1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Sheria Kali ikitekelezwa ndugu yangu watu wanabadilika.Kuna school of thought (mkondo wa uelewa) kwamba mojawapo ya madhara ya dini za kigeni ni mporomoko wa kimaadili ya asili ya Waafrika. Katika mkondo huo wa uelewa yafuatayo yanatajwa na asili yake:-
1. Ushoga ulitoka Ulaya.
2. Ubakaji ulitoka Ulaya.
3. Mlango wa KIA ulitoka Uarabuni.
NB. Waafrika waliishi bila nguo (nguo zililetwa na Mzungu) lakini hakukuwa na matukio kama haya au kama yalikuwepo basi ni kwa uchache sana ambacho hakitoshi kuhalalisha kuwa ni janga la dunia. Lakini hata hivyo leo watu wanaabudu kwa mfumo wa kigeni kwa kuvalia nguo zisizo na staha na kuibua mjadala mpya wa kimaadili.
Kwanini dini ihusike?
Kwa sababu Dini ndiyo ilitangulia ku-document mambo hayo kwenye Misahafu, Sheria za nchi dhidi ya maovu hayo hazikuwepo (zimetungwa hivi karibuni) na mila na desturi za asili hazikusisitiza dhidi ya maovu hayo kwa sababu ama hayakuwepo au yalikuwepo kwa uchache sana.
Aidha, nadhani adhabu kali haziwezi kumaliza kadhia hii, tunayo sheria kali ya ubakaji lakini bado Madawati ya Jinsia kwenye vituo vya Polisi yanapokea kesi nyingi sana. Watu wanachomwa moto wa matairi lakini bado. Kwenye Biblia kuliwa na kupigwa mawe hadi kufa, kufungwa jiwe la kusagia shingoni lakini bado akina Mfalme Daudi, Abimeleki walichepuka.
Daudi alichepuka mana alijua mfalme yupo juu ya Sheria. Ndio maana Mungu aliingilia kati na kumwadhibu mana hapakua na mtu wa kumwadhibu mfalme.
Wanawake wanakua bidhaa ya kujiuza na kutafuta kipato Kwa zinaa mana Kuna kitu kinaitwa haki sawa. Lakini hakuna shujaa mbele ya adhabu ya kufa.
Kuna mwamba alikaa madarakani miaka mitano TU nchi ikanyooka kwasababu ukikaidi unapitezwa fasta unaacha familia yako. Kila mtu akawa na hofu. Tatizo hata kesi za kubaka ni rushwa. Adhabu ikiwa Kali na rushwa inakua kubwa hivyo inageuka kuwa ni dili badala ya kudhibiti vitendo hivyo.
Sheria ya ubakaji hata mtu akipata ngono Kwa ahadi ya madaraka au cheo Huko ni kubaka. Je,ni wangapi wanabakwa Kwa manufaa yao ? Mashuleni,vyuoni na makazini Kwa kuahidiwa kupewa haki kwa Upendeleo?
Adhabu Kali inaondoa makosa kama rushwa itaondoka. Hakuna Sugu wa kufa. Vibaka wangekatwa mikono kama Mila nzuri za kiislam zinavyoelekeza wizi ungeisha kabisa. Kuna nchi hakuna wizi na maendeleo ni makubwa. Tanzania watu wanaambiana bila wizi huwezi kutoboa.
Matatizo ya Waafrika ni zao la viongozi wa bovu na sio Ukoloni. Wakoloni wameondoka miaka mingi na hatukusikia kuwa walikua wanaibia serikali zao ili wajilimbikizie Mali tofauti na Sasa viongozi Wanapeana ulaji kupitia ofisi za umma