Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
- Thread starter
- #141
Alafu kujuwa ukweli wa madai ya Karl Marx kwamba dini ni kilevi cha kusaidia kutawala watu wanyonge ebu ona hii:-Waadventista wa Sabato wanamuamini Yesu lakini hawaamini tarehe ya kuzaliwa kwake (25 Disemba) japo wao nao hawana tarehe halisi (mbadala ya hiyo). Pia wanapromote siku ya ibada (Sabato) ambayo Biblia hiyo hiyo inasema hatuko chini ya Torati, kwao usipoishika Torati ya Sabato basi hutoziona Mbingu.
Wakatoliki wanamfanya/wanampromote Bikira Maria kama nafsi ya pili ya Mungu na kwamba Mungu ana nafsi nne (Baba, Maria, Yesu, Roho Mtakatifu)
Lutheran Chapel ya Harvard University US, chuo maarufu duniani kwa vipanga, kama Wakatoliki, nao wanaamini nafsi nne za Mungu (Baba, Mama, Mwana, Roho Mtakatifu), kwamba hakuna Mwana na Baba bila Mama, japo hawasemi Mama wanayemmaanisha ni Maria ua la, aidha, hawatuambii Mungu alioa lini? Binti wa nani? Ndoa ya Mungu ilifungwa Kanisa lipi? Na Mchungaji yupi?
Hivi sasa kuna versions za Biblia 25 na zinaendelea kuongezwa zingine, Wakatoliki wame-expand Biblia kwa kuongeza vitabu vipya. Kuna hatari siku za mbeleni tukawa na vitabu labda vinaitwa Injili ya Papa Mtakatifu, au Waraka wa Bikira Maria kwa Watu Weusi au Injili ya Malkia Elizabeth Mtakatifu (kwa Waanglikana).
Ni mapambano kama unavyosema japo siyo ya Msalaba bali ya falsafa za kiimani.
TUMEVURUGWA AFRIKA! DUNIA IMEVURUGWA!
1. Malkia Elizabeth ni Mkuu wa Ufalme wa Uingereza na Kiongozi wa Anglikan duniani (japo hana taaluma ya Theologia)
2. Papa ni Mkuu wa nchi ya Vatican na Kiongozi wa Roman Catholic duniani.
3. Aga Khan (Aga Khan siyo jina ni cheo/title kama ambavyo Farao pia ni cheo/title) ni Kiongozi wa Ismailia (ambayo ndiyo diaspora inayoongoza duniani kwa idadi kubwa, wanawezatengeneza nchi maana ndiyo wameshika biashara kubwa kubwa pia huko duniani)
Tukirudi kwenye namba 1 na 2 hapo juu, ni kwamba ili wafanikiwe kutawala kama anavyosema Marx, waliwaandikia watu kwenye Biblia namna ya kuwaheshimu ili wadumu kwenye nyadhifa zao, soma ile Scripture ya Rumi.13:1-7 “Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu.
Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala anapinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu, kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumuogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.
Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na upanga bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. Kwahiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.
Kwa sababu hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. Walipeni wote haki zao, Mtu wa kodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mlipe ushuru, astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, mheshimu.
Sasa viongozi wa Afrika ambao ni copy paste (wasiotumia initiatives zao wanatumia hii Rumi.13:1-7 kama Implied Article of the Constitution) ili nao waendelee kutawala bila bughudha kama hao namba 1 na 2.
AFRIKA TUMENASA.
Asomaye na afahamu.