Waadventista wa Sabato wanamuamini Yesu lakini hawaamini tarehe ya kuzaliwa kwake (25 Disemba) japo wao nao hawana tarehe halisi (mbadala ya hiyo). Pia wanapromote siku ya ibada (Sabato) ambayo Biblia hiyo hiyo inasema hatuko chini ya Torati, kwao usipoishika Torati ya Sabato basi hutoziona Mbingu.
Wakatoliki wanamfanya/wanampromote Bikira Maria kama nafsi ya pili ya Mungu na kwamba Mungu ana nafsi nne (Baba, Maria, Yesu, Roho Mtakatifu)
Lutheran Chapel ya Harvard University US, chuo maarufu duniani kwa vipanga, kama Wakatoliki, nao wanaamini nafsi nne za Mungu (Baba, Mama, Mwana, Roho Mtakatifu), kwamba hakuna Mwana na Baba bila Mama, japo hawasemi Mama wanayemmaanisha ni Maria ua la, aidha, hawatuambii Mungu alioa lini? Binti wa nani? Ndoa ya Mungu ilifungwa Kanisa lipi? Na Mchungaji yupi?
Hivi sasa kuna versions za Biblia 25 na zinaendelea kuongezwa zingine, Wakatoliki wame-expand Biblia kwa kuongeza vitabu vipya. Kuna hatari siku za mbeleni tukawa na vitabu labda vinaitwa Injili ya Papa Mtakatifu, au Waraka wa Bikira Maria kwa Watu Weusi au Injili ya Malkia Elizabeth Mtakatifu (kwa Waanglikana).
Ni mapambano kama unavyosema japo siyo ya Msalaba bali ya falsafa za kiimani.
TUMEVURUGWA AFRIKA! DUNIA IMEVURUGWA!