rushwa ya kuwadhibiti wapinzani na wageni. Katiba ikamlinda. Akavuruga nchi zaidi na kuvuruga uchumi.
 
First year ana miaka 17 anabakwa ili asipate sup. Akikataa anafeli anarudi mtaani jamii haimsikilizi inamcheka na wengine wanadiriki kumwambia acha ujinga kwani ataondoka nayo ,mtumikie kafiri upate mradi wako.
Akienda Polisi ,anaombwa ngono( anabakwa Tena) asaidiwe kesi yake. Akienda Kwa wajuu yake naye anamwambia nikubalie Mimi mana yule yupo chini yangu hawezi kukusaidia. Akienda Kwa mkuu kitengo naye hamsikilizi mana hua anambaka secretary ili ampe safari na posho.
Akienda mahakamani anakutana na hakimu aliyekua amebakwa ili asifelishwe kwenye mitihani. Ni jamii iliyojaa waovu wenye nguvu kifedha ,kielimu na kimadaraka.

Sheria Kali inayosimamia Kwa haki bila Upendeleo ni mwiba Kwa waovu.
Kwahiyo maisha by 90% ni kubakana tu hadi Makleri na Maustaadh nao wanabaka siku hizi. Tukimbilie wapi?

Ndiyo maana Afrika Kusini wameona bora yaishe wakaja na sheria ya mwanamke kuolewa na wanaume wengi kwa wakati mmoja na mwanaume kuoa wanawake wengi kwa wakati mmoja (hakuna idadi kama zile ndoa za Kikristo na Kiislamu).

Sheria kali zinafifishwa kwa kudurusiwa (reviewed) na utawala mpya unavyoingia. Enzi ya Magufuli ela za serikali ziliogopwa kama Corona kwa sababu ya sheria kali, leo hali siyo hiyo, ela za serikali ndiyo tamu.... kama bia za bar, zinawindwa hata gizani kuliko ela za sekta binafsi.
 
Makleri, Maustaadh, Mitume na Manabii nao siku hizi tunasikia wanabaka eti.

Nafikri ndiyo maana Papa wa kwanza labda aliona akaweka sera ya Useja (Celibacy) na kuweka laana ndani ya sera hiyo. Kwa laana hiyo, Mtawa au Kleri akizaa lazima mtoto anakuwa chizi tuuuu...... hivyo watu wenye roho za Uyezebeli (Ukahaba) wanawakwepa sana Makleri na Watawa kwa kuogopa kuzaa watoto machizi,
 
Kwahiyo maisha by 90% ni kubakana tu hadi Makleri na Maustaadh nao wanabaka siku hizi. Tukimbilie wapi?

Ndiyo maana Afrika Kusini wameona bora yaishe wakaja na sheria ya mwanamke kuolewa na wanaume wengi kwa wakati mmoja na mwanaume kuoa wanawake wengi kwa wakati mmoja (hakuna idadi kama zile ndoa za Kikristo na Kiislamu).

Sheria kali zinafifishwa kwa kudurusiwa (reviewed) na utawala mpya unavyoingia. Enzi ya Magufuli ela za serikali ziliogopwa kama Corona kwa sababu ya sheria kali, leo hali siyo hiyo, ela za serikali ndiyo tamu.... kama bia za bar, zinawindwa hata gizani kuliko ela za sekta binafsi.
Dawa ni Moja TU watu wema kuungana dhidi ya waovu.
Waovu wachache hua wanatumia mbinu nyingi kuwatesha watu wema mpaka wanaufyata.
Mfano ni Mitaani unakuta vibaka wapo Wawili wanasumbua mtaa wenye Wakazi mia Tano . Wanajifungia ndani na mageti na sengenge . Badala ya wengi kuungana na kuwakamata vibaka Wawili na kukata viweko wao ndio wanatishwa na vipanga viwili badala ya kutoka na Mashoka na mishale na kuwawinda vibaka mtaa ukabaki salama.
 
“For evil to flourish, all that is needed is for good men choosing to do nothing, [Burke, E. 1756]”
 
Dini na madhehebu yana wamiliki wake, sio mungu. RC wamiliki wako Italia, Anglican wako UK, Lutheran wako Ujerumani, SDA wako USA, Shia na Suni wako Uarabuni, Budha wako India, Shinto wako Japan, nk.

Viongozi wa hizo dini popote walipo Duniani lazima wa report ama kuchaguliwa na kua endorsed na hao viongozi wao kutoka makao makuu.

Sisi huku Afrika kazi ni kupokea tu hizi dini, kupumbaza watu na kuwafanya waendelee kua masikini kwa kuwatoza michango isiyo na kichwa wala miguu kwa jina la zaka, sadaka na michango mingine, kiasi kidogo kinabakia hapa kikubwa wanapelekewa wamiliki wa kanisa huko walipo.

