Msingeshindana kufungua nyuzi za kuponda wanaoamini katika Dini, Nyie mkipewa mamlaka ndo mtakuwa wa kwanza kuchoma nyumba zote za ibada
Binafsi nimekuwa mtetezi wa uhuru wa kuamini na kuabudu, pamoja na wa kutoanini na kutoabudu, kwa watu wote.
Mara nyingi tu, nilisema hii ni haki ya kikatiba, ni haki ya kiutu, imewekwa kwenye mikataba ya kimataifa, mpaka kwenye Universal Declaration of Human Rights.
Nilitoa mfano wa kupinga msimamo wa rais Kagame aliposema kuwa wachungaji wa makanisa wawekewe sharti la kuwa na degree ya chuo kikuu, nikisema sharti hilo linaingilia uhuru wa kuabudu.
Nilienda mbali kabisa na kusema kuwa, kimsingi, uhuru wa kuabudu ni upande mmoja wa shilingi ile ile ambayo upande wake wa pili ni uhuru wa kutoabudu., hivyo, kumvunjia mtu uhuru wake wa kuabudu, kutapelekea mmomonyoko wa uhuru wangu wa kutoabudu.
Nilisema pia, ingawa mimi si muumini wa dini yoyote na siamini hata katika uwepo wa Mungu, nitasimama na wanaoamini kat8ka kutetea uhuru wao wa kuabudi.
Kuna siku nilipata matatizo kutoka kwa jamaa mmoja atheist ambaye uelewa wake kwenye hiki suala ulikuwa finyu.
Rekodi za JF zipo, zitaonesha haya yote.
Naomba unitoe katika hilo kundi na uelewe kuwa dhana yabkwamba kila atheist anataka kuchoma na kufungia makanisa na misikiti ni dhana potofu.
Naweka mfano mmoja wa post hizi, huu ni wa August 2023.
Post in thread 'Rais Paul Kagame aahidi kuwasweka gerezani mahujaji wa Kikatoliki wanaotukuza ufukara'
Rais Paul Kagame aahidi kuwasweka gerezani mahujaji wa Kikatoliki wanaotukuza ufukara