Huh[emoji15]
We jamaa umechotwa akili kweli.
Wamissionary walikua watangulizi wa ukoloni, walikuja kwa kisingizio cha kuleta habari njema ( biblia) lakini waliporudi kwao walipeleka taarifa za kiintelijensia kuhusu tamaduni zetu na resources tulizonazo.
Wamissionary walichangia sisi kurahisishwa kuvamiwa na kusign bogus treaties.
Wewe bibi yako kakudanganga unakuja kutudanganya na sisi kwasababu unapenda watu waliotuvamia kwa bunduki na kutuuza kama watumwa.
Waafrika ndio maana tunadharaulika.
Acha siasa.
Mmisionari wa kwanza aliika Zanzibar akakuta Kuna serikali ya Sultani na Waislam walikuwepo. Na hata waliotafsiri Biblia walikua ni waislam na walimpa mpaka Eneo la kujenga kanisa. Walikuta tayari waafrika tunatawaliwa na Waarabu Kwa Karne nyingi. Dini ni dini na serikali ni serikali tangu enzi za Farao.
Kinachafanyika ni serikali kuweka chawa wake Kwa baadhi ya watu kwenye dini ili watawake kwa urahisi. Mimi nimetokea kwenye Eneo lililofikiwa na Wamisionari wa mwanzo kabisa Amini usiamini walikua ni watu Wazuri sana huwezi kuwalinganisha hata na viongozi wa dini wa Leo.
Huwezi kuwalinganisha hata na wanasiasa wa Leo. Vitabu vingi vya historia ni vya uongo kutokana na mahitaji na malengo ya wapigania nafasi za madaraka kupitia kile walichokiita Uhuru. Wasingeweza kuwasifia wakoloni wakati wanataka kuwaondia madarakani. Hata Leo inatokea Kwa wapinzani wanapotaka kuwatoa watawala madarakani ni lazima wawape Jina baya.
Serikali ya Kikoloni ilikua ni katili kama zilivyo serikali nyingi Duniani mpaka Leo. Mbowe anateseka gerezani sio kwamba anateswa na wazungu Bali ni Watawala wanaolinda utawala wao dhidi ya upinzani. Wakoloni waligeuka kuwa wabaya sana baada ya watu kuanza kudai uhuru na kuhujumu Miundo mbinu yao ya kiuchumi.
Hata Leo ukitaka kuiona serikali kuwa Haina Cha mkoloni Wala Mwafrika jaribu kuhujumu Miundo mbinu yake au kudai haki Kwa nguvu. Ni hulka ya binadamu sio dini Wala rangi. Nyerere alilelewa na wamisionari na watawala wengi ni zao la wamisionari. Wangekua wabaya kivile tunavyodanganywa wasingewapa Elimu ya kujitawala.
Wangekua wabaya wasingeweza kuvunja ukabila uliokua umejichimbia kila mahali na kuzaa viligha vingi mana watu walikua hata hawachangamani. Watu wakajikuta wanakutana Misikitini na makanisani wa makabila tofauti. Wanakutana kwenye shule. Wamisionari walijitoa sana.
Leo hii Kuna wahubiri wabongo wenzetu lakini hawana msaada wowote wa kijamii zaidi ya kumiliki Makanisa mijini na kula Bata,hawawezi kuishi vijijini na maporini kama wamisionari walivyotoka kwao na kuja Afrika kuishi maisha mapya Kwa watu wasiojua kusoma Wala kuandika.
Usifikiri ilikua ni kazi rahisi. Ilihitaji akili kubwa. Nilikaa Mzee mmoja alizaliwa mwaka 1904 akasomo mpaka darasa la nne akawa Karani wa Wazungu Mission sehemu Moja sitaitaja jina. Alikua ni Muislam . Sijawahi kumsikia akiwasema vibaya wamisionari. Waliheshimu sana dini yake na walimshauri abadili dini lakini alikataa kabisa.
Walikua wanafuga na kula nguruwe lakini yeye alikua anapewa chakula tofauti na nyama ya nguruwe. Walikua wanamtania TU na sio kimlazimisha kula nguruwe. Walikua ni waungwana sana. Huyo Mzee alikua analaumu sana serikali baada ya uhuru. Alikua anasikitika jinsi watu walivyokuwa wanavunja Sheria bila kuchukuliwa hatua Kali.
Hata Leo Kuna watu wasioipenda serikali kutokana na kukandamizwa; watu hao kwao viongozi wa dini wanaonekana kuwa ni usalama wa Taifa na kikwazo kikubwa na hata kuambiwa kuwa wanalinda Chama Tawala. Kumbe ni Ile hali TU ya dini kujaribu kujiepusha na Dola na mambo yake. Kuuchukia Ukolini isiwe sababu ya kuwachukia Wamisionari waliotutoa kwenye Giza Nene la ukabila na ujinga.
Wamisionari walikaa sana Kilimanjaro, Iringa, Kagera ,Lushoto na Masasi. Sasa ,jiulize, je, watu wa maeneo hayo waliteswa na kukandamizwa na wamisionari? Je,watu wa maeneo hayo walikosa maendeleo,Elimu,Afya na Miundo mbinu mingine?
Ni Kwa nini maeneo hayo ndiyo yenye maendeleo na wasomi wengi endapo wamisionari walikua ni wabaya.? Si wengeendelea zaidi maeneo mengine ?
Baada ya uhuru watawala wa Kiafrika walijilimbikizia sifa zote nzuri na kuandika historia inayoonyesha kuwa Watu weupe hakuna jema hata Moja walilolifanya Afrika zaidi ya kuiba Mali zetu. Wakati huo huo watawala hao walijigeuza na kuwa wakoloni wabaya mara mia ya wakoloni mpaka Leo Kwa kutumia vitabu vya historia.