Nawapongeza hawa kina Kakobe, Gwajima, Mwamposa wao kuanzisha makanisa yao na wao kua wamiliki na kula hizo hela. Watu mnachangaje hela Tanzania anapelekewa papa italia kula? Wakila kina Mwamposa maneno ila anazokula Papa hazisemwi.
HV yanaukweli haya lkn
 
Unasema "babu zetu wasingewepanda wamissionary kama wengukua wabaya".
Unasahau, wamissionary walifika na zawadi na tabasamu wakihubiri tu neno. Wamissionary hawakuingia na bunduki, bali zawadi na tabasamu kwasababu nia yao walifika ili watuchunguze. Wakajifanya ni marafiki. Lakini nyuma ya pazia walirudi kwao na kupeleka taarifa zilizotuletea matatizo na walijua serikali zao zingetufanya nini baada ya wao kurudi nyumbani na kupeleka taarifa.
.
Muafrika ni mtu rahisi sana kurubunika, cheki wewe maskini wamekurubuni hadi unawepanda wakoloni na huambiliki chochote. Matokeo yake wanakudharau tu. Inasikitisha sana😔

Sio KILA ulichodanganywa kwenye somo la historia ni sahihi,mengi yalijaa chuki dhidi ya weupe.
Missionary awakuja kuchunguza wao walileta dini kwa maagizo ya Yesu Kristo ambae hakuwa Mzungu.
Wakaja wakakuta dini za jadi ni dhaifu kuweza kushindana na dini mpya.
Hii ni nature kwenye competition ya kiimani imani bora ndiyo inasimama.
 
Kuna mmoja yuko Matembele Dsm, kumuona ili akuombee lazima ufanye booking kwa 300,000/, anakiita kiasi hicho kama ni Consultation Fee. Yesu na Mitume kuwaona ilikuwa ni bure.

View attachment 2134160
Taswira kwa hisani ya google.
Anapingana na maagizo ya Yesu,Yesu aliagiza injili isiuzwe anaeuza injili hao ni mawakala wa kuzimu utumia white magic kutenda miujiza.Ukimjua Mungu ukiyajua maandiko utakuwa huru wala uhitaji nabii au mganga wa kienyeji kutatua shida zako.
Wengi ni wateja wa mitume na manabii sababu ni vipofu awataki kujifunza maandiko KILA kitu kipo wazi.
Mtumishi yeyeto anaetoza pesa Ili akuombee au akuuzie upako huyo ni agent no 666

Screenshot_20220315_072316.jpg
 
Sio KILA ulichodanganywa kwenye somo la historia ni sahihi,mengi yalijaa chuki dhidi ya weupe.
Missionary awakuja kuchunguza wao walileta dini kwa maagizo ya Yesu Kristo ambae hakuwa Mzungu.
Wakaja wakakuta dini za jadi ni dhaifu kuweza kushindana na dini mpya.
Hii ni nature kwenye competition ya kiimani imani bora ndiyo inasimama.
Ubaya wa historia kuhusu wakoloni huwezi kuthibitisha kwamba wamissionary walikua na nia njema. Utanipa tu story na wewe ulizodanganywa.

Wewe unathibitisha vipi yesu alitoa hayo maagizo zaidi tu ya kusimuliwa hadithi na kupewa biblia ambazo ni madai ( claims) ya watu kuwa ni neno la Mungu.
Yani sisi tupo Tanzania alafu wanakuja watu wanasema wanatuletea maagizo ya Mungu na wewe unaona ni sahii🤦🏾‍♂️
 
Mkuu rejea kwenye vitabu tena...ukristo umeanzia ulaya..kuna tofauti kubwa kati ya yesu na ukristo...!!kimsingi yesu hakuwa mtu wa bara ulaya lkn pia hakua mkristo!!ukristo umetoka bara ulaya hata yesu mwenyewe haujui ukristo maana umeanzishwa mwishoni mwa karne ya 3 baada ya yesu kupigwa zake huko na kuuwawa kwa sababu alikua akipinga dola ya urumi..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Sio KILA ulichodanganywa kwenye somo la historia ni sahihi,mengi yalijaa chuki dhidi ya weupe.
Missionary awakuja kuchunguza wao walileta dini kwa maagizo ya Yesu Kristo ambae hakuwa Mzungu.
Wakaja wakakuta dini za jadi ni dhaifu kuweza kushindana na dini mpya.
Hii ni nature kwenye competition ya kiimani imani bora ndiyo inasimama.
kijana historia imeandikwa na hao hao wazungu!

Jarbu kufanya hivi.
kuanzia sasa futa yooote ambayo ulifundishwa ukiwa kama mtumwa na anza kujifunza upya yale ambayo hawakutaka ujufunze.
mfano. Magic, Numerology, demonology, AstrolOGY.

NA YOTE KWA YOTE JIFUNZE TRUE AFRICAN HISTORY,
Hapa kuna waafrica ambao hawana ajenda yoyote zaidi yakutaka wewe ujue wapi ulipotoka wapo wengi wana historia wa kiafrika wameandika vitabu.
 
Back
Top Bottom