Hili jambo ni nyeti kiasi kwamba inakuwa ngumu kukupa ufafanuzi mwingine maana naweza jikuta matatani kisheria.
Ngoja nijaribu kujilipua: Mfano kuna jambo system wameona jambo flani baya linafanywa na mamlaka ya juu na wakishauri lisifanyike hivyo au wakipewa amri walifanye lakini hawataki inabidi wakubali. Lakini kabla halijafanyika wanaona bora wavujishe kwa umma ili mamalaka ilazimike kusitisha (abort the mission) kisha wao wanakuwa wamelisaidia taifa lao bila kuingia matatani kama 'insubordinate' kwa mamlaka kwa kukataa kutekeleza amri au agizo.
Siri zingine huvujishwa kwa makusudi na sehemu ya wahusika kuokoa jambo baya lisitendeke au lisiendelee hasa kwa kioingozi mkali au asiyetaka kukubali kirahisi mawazo/ushauri ya/wa wasaidizi wake kimamlaka.