msomi uchwara
JF-Expert Member
- Oct 17, 2017
- 4,280
- 7,903
Huyu RPC wa sasa wa kanda maalumu ya DSM Mimi naona ndiye mtu sahihi kuwa next IGP
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yes alikuwa Boss wa Tiss kabla ya kwenda UN.Mahiga alishawahi kuwa mkuu wa TISS?
Hii nafasi ni Hamduni ndo anachukua. Siku hizi kuna kautaratibu flani usio rasm boss wa Tiss lazima apitie kwanza kuwa Boss wa Takukuru.
Augustine Lyatonga Mrema.Ni kipi kisa cha Kombe kuuwawa kwa risasi ?
Zamu yao mwendazake alikuwa na udini na ukabila walijaa wakristo watupu utadhani nchi yao peke yaoTeuzi sahivi ni ajili ya waislamu mkuu
Mtaumia sanaSahivi ni kujiita Mohamed au Athumani
Du nyerere aliwachagua wakristo watupuAngalia hapa kwa uzuri.
ORODHA YA WAKURUGENZI WAKUU WA 'TISS' TANGU UHURU.
Idara ya usalama wa Taifa (TISS) imeundwa kwa sheria ya bunge namba 15 ya mwaka 1996 (Tanzania Intelligence and Security Service act No. 15 of 1996) iliyosainiwa na Rais Benjamin Mkapa tarehe 20 mwezi Januari mwaka 1997. Sheria hiyo ndio inayoipa mamlaka Idara hiyo kufanya kazi zake ndani na nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Pamoja na idara hii kusajiliwa kisheria mwaka 1996, lakini ilkuwepo tangu wakati wa utawala wa kikoloni chini ya ofisi ya Gavana wa Tanganyika. Baada ya Uhuru mwaka 1961 ilihamishiwa ofisi ya Rais.
Tangu idara hii kuanzishwa hadi sasa imeongozwa na Wakurugenzi 9 akiwemo Diwani Athumani Msuya aliyeapishwa jana.
Wa kwanza ni mzee Emilio Mzena, huyu aliongoza mwaka 1961 hadi mwaka 1975. Ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza idara hii kwa miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14). Aliaminiwa na Mwalimu Nyerere baada ya idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua.
Wa pili ni Dr.Lawrence Gama (PhD). Huyu alipokea kijiti kutoka kwa Mzena. Aliongoza kwa miaka mitatu tangu mwaka 1975 hadi mwaka 1978, kabla ya Mwalimu Nyerere kumuondoa katika nafasi hiyo na kumteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma.
Wa tatu ni Dr.Hassy Kitine (PhD) ambaye aliongoza idara hii kwa miaka miwili toka mwaka 1978 hadi 1980. Kitine alichaguliwa kuongoza idara hiyo nyeti akiwa kijana wa miaka 36 tu. Anakumbukwa kwa jinsi alivyoiwezesha TISS kushirikiana na Idara ya Usalama na Utambuzi Jeshini (MI) Chini ya Meja Jenerali Tumainieli Kiwelu, kuiteka nyara ndege ya makomandoo kutoka Libya iliyokuja kumsaidia Idd Amin katika vita ya Kagera.
Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alimteua kijana mwingine mwenye miaka 35 Dr.Agustine Mahiga (PhD) - ambaye ni waziri wa sheria kwa sasa - kuwa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TISS. Alikaimu nafasi hiyo hadi mwaka 1983, Nyerere alipomuondoa na kumteua Kaimu Balozi wa Tanzania (Minister Plenipotentiary) nchini Canada.
Baada ya Mahiga kwenda Canada, Mwalimu Nyerere alimteua Luteni Jenerali Imrani Kombe kuwa Mkurugenzi mkuu wa 5 wa TISS mwaka 1983. Nyerere alipong'atuka alimuacha kombe kwenye idara hiyo na alidumu hadi mwaka 1995.
June 30 mwaka 1996 Jenerali Kombe aliuawa na Jeshi la polisi kwa madai kuwa walifananisha gari lake (Nissan Patrol) na gari iliyokua imeibiwa na mtuhumiwa Ernest Mushi maarufu kama "White".
Alimininiwa risasi 4 kifuani licha ya kushuka kwenye gari na kunyoosha mikono juu kama ishara ya kusurrender. Askari waliohusika na mauaji hayo walihukumiwa kunyongwa lakini Rais Kikwete aliwapunguzia adhabu mwaka 2011. Bado kifo cha Jenerali Kombe kina maswali mengi kuliko majibu.
Baada ya Kombe kustaafu alifuata Kanali Apson Mwang'onda. Huyu aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 6 wa TISS ambaye aliongoza idara hiyo hadi mwaka 2005 alipostaafu. Kanali Mwang'onda anasifiwa kwa kuifanyia marekebisho makubwa idara ya TISS ya kimfumo na kiutendaji. Ndiye aliyewezesha muswada uliounda sheria ya TISS mwaka 1996.
Mwaka 1980 Mwalimu Nyerere alifanyiwa jaribio kubwa la kutaka kupinduliwa na baadhi askari wa JWTZ (akina Tamin, McGhee na Kepteni Maganga) . Hili lilikua jaribio la 3 kubwa la kumpindua Nyerere, lakini ni jaribio la 7 katika orodha ukijumlisha na mengine madogo. Kanali Apson Mwang'onda akiwa Mkurugenzi wa ndani wa TISS (DOI) alifanikiwa kuzima jaribio hilo. Historia hii ilimuongezea sifa ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa TISS mwaka 1995.
Mwaka 2005 Rais Jakaya Kikwete alimteua Othman Rashid kuongoza idara hiyo hadi mwaka 2016 alipostaafu. Othmna Rashid alikuwa Mkurugenzi wa 7 wa idara hiyo.
August 24 mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Mchungaji Dr.Modestus Kipilimba (PhD) wa Kanisa la City Harvest Church la jijini Dar es Salaam kuwa Mkurugenzi Mkuu wa 8 wa TISS. Kabla ya uteuzi huo Kipilimba alikua Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA).
Mchungaji Dr.Kipilimba amedumu katika nafasi hiyo hadi 12 September 2019 alipotenguliwa uteuzi wake na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi CP Diwani Athumani Msuya.!
Credit: Malisa
Meza chupa sasa ndio waislam wanachaguliwaMpuuzi wewe kwahiyo watanzania wenye uwezo ni waislamu pekee? mhate dingi ako na siyo mimi
Huyo baba yako wa taifa ndio muasisi wa udini Tanzania wakurugenzi wake wa tiss wote wakrstoUkiwa unaitwa Mohamed au Athuman hata kama huna sifa,utateuliwa ktk nafasi yoyote.Tunakoelekea siyo kuzuri.Baba wa taifa alikuwa hapendi kabisa mambo ya udini na ukabila.
Mafisidi wote wagalatiaWavivu wakubwa nyie
apson na diwani hawakai category moja.. mbingu na ardhiHata hivyo historia haita msahau diwani na apson, lakini diwani akumbukwe aisee!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Bramo , huyo Suzy, sio tuu ni binti wa Mama Kamm, bali Mama yake mzazi ni Jaji Mstaafu Salome Kaganda aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi, huyu mama ni Mama Maadili mpaka kwenye damu, hivyo wamelelewa kimaadili, hivyo ili kukusaidia to save ya voucher na time, sikupi namba yake to help you na maimivu, utajisumbua bure na kuishia kuumia bure.Lete Namba ya Suzy Mkuu