Dk. Jonh Pombe Magufuli achukua fomu kugombea urais wa Tanzania

Dk. Jonh Pombe Magufuli achukua fomu kugombea urais wa Tanzania

Hili nalo jizi tu.yaan huu mwaka kura yangu ni ukawa tu
 
Jembe la ukweli hilo, Magufuli ndio mwente track record anayeweza kututoa point A mpaka B kwa slope iliyo chanya.[/QUOTE
]
Huyu bwana hajamaliza hata mwezi kazini tayari anashambulia wanasiasa.

Prof.Assad amehojiwa na idhaa ya Kiswahili ya UN, na kutoa madai kwamba Tanzania kuna tatizo la "POLITICAL ENTREPRENEURSHIP."

Anadai watu wanaendekeza faida binafsi ktk maamuzi yao wakiwa madarakani.

Amekwenda mbali na kusema ule mradi wa MAGUFULI wa kuuza NYUMBA ZA SERIKALI ni mfano wa "POLITICAL ENTREPRENEURSHIP."

Kwa kweli Professor atakaporudi nyumbani anapaswa at least aseme kuwa alinukuliwa vibaya, hata kama kuna ushahidi wa sauti yake.

Mahojiano yake yapo hapa chini, lakini specifically unaweza kuanzia dakika ya 6.

Tutatekeleza majukumu kukidhi matarajio: Profesa Assad | Idhaa ya Redio ya UM

Acha propaganda za kisiasa
Hivi kwa akili yako leo waziri wa utalii anaweza kuja na kusema, okay ngoja niuuze mlima kilimanjaro ama mbuga ya serengeti. Mambo mengine hayahitaji ku-argue.
 
Ripoti ya CAG kwenye wizara ya ujenzi bilioni 262 hazijukani zimekwenda sasa usafi wake uko wapi au ccm ukiiba unakuwa msafi kama yule wa monduli mnavyomsifia.

hahaha

Kwa ccm inaelekea ukiiba sana unatakasika.
 
ikulu sio wodi ya wagonjwa walioenda kwa babu wa loliondo wagonjwa wanaishi kwa kikombe cha babu ni shida kuwapa
 
Pole sana hata Mh.Pinda kajenga uwanja wa ndege Katavi na hata barabara ya Kizi - Kibaoni! hoji na wengine wengi tu acha kumshambuia Magufuli.

Kwa kuwa barabara hizo zimejengwa Tanzania na sio Burundi basi hakuna tatizo kabisa.

Yeyote atajayeleta hoja kama hii atakuwa ameishiwa, labda kama angekuwa anajenga barabara kwao tu, lakini Magufuli tumeshuhudia bajeti ya wizara yake anabalance pande zote za nchi.Miaka michache iliyopita waziri alivyokuwa Mramba nakumbuka wakati wa kipindi fulani alipeleka bajeti iliyojaa barabara za nyumbani kwake tu, ikaleta sana mgogoro bungeni.Kwa Magufuli sijawahi kusikia hiki.Yupo busy pande zote za nchi anahangaika na Barabara.

Kama tunachagua rais kwa record yake, basi hakuna kama Magufuli.Hao wengine tunaoona hawajakosea lolote serikalini kama akina Dr Slaa ni kwa sababu hawajawahi kuwa viongozi.

Tukiwajudge kwa uongozi wao ndani ya Chadema kuna uchafu mwingi kuliko uadilifu, na kama watu wanahoji taarifa ya CAG basi warejee pia taarifa hiyohiyo imesema kuwa Chadema mahesabu yao hayapo sawa, sasa tucoclude kuwa hiyi pesa Dr Slaa amekula?

Kuhusu nyumba, jana hiyo hoja imeelezwa kwa urefu sana na Sumaye, kaeleza mchakato mzima wa kufikia maamuzi yale,hakukuwa na uamuzi wa wizara, ilikuwa juu ya wizara.Maamuzi yale yalitokana na tume mbalimbali zilizoundwa na Rais, kwa miaka mingi tofautitofauti, na akasema kuwa uamuzi wa kuuza nyumba ulitolewa na Rais mwenyewe.

Ni muhimu tujitahidi kuwatendea watu haki.

Na ata kama Magufuli angekuwa amefanya uamuzi huo mwenyewe, bado yeye ni binadamu, hakuna mtu anayeweza kufanya maamuzi kwa miaka karibu 20 sasa serikali alafu asifanye ata moja la kukosea, ni binadamu sio malaika.Lazima kuna vitu binadamu atakosea, mpime kwa ujumla wake.Otherwise itabidi tuachane na wanadamu turudi misikitini na makanisani mpaka Mungu amshushe malaika mmoja aje kuwa Rais, maana kwa mwanadamu hayupo asiye na kosa ata moja.Hayupo!!
 
Loss zote zilizotokana na ufanyaji kazi wa Magufuli, kama vile kushika samaki, kuvunja nyumba na baadae serikali kuamuliwa kulipa, hiyo si kwamba Magufuli ndo alisababisha loss. Losaa ni wale walioshindwa kusimamia sheria ili serikali ipate faida kutokana na utendaji huo. Hii ni sawa na

MWAKYEMBE na BUNGE halikusababisha loss tuliyopata ama tunayoendelea kupata kwa sakata la RICHMOND, maana napo serikali ilishindwa ikalipa fidia na bado tunaendelea kulipa fidia.

Ningewaomba tutofauti mambo haya. Hata hivyo, MAGUFULI ndo chagua sahihi kwa wakati wote kwa kipindi chote hiki cha miaka 10.
Tusikubali kunyweshwa sumu kama tulivyonyweshwa sumu mwaka 2005, tukamkataa mgombea stahiki SALIM AHMED SALIM kwa kuendekeza ngojera zisizo na tija.
 
Ukweli ccm ni magufuli na Lowassa vinginevyo ukawa wanachukua mapemaaaa! Magufuli ana nafasi kubwa zaidi. Umri wake mzuri na mchapakazi. Kila wizara aliyosimamia imefanya vizuri. Anaheshimu sheria za nchi atasimamia katiba yetu.
 
huyu jamaa ni mchafu sana
eti barabara inatengenezwa klmt kadhaa akiwepo mpaka zinaisha anasema mbomoe ?????
ulikuwa wapi wakianza kilometa ya kwanza,ya pili????
hizi gharama ni za nani?????

angalia madudu ya kilwa road
barabara inatengenezwa mwaka sasa

mwaka?? zaidi ya miaka 4 haikamiliki
 
Ukiona jiwe limetupwa kwenye giza ukasikia kelele ujue limempata mtu.
 
ratiba ya jana ilionyesha hivyo..amechukua bila kutangaza nia aakijiamini kwamba watz wanajua utendaji wake...waache wamlete mwizi huyu ....lazima atwambie zile 268 bil zimeenda wapi

mwambie atuambie zile 262 za wizara ya ujenzi alipeleka wapi ripoti ya CAG hajaona hizo pesa zilifanyiwa nini?

Jembe huoni hata aibu kusema. Maeneo yote nyeti wameuziwa watu binafsi, including vimada wake e.g Kebbys Hotel. Wewe umekaa kushabikia upuuzi. Huyu mtu angekuwa China angekuwa ameshanyongwa siku nyingi

Ongeeni tu lakini watanzania wanamkubali sana na kazi yake wanaijua...karibuni october mgalagazwe na mwanaume huyo
 
huyu jamaa ni mchafu sana
eti barabara inatengenezwa klmt kadhaa akiwepo mpaka zinaisha anasema mbomoe ?????
ulikuwa wapi wakianza kilometa ya kwanza,ya pili????
hizi gharama ni za nani?????

angalia madudu ya kilwa road
barabara inatengenezwa mwaka sasa

We Maksai wa kike watu tushakula pesa za uncle EL tulia tufanye maamuzi kwa maslai mapana ya nchi! Ebo!
 
Back
Top Bottom