Dini zingesambazwa kama ambavyo Atheism inasambaa sidhani kama zingekuwa na wafuasi wengi hivi

Dini zingesambazwa kama ambavyo Atheism inasambaa sidhani kama zingekuwa na wafuasi wengi hivi

Ndio ni mtazamo wangu kutokana na uelewa wangu na jinsi navyoona hoja za hao atheists ambazo kwa kiasi kikubwa zinaishia katika mitazamo ya kidini zaidi kuliko suala la kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu na ndio maana wale wasio na dini ila wanaamini Mungu huwa hawana shida na hoja za atheists maana zinashambulia dini zaidi.
Cha kushangaza wakristo wenye dini mbele ya waislamu ni wapagani na waislamu wenye dini mbele ya wakristo ni wapagani .
 
Kama na umri huu hujui kuzikwa kikristo kukoje pole .
Akiwa hai alikua anapinga uwepo wa Mungu ila alivyokufa alikubali uwepo wa Mungu akazikwa kikristo , mzee unachekesha sana.
 
Yoshua alisimamisha jua, ukoma ni laana kutoka kwa Mungu , sayansi imesaidia uelewe nini apo?
Yani Yoshua kasimamisha jua, wakati jua lenyewe limesimama. Au hapo zamani jua lilikuwa Linamove, na Joshua ndiye aliyelisimamisha??
 
Me nilianza na kujiuliza, kama huko Mbinguni kulitokea vita kati ya malaika waasi (shetani) na majeshi ya malaika wa Mungu.

je, walitumia silaha ya aina Gani? Ukiisoma na kusikia story ya vita huko mbinguni utaona walitumia silaha Fulani. Sasa, unatumia silaha kwa lengo lipi wakati unayepigana Naye Hawezi kufa (wanasema malaika ni roho na roho haifi). Au walitumia maombi/sala maana yake Kuna wahubiri wanafundisha silaha ya kumshinda shetani ni maombi, Yani malaika wa Mungu walikuwa "wanakemea", "kunena kwa lugha", etc ili kumshinda shetani

Na kama Mungu kumtoa shetani huko mbinguni ilibidi iwe vita, je, unadhani sisi wadhambi na kiongozi wetu shetani tutakubali kuchomwa moto na Mungu. Yani Mimi unanipeleka eti jehanamu nikachomwe moto alafu "nisikinukishe", thubutuu!!
 
Stalin serikali yake ni Atheist government na watu waliuliwa sababu ya dini zao na kuwa forced Atheist, Fascism na Communism zote ni Atheist ideology ama hufahamu? Ukipenda boga penda na ua lake.

Soma hapo inaelezea vizuri kabisa

Ndio maana nimekuambia utakuwa unachanganya utekelezaji wa siasa za kikomunisti na masuala ya atheism
 
Kumbuka kutoka zero [emoji1787][emoji1787]...India wamevunja msikitini juzi tu hapana wanakosa wafuasi...

Inasambaa ni mpango wa Mungu.
Kumbuka china inapakana na afaghstan, Pakistan na nchi nyingine za kiislamu na waislamu wengi wanapatikana mipakani mwa china kwenye nchi za kiislamu.

Nchini china Kuna wakristo takribani million 60 sawa na asilimia 2% na waislamu milioni 20 sawa na asilimia 1% kwa makadirio.

Ukristo ndio dini inayosambaa kwa Kasi nchini China kuliko dini yeyote.
Uislamu ndio dini inayopigwa vita sana na serikali ya kikomunist ya China.
 
Mimi binafsi ukianza kunisifiasifia kwa muda mrefu, unanishangilia, unaniombaomba msaada, unanililia, sometimes hata kukaa karibu yangu muda mrefu nakuona kero.

Lakini Mungu eti anapenda. Yani kwa kifupi Mungu anapenda machawa. Yani Mungu ameniumba ili apate kiumbe wa kumuinamia (kumuabudu) Yani amekaaaa, akafikiriaaa akasema ngoja nimuumbe binadamu ili aniabudu, kwa lugha nyingine Mungu aliamua aumbe machawa.

Nina maswali mengi kichwani, nikiamua kuandika yote nitajaza server za jf
 
Cha kushangaza wakristo wenye dini mbele ya waislamu ni wapagani na waislamu wenye dini mbele ya wakristo ni wapagani .
Kwani ulitaka iwe vp au hoja yako ni ipi hapo? Cha kushangaza hoja kama hizo ndio hoja za atheits ndio maana mie nasema sijaona hadi sasa hoja za msingi za atheists.
 
Kwanza atheism si dini, hivyo haina mtume wala "mtu wetu".

Pili, hizo habari hazithibitishiki. Yani kuna nesi aliripotiwa kusema kuwa Voltaire alisema hivyo wakati anakufa. Nurse hana hata mtu wa pili kuwa shahidi wa ku corroborate story. Maana yake nesi anaweza kuwa muumini aliyetaka kupandikiza maneno kwa Voltaire tu.

Hearsay, baseless, unfounded, unverified, uncorroborated claim.

Lakini zaidi ya yote, hata kama Voltaire alisema hayo kweli, atheism haiendeshwi na maneno ya mtume mmoja, kila mtu ana akili zake na anapima mambo kimantiki mwenyewe. Na Voltaire kafa zamani sana wakati mambo mengi hayajagunduliwa, kwa nini tujali alichosema Voltaire?

Hizo tabia za kujali walichosema mitume wa zamani ni tabia za dini. Hizo ndizo tabia ambazo atheists wanazikataa katika dini.

Sasa kwa nini unataka kuturudisha katika dini kusujudia maneno aliyoyasema mtu aliyekufa mwaka 1778?

Kumalizia, moja ya vitu ninavyopenda katika atheism ni kukataa logical fallacy ya appeal to authority. Tunakataa authority ya Mungu, mitume, Voltaire. Tunakwenda na reason.

Sasa katika ulimwengu huo, hata ukimchafua Voltaire, hilo si muhimu kwetu, kwa sababu hatuendi kwa authority ya mtu, tunajua kufuata authority ni logical fallacy.

Tunakwenda kwa reason.
Umefafanua vizuri
 
Kumbuka china inapakana na afaghstan, Pakistan na nchi nyingine za kiislamu na waislamu wengi wanapatikana mipakani mwa china kwenye nchi za kiislamu.

Nchini china Kuna wakristo takribani million 60 sawa na asilimia 2% na waislamu milioni 20 sawa na asilimia 1% kwa makadirio.

Ukristo ndio dini inayosambaa kwa Kasi nchini China kuliko dini yeyote.
Uislamu ndio dini inayopigwa vita sana na serikali ya kikomunist ya China.
Nchi zote dini zimesambaa wewe jidanganye😅😅
 
Me nilianza na kujiuliza, kama huko Mbinguni kulitokea vita kati ya malaika waasi (shetani) na majeshi ya malaika wa Mungu.

je, walitumia silaha ya aina Gani? Ukiisoma na kusikia story ya vita huko mbinguni utaona walitumia silaha Fulani. Sasa, unatumia silaha kwa lengo lipi wakati unayepigana Naye Hawezi kufa (wanasema malaika ni roho na roho haifi). Au walitumia maombi/sala maana yake Kuna wahubiri wanafundisha silaha ya kumshinda shetani ni maombi, Yani malaika wa Mungu walikuwa "wanakemea", "kunena kwa lugha", etc ili kumshinda shetani

Na kama Mungu kumtoa shetani huko mbinguni ilibidi iwe vita, je, unadhani sisi wadhambi na kiongozi wetu shetani tutakubali kuchomwa moto na Mungu. Yani Mimi unanipeleka eti jehanamu nikachomwe moto alafu "nisikinukishe", thubutuu!!
Kwahiyo hapo ndio ukaona uwe atheist na si kuacha kuamini dini au kuwa agnostic?
 
Kwani ulitaka iwe vp au hoja yako ni ipi hapo? Cha kushangaza hoja kama hizo ndio hoja za atheits ndio maana mie nasema sijaona hadi sasa hoja za msingi za atheists.
Nan kasema apo nimetoa hoja ? Ya ki atheist,
 
Mimi binafsi ukianza kunisifiasifia kwa muda mrefu, unanishangilia, unaniombaomba msaada, unanililia, sometimes hata kukaa karibu yangu muda mrefu nakuona kero.

Lakini Mungu eti anapenda. Yani kwa kifupi Mungu anapenda machawa. Yani Mungu ameniumba ili apate kiumbe wa kumuinamia (kumuabudu) Yani amekaaaa, akafikiriaaa akasema ngoja nimuumbe binadamu ili aniabudu, kwa lugha nyingine Mungu aliamua aumbe machawa.

Nina maswali mengi kichwani, nikiamua kuandika yote nitajaza server za jf
Mkuu eleza kwanini kudai hakuna Mungu ni sahihi na ndio ukweli wenyewe tofauti na kuamini Mungu au kuwa agnostic? Hicho unachokifanya hata mtu asiye na dini ila anaamini mungu anaweza kufanya.
 
Kwahiyo hapo ndio ukaona uwe atheist na si kuacha kuamini dini au kuwa agnostic?
Me sipendi kujiita atheist, me naishi kawaida TU kiubinadamu nikiongozwa na falsafa ya humanity.
Zamani nilikuwa too spiritual, ilibaki kidogo niingie seminari kuu, lakini baadae nilipoanza kuamua kujudge Kila kitu kinachohusu dini, kama mtu aliyekutana na mmisionari Kwa mara ya kwanza. Niliona Kuna vitu vingi havipo sawa Kwa myazamo wa kimantiki.

Unaweza ukajibu baadhi ya maswali niliyouliza kwenye post uliyoniquote??
 
Sasa atheists wana hoja nyengine zaidi ya kukosoa na kukebehi dini? Usahihi wao atheists ni kwa kutoa kasoro dini na kukebehi.
Dini imejegwa kwa misingi ya imani , habari za uwepo wa Mungu ni za kiimani tu , katika misingi hiyo lazima wawepo wasio amini hizo habari zisizothibitika .

Sasa kitu ambacho ni kila mtu anaamni tu bila uthibitisho ,utasemaje atheists hawana hoja ?
 
Mkuu eleza kwanini kudai hakuna Mungu ni sahihi na ndio ukweli wenyewe tofauti na kuamini Mungu au kuwa agnostic? Hicho unachokifanya hata mtu asiye na dini ila anaamini mungu anaweza kufanya.
Kuhusu kuamini Mungu kama yupo au hayupo Mimi jibu langu ni SIJUI.
Ukitumia logic utasema Mungu hayupo. Kama yupo (labda waliomuelezea Mungu kwa maandiko Kuna vitu walikosea) basi hawezi kuwa kama tunavyofundishana kwenye haya madini ya kigeni.

Je, kusema sijui kwamba Mungu yupo au hayupo ni makosa?? Ila ukisema Mungu yupo bila kuwa na uthibitisho ni sahihi??
 
Back
Top Bottom