Hizi kodi za makadirio ndiyo zinatoa mwanya wa watumishi wa TRA kuchukua rushwa ambayo mida mwingine zinakuwa kubwa kuliko kodi zilizokadiliwa. Konteina moja lenye mizigo inayofanana mizigo iliyotoka sehemu moja lakini wafanyabishara wanalipa kodi tofauti. Wananchi wanaumia wanasiasa wanasifika mama anaupiga mwingi. Hali ni mbaya kwa kweli mtaani, wawakilishi wao wakiwasemea wanaonekana wanajiandaa na ubunge wa mwaka 25 ilimradi tafarani, chawa ndiyo wamekuwa watafiti wa uchumi, ndiyo maafisa jamii, chawa likiongelewa swala linalohusu jamii lakini linaigusa serikali basi watalidaka juu juu kwa kulikanusha kana kwamba hakuna kitu kinachoendelea, mambo ni shwari ila kinachoendelea ni wivu na wanaokiongea hawamtakii mema mh rais. Na wanamalizia na kauli yao. "Hali ni shwari, mama endelea kuupiga mwingi" wakati kiuhalisia hali ni mbaya mtaani.