Dini zinamilikiwa na Wazungu au Waafrika?

Sheria Kali ikitekelezwa ndugu yangu watu wanabadilika.

Daudi alichepuka mana alijua mfalme yupo juu ya Sheria. Ndio maana Mungu aliingilia kati na kumwadhibu mana hapakua na mtu wa kumwadhibu mfalme.

Wanawake wanakua bidhaa ya kujiuza na kutafuta kipato Kwa zinaa mana Kuna kitu kinaitwa haki sawa. Lakini hakuna shujaa mbele ya adhabu ya kufa.

Kuna mwamba alikaa madarakani miaka mitano TU nchi ikanyooka kwasababu ukikaidi unapitezwa fasta unaacha familia yako. Kila mtu akawa na hofu. Tatizo hata kesi za kubaka ni rushwa. Adhabu ikiwa Kali na rushwa inakua kubwa hivyo inageuka kuwa ni dili badala ya kudhibiti vitendo hivyo.

Sheria ya ubakaji hata mtu akipata ngono Kwa ahadi ya madaraka au cheo Huko ni kubaka. Je,ni wangapi wanabakwa Kwa manufaa yao ? Mashuleni,vyuoni na makazini Kwa kuahidiwa kupewa haki kwa Upendeleo?

Adhabu Kali inaondoa makosa kama rushwa itaondoka. Hakuna Sugu wa kufa. Vibaka wangekatwa mikono kama Mila nzuri za kiislam zinavyoelekeza wizi ungeisha kabisa. Kuna nchi hakuna wizi na maendeleo ni makubwa. Tanzania watu wanaambiana bila wizi huwezi kutoboa.

Matatizo ya Waafrika ni zao la viongozi wa bovu na sio Ukoloni. Wakoloni wameondoka miaka mingi na hatukusikia kuwa walikua wanaibia serikali zao ili wajilimbikizie Mali tofauti na Sasa viongozi Wanapeana ulaji kupitia ofisi za umma
 
Wengine tunaamini ni utapeli wa kiimani na kiroho.
Maisha ni kuamuwa tu, amini chochote na kuabudu hata ng'ombe poa tu, ila tahadhari, fuata sheria za nchi bila shuruti ama sivyo utaishia pabaya
 
Dini ni biashara ya uchuuzi wa sadaka kutoka afrika kuelekea roma. Na bado biashara hii ina nguvu zaidi afrika.
 
Whaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaat.....?

Is this a new revelation?

Why not preached and taught in everyday life?

My friend! won't they behead you for this secret and bitter truth?
Hakuna mtu anayeweza kujitokea kuyafundisha haya ni kudanganyana tu ndo wanajua
 
Unasema "babu zetu wasingewepanda wamissionary kama wengukua wabaya".
Unasahau, wamissionary walifika na zawadi na tabasamu wakihubiri tu neno. Wamissionary hawakuingia na bunduki, bali zawadi na tabasamu kwasababu nia yao walifika ili watuchunguze. Wakajifanya ni marafiki. Lakini nyuma ya pazia walirudi kwao na kupeleka taarifa zilizotuletea matatizo na walijua serikali zao zingetufanya nini baada ya wao kurudi nyumbani na kupeleka taarifa.
.
Muafrika ni mtu rahisi sana kurubunika, cheki wewe maskini wamekurubuni hadi unawepanda wakoloni na huambiliki chochote. Matokeo yake wanakudharau tu. Inasikitisha sana😔
 
Kwahiyo hawa Waafrika na wengineo nisiowataja walikuja kusaliti uaminifu wao kwa wakoloni hawa waliowapa uhuru na vyeo vya Urais na Uwaziri Mkuu?

Mandela vs State President C.R. Swart 1962 and Pik Botha 1990.

Mugabe and Canaan Banana vs Ian Smith.

Kaunda and Banana, Mugabe vs Cecil Rhodes.

Nyerere vs Sir Richard Turnbull.

Karume and Nyerere vs Sultan Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said.

Oginga and Kenyatta vs Sir Patrick Muir Renison.

Obote and Mutesa II vs Sir Walter Coutts.

Hahahaaaa..... "...wanabakwa kwa manufaa yao..." hahahaaaa.....
 
First year ana miaka 17 anabakwa ili asipate sup. Akikataa anafeli anarudi mtaani jamii haimsikilizi inamcheka na wengine wanadiriki kumwambia acha ujinga kwani ataondoka nayo ,mtumikie kafiri upate mradi wako.
Akienda Polisi ,anaombwa ngono( anabakwa Tena) asaidiwe kesi yake. Akienda Kwa wajuu yake naye anamwambia nikubalie Mimi mana yule yupo chini yangu hawezi kukusaidia. Akienda Kwa mkuu kitengo naye hamsikilizi mana hua anambaka secretary ili ampe safari na posho.
Akienda mahakamani anakutana na hakimu aliyekua amebakwa ili asifelishwe kwenye mitihani. Ni jamii iliyojaa waovu wenye nguvu kifedha ,kielimu na kimadaraka.

Sheria Kali inayosimamia Kwa haki bila Upendeleo ni mwiba Kwa waovu.
 
Mugabe alikua ni kuwadi wa Mabeberu Kwa muda mrefu mpaka vilipoanzishwa vyama vingi ndipo akaona wananchi wamemchoka. Akataifisha mashamba ya Wazungu akawagawia maafisa wa juu wa Jeshi na Polisi na usalama wa Taifa kama rushwa ya kuwadhibiti wapinzani na wageni. Katiba ikamlinda. Akavuruga nchi zaidi na kuvuruga uchumi.
 
Kwahiyo maisha by 90% ni kubakana tu hadi Makleri na Maustaadh nao wanabaka siku hizi. Tukimbilie wapi?

Ndiyo maana Afrika Kusini wameona bora yaishe wakaja na sheria ya mwanamke kuolewa na wanaume wengi kwa wakati mmoja na mwanaume kuoa wanawake wengi kwa wakati mmoja (hakuna idadi kama zile ndoa za Kikristo na Kiislamu).

Sheria kali zinafifishwa kwa kudurusiwa (reviewed) na utawala mpya unavyoingia. Enzi ya Magufuli ela za serikali ziliogopwa kama Corona kwa sababu ya sheria kali, leo hali siyo hiyo, ela za serikali ndiyo tamu.... kama bia za bar, zinawindwa hata gizani kuliko ela za sekta binafsi.
 
Makleri, Maustaadh, Mitume na Manabii nao siku hizi tunasikia wanabaka eti.

Nafikri ndiyo maana Papa wa kwanza labda aliona akaweka sera ya Useja (Celibacy) na kuweka laana ndani ya sera hiyo. Kwa laana hiyo, Mtawa au Kleri akizaa lazima mtoto anakuwa chizi tuuuu...... hivyo watu wenye roho za Uyezebeli (Ukahaba) wanawakwepa sana Makleri na Watawa kwa kuogopa kuzaa watoto machizi,
 
Dawa ni Moja TU watu wema kuungana dhidi ya waovu.
Waovu wachache hua wanatumia mbinu nyingi kuwatesha watu wema mpaka wanaufyata.
Mfano ni Mitaani unakuta vibaka wapo Wawili wanasumbua mtaa wenye Wakazi mia Tano . Wanajifungia ndani na mageti na sengenge . Badala ya wengi kuungana na kuwakamata vibaka Wawili na kukata viweko wao ndio wanatishwa na vipanga viwili badala ya kutoka na Mashoka na mishale na kuwawinda vibaka mtaa ukabaki salama.
 
“For evil to flourish, all that is needed is for good men choosing to do nothing, [Burke, E. 1756]”
 
HV yanaukweli haya lkn
 
HV yanaukweli haya lkn
Kuna mmoja yuko Matembele Dsm, kumuona ili akuombee lazima ufanye booking kwa 300,000/, anakiita kiasi hicho kama ni Consultation Fee. Yesu na Mitume kuwaona ilikuwa ni bure.


Taswira kwa hisani ya google.
 

Sio KILA ulichodanganywa kwenye somo la historia ni sahihi,mengi yalijaa chuki dhidi ya weupe.
Missionary awakuja kuchunguza wao walileta dini kwa maagizo ya Yesu Kristo ambae hakuwa Mzungu.
Wakaja wakakuta dini za jadi ni dhaifu kuweza kushindana na dini mpya.
Hii ni nature kwenye competition ya kiimani imani bora ndiyo inasimama.
 
Kuna mmoja yuko Matembele Dsm, kumuona ili akuombee lazima ufanye booking kwa 300,000/, anakiita kiasi hicho kama ni Consultation Fee. Yesu na Mitume kuwaona ilikuwa ni bure.

View attachment 2134160
Taswira kwa hisani ya google.
Anapingana na maagizo ya Yesu,Yesu aliagiza injili isiuzwe anaeuza injili hao ni mawakala wa kuzimu utumia white magic kutenda miujiza.Ukimjua Mungu ukiyajua maandiko utakuwa huru wala uhitaji nabii au mganga wa kienyeji kutatua shida zako.
Wengi ni wateja wa mitume na manabii sababu ni vipofu awataki kujifunza maandiko KILA kitu kipo wazi.
Mtumishi yeyeto anaetoza pesa Ili akuombee au akuuzie upako huyo ni agent no 666

 
Ubaya wa historia kuhusu wakoloni huwezi kuthibitisha kwamba wamissionary walikua na nia njema. Utanipa tu story na wewe ulizodanganywa.

Wewe unathibitisha vipi yesu alitoa hayo maagizo zaidi tu ya kusimuliwa hadithi na kupewa biblia ambazo ni madai ( claims) ya watu kuwa ni neno la Mungu.
Yani sisi tupo Tanzania alafu wanakuja watu wanasema wanatuletea maagizo ya Mungu na wewe unaona ni sahii🤦🏾‍♂️
 
Mkuu rejea kwenye vitabu tena...ukristo umeanzia ulaya..kuna tofauti kubwa kati ya yesu na ukristo...!!kimsingi yesu hakuwa mtu wa bara ulaya lkn pia hakua mkristo!!ukristo umetoka bara ulaya hata yesu mwenyewe haujui ukristo maana umeanzishwa mwishoni mwa karne ya 3 baada ya yesu kupigwa zake huko na kuuwawa kwa sababu alikua akipinga dola ya urumi..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
kijana historia imeandikwa na hao hao wazungu!

Jarbu kufanya hivi.
kuanzia sasa futa yooote ambayo ulifundishwa ukiwa kama mtumwa na anza kujifunza upya yale ambayo hawakutaka ujufunze.
mfano. Magic, Numerology, demonology, AstrolOGY.

NA YOTE KWA YOTE JIFUNZE TRUE AFRICAN HISTORY,
Hapa kuna waafrica ambao hawana ajenda yoyote zaidi yakutaka wewe ujue wapi ulipotoka wapo wengi wana historia wa kiafrika wameandika vitabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…