Ni kweli na wala hujakosea, wengine sisi ni mbumbu ambao hatuna hadhi ya kuhoji mambo mazito kama haya. Marehemu Steve Jobs alisema maneno mazuri sana na sintayasahau ...STAY HUNGRY, STAY FOOLISH.
Mkuu, post yangu ya nyuma nimejirkeza kadiri ya uwezo wangu kwamba Marekani ikiachana na mfumo Keynesian tangia enzi za Nixon 70's. Rais ambaye aliyetaka kuufufua huo mfumo alikuwa Obama, lakini na yeye alipata shida kutoka na upande wa Republican kutaka pesa itumike kuokowa mabenki na capital investments na huku yeye Obama akitaka kusaidia watu wa kawaida aliopoteza kazi na wengine kushindwa kulipa mikopo ya nyumba nk. Kwenye kipengele hicho hicho nimesema mfumo Keynesian unadokolewa kidogo kidogo na rais aliye madarakani ili kuepusha uchumi kuyumba. Hapo ndio unaposema tax cut, lakini hiyo sio sababu ya kusema Marekani inatumia mfumo huu kuendesha uchumi wao wa kila siku au kila mwaka. Kama hivyo ni kweli, Biden anapanga kupandisha kodi na Trump amepunguza ruziki kwenda kwa wakulima na sekta zingine 2020, je na hapa bado kuna huo mfumo bado upo? Na kwa nini watumie huo mfumo wakati uchumi ulikuwa unaajiendesha wenyewe (pre Covid)?
The White House's 2020 budget plan to slash federal funding for farm subsidies and other safety net programs for agricultural producers is getting criticized by farmers who say they are already struggling.
www.cnbc.com
Humu JF Kuna watanzania wanaishi Marekani, ladba watowe ushuhuda kama infrastructure ya Marekani bado iko up to world stand au ndio mguu mmoja unachungulia kwenye kaburi. Tokea miaka ya 70, mimi sijaona uwekezaji mkubwa kama kwenye reli mpya, treni mpya super highway mpya. Ukilinganisha na nchi ndogo za Asia, Marekani wamejisahau kabisa kwenye nyanja ya miundo mbinu. Trump alijitutumua na msemo wake wa America First, akaahidi atafanya maajabu ya kurudisha viwanda, kujenga viwanda vipya, na hata kujenga reli nchi nzima. Mwaka wa nne huu, hata reliable 5G infrastructure ni shida. Hata Tanzania tumewashinda, tukichukulia ukubwa wa nchi yetu pamoja na ukubwa wa uchumi wetu, ndani ya miaka mitano tumeweza kuanzisha na kuendeleza major infrastructure projects tatu na zingine ziko kwenye pipelene.
The fabric of America is crumbling. The American Society of Civil Engineers (ASCE) gives the nation's infrastructure a D+ grade -- that's the roads and bridges we drive on every day, the airports we use for business and vacation travel, and the schools where we send our children to learn. And...
www.cnn.com
In the July-August 2017 edition, Tony Munoz, Publisher Editor-in-Chief of The Maritime Executive, w...
www.maritime-executive.com
Labda niseme tena, military spending can not and will not stimulate economy. Swali moja la kujiuliza kwani wanaojihusisha na jeshi (iwe kampuni binafsi za supply au hata wanajeshi wenyewe) wako wangapi? How can you compare agricultural spending with military spending in terms of value of return. Infact, kila $ inayokwenda kwenye matumizi ya kijeshi, ni pesa iliyopokonywa kutoka miradi mingine ya maendeleo ambayo ingeweza kuleta chachu kwenye uchumi.
https://www.investopedia.com/articles/investing/072115/how-military-spending-affects-economy.asp
Haya mambo ya kutumia PPP vs GDP kulinganisha pesa ya nchi moja kwa nyingine ndio kujuwa uchumi wa nchi unafananaje, ni maswali yenye utata mwingi. Nchi nyingi viwango vyao vya thamani ya pesa inashuka kulinganisha na walivyokuwa wanatumia zamani GDP. Kuna report inaonyesha Marekani hawajapishana sana na China kama walitumia PPP.
Hii hapa ni kauli yako:
Tatu, wewe siyo mtu mkweli au aidha huelewi nilichokisema: Tanzania hatuna Progressive Tax tuna Proportional Tax.
Makundi yote hulipa asilimia moja ya pesa katika vipato vyao, kama ipo hebu tupe mifano. Uchina ukiwa tajiri na kodi inaanza kuwa Progressive. Kafanye tafiti zaidi au kama unataka tuanze kuongelea kodi basi fungua uzi mwingine.
Sasa kama hatuna progressive tax, rate ya 9% to 30% inatoka wapi na nani anatakiwa kuilipa? Ukimuuliza Google kama Tanzania ina tumia progressive tax, atatoa majibu ya haraka sana.
Umeniuliza ruzuku ya Marekani ya trilioni moja nimeitoa wapi, jibu ni bajeti ya Marekani ya mwaka 2019 iko wazi kabisa.
In fiscal year 2023, the federal government spent $6.1 trillion, amounting to 22.7 percent of the nation’s gross domestic product (GDP). About nine-tenths of the total went toward federal programs;...
www.cbpp.org
Imeulizwa kama subsidies za US haziingiliani na masharti ya WTO....
Unafikiri kwanini USA wanamkataa yule mama MNigeria Ngozi asuchukuwe ukurugenzi wa WTO? America will protect America